Hivi mtu kama huyu una deal nae vipi? ananizungusha kunilipa pesa yangu

patrickk

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2012
Posts
745
Reaction score
5,931
Iko hivi...

Kuna Mzee mmoja naheshimiana nae Sana, imepita kama muda alienda dukani kwangu kuchukua vifaa Kwa ajili ya kufanya finishing ya apartments zake anazojenga, akachukua vifaa vya 7,280,000/= ikaandikwa deni, sio mara ya kwanza kufanya hivo ni mtu nimeshafanya nae biashara muda mrefu Wala Hana shida, na huku Kanda ya ziwa matajiri wengi wanapenda hardware ambazo wanakopesheka then wanakuja kulipa badae, huyu Mzee pia ashaniletea wateja watachukua vitu then watalipa tu baada ya muda Wala sijawahi kupata tatizo nao

Sasa kama siku kumi zilizopita alinipigia Simu, kanitaarifu kua amepata msiba wa watoto wake wawili wa kiume walikua wametoka machimboni kakola wakiwa na pikipiki wakapata ajali wakafariki, akaniambia anaenda msibani ila pesa yangu amemuachia Kuna kijana hua anatembea nae nadhani ni dreva wake/manager anasimamia biashara zake(whatever the case).... Huyu kijana hua namuona nae mara Kwa mara!!! Dah, nikampa pole pale nikamwambia amwambie kijana aniletee million 7, hio laki 2 na 80 nikamwambia Mzee nimetoa kama rambirambi nipo na majukumu ningekua na muda ningekuja msibani..... Basi tukapeana pole pale tukaagana

Ikapita kama nusu saa napokea Simu namba mpya, akajitambulisha ni yule kijana wa Mzee Kuna pesa kapewa anipe, nikamwambia zipitishe dukani pale, akaniambia yupo mbali nimpe acc number ya nmb au crdb aniwekee, nikamtumia zote mbili....

Imefika kama saa 2 usiku napata sms ya nmb nimewekewa milioni 5, nikavuta subira pale, baada ya kama nusu saa nikampigia yule kijana akadai mahali ameenda hawakua na float ya kutosha hio million 2 Bado anayo anatafuta wakala mwingine aweke, nikamwambia sawa!!!

Nimekaa mpaka kesho naona kimya, nikampigia tena anasema nipe kama nusu saa ntakua nimeweka!!! Kimya.... Mpaka zikapita kama siku 3, Kila nikimpigia anapokea Kwa wakati tu ananiambia nakuwekea hio Hela ila haweki....

Tumeenda hivo hivo mpqka wiki ikaisha, the same routine, napiga Simu anapokea then anasema anaweka ila haweki, Kila siku anasema yupo mbali akifika mjini anaweka..... Sasa majuzi akaanza kutopokea Simu kabisa, nikaona kama red flags hapa!!! Kila nikimpigia hapokei hata nikijaribu namba zingine hapokei... Nikafanya upelelezi nikapajua kwake,nikaenda jioni sikumkuta nikamkuta mke na watoto... Nikauliza tu kama jamaa yupo wakasema hayupo ila mke wake akawa na mashaka kwanini sijampigia Simu kabla sijaenda, sikumwambia chochote nikawa nimeondoka zangu.....

Badae usiku jamaa kanipigia sijui alikua amelewa Kawa mkali kweli kwanini namfatilia mpaka kwake, nikamwambia kijana staki mazoea nataka pesa zangu akakata Simu badae akanitumia sms atapitisha pesa dukani ila akawa analalamika tu kwanini nimeenda kwake, sikumjibu

Mpaka Leo kimya na Simu hapokei kabisa, Sasa kuna jamaa yangu ni askari kuna Jana tumekaa tu mahali nikamgusia hii ishu akasema twende tu kwake na Tenga tukamchote, nikamwambia subiri kwanza

Nimeulizia Mzee tajiri wake Bado yupo msibani, nawaza kumpigia ila naona kama ntampa stress tu ukizingatia Bado yupo kwenye majonzi kupoteza watoto wawili sio mchezo......

Sasa option nilizonazo ni hizo mbili, either nimpigie yule Mzee niongee nae nimuelezee Kila kitu japo nae atanilaumu kwanini sikumpa taarifa mapema au huyu kijana ni deal nae mwenyewe tu,

What's the right approach???
 
Mtumie mzee message.....umepewa pesa nusu na kijana wake. Kisha anzia hapo.
 
Kwa kweli unazingua mkuu.

Huyo kijana hujafanya nae biashara yoyote na hakuna pesa unamdai.

Mzee unayemdai ndie anayepaswa kufuatilia sio wewe.
 
Mkuu hili jambo liliishaje? Na Mimi nimepata jambo linafanana na hilo!
 
Nipe hiyo kazi mzee tupo huku kwa Madiba hatuna kazin,njoo dm nikamalizane nae huyo mapema tuu
 
Back
Top Bottom