Hivi mtu mwenye imani ya Rasta anaweza kupata ajira serikalini?

Hivi mtu mwenye imani ya Rasta anaweza kupata ajira serikalini?

Serikali haiajiri dini ,inaajiri dini inaajiri mtu mwenye taaluma na maadili. Na watu hawawi na maadili ya utumishi kwa sababu ya dini zoa.

NAMPONGEZA SAANA PROFESA SAMIA SULUHU HASASAN KWA KUBUNI SALAMU YA KITAIFA ISIYO NA DINI Hakuna kitu kibaya kwa nchi yenye mchanganyiko kama ya kwetu kuingiza dini ,salamu za kidini kwenye hadhira yenye Imani tofauti. Wasemaji wa timu za miguu, na watangazaji wajitafakari wanapokuwa hewani waepike kabisa kudhani kuwa washabiki wao ni dini moja
 
Tatizo sisi watanzania tunajali apearance kuliko content/uwezo wa mtu, kuna watu ni vilaza humo maofisini lakini kwa kuwa wanamuonekano mzuri basi wamepewa kazi bila kujari kichwani hawana kitu
Wadau naomba kujuzwa hili maana Nina mjukuu wangu anasoma ndoto yake aje kuwa Dr na sisi ni rastafari je anaweza pata ajira
 
Kama akiwa ameshasoma na ni daktari anaweza kuweka hizo rasta maana sidhani kama udaktari wanaangalia sana muonekano kushinda utaalamu na uzoefu.

Ila kwa levo yake ya elimu kwa nijuavyo shule zetu za Tanzanihuwa wanalazimishwa kunyoa, sipati picha akifika form five kuwa kuna shule itamruhusu awe na nywele
Kama iman yake ni hyo hawezi kunyolewa.. Pia sometimes huwa wanakua na vibali maalumu..
 
Serikali haiajiri dini ,inaajiri dini inaajiri mtu mwenye taaluma na maadili. Na watu hawawi na maadili ya utumishi kwa sababu ya dini zoa.

NAMPONGEZA SAANA PROFESA SAMIA SULUHU HASASAN KWA KUBUNI SALAMU YA KITAIFA ISIYO NA DINI Hakuna kitu kibaya kwa nchi yenye mchanganyiko kama ya kwetu kuingiza dini ,salamu za kidini kwenye hadhira yenye Imani tofauti. Wasemaji wa timu za miguu, na watangazaji wajitafakari wanapokuwa hewani waepike kabisa kudhani kuwa washabiki wao ni dini moja
Profesa Samia!
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Profesa Samia!
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Ndio ni mgonduzi wa jambo jema lenye kuleta harmony na amani kwenye nchi.
Mwanzoni kwenye hafla za kiserikali na kijamii ilikuwa inachukua nusu saa kumsalimia Kila mtu na dini yake.

Lakini bado zilileta gumzo kwa nini salamu ya dini Fulani imeitangulia.

Kadhalila , unakutana na mtu mtaani tuu anajua kabisa Imani yako ila kakomaa SALAMALEKU, au BWANA YESU ASIFIWE ukimwambia anakuambia ooohh mara maana ya hayo maneno ni mazuri Sana , mazuri kwako.
Unakuta vyombo vya habari redio au television mtangazaji yupo hewani salamu anayosalimia jamii ni ile anayoitumia kwenye dini yake. Sio vyema na ndio maana nimempa u profesa Raisi wetu wa awamu ya sita kwa Ugunduzi wa salamu Bora kabisa kwa watu wote. Suala la salamu za dini zibakie misilitini na makanisani na mnapokutana watu wa Imani Moja tuu.
 
Mbona wapo marasta wanapiga mzigo serikalini japo ni wachache. Mmoja ninaefahamiana nae ni engineer mmoja mkubwa tu yupo mkoa mmoja kanda ya ziwa. Muda wote akiwa ofisini utamkuta kavaa yale makofia yao.
 
Hata Mimi Ni Rasta napitia changamoto nadhani huu utumwa wa fikra ndo inasababisha kujali mwonekano wa mtu na kuacha content
 
Back
Top Bottom