Hivi Mungu anapenda kelele?

Hivi Mungu anapenda kelele?

Nimesoma uzi mmoja wa Tycoon mmoja hapa Jf, anadai utafiti wake wa miaka 22 unaonesha Mungu wa walokole ndio ana nguvu kuliko Mungu anaeabudiwa na Madhehebu mengine.

Nimejaribu kuchunguza Mifumo wanayoitumia walokole wengi 100% katika ibada zao, maombi kiujumla huwa zimejaa kelele nyingi sana (elewa maana ya kelele wala sijadhihaki mtu)

Imefikia hatua wasipokua na umeme basi ibada huwa inapoa sana makanisani mwao.

Je, Bila kelele nyingi MUNGU hawezi kuinuka na kutetea watu wake dhidi ya shetani?
Hakuna Mungu katika uhalisia.

Mungu muweza wa yote mjuzi wa yote na mwenye upendo wote kwanini anataka tena hadi tumuombe??
 
Hujanijibu swali langu lakini

Sent using Jamii Forums mobile app
Jibu nimekupa indirectly kwamba hakuna vingine vina majina Ila tuna uwezo wa kuvihisi km upepo, harufu, nk

Je! Umewahi kumhisi Mungu kwamba hapa nimekaa na Mungu au hapa naongea na Mungu Ila haumuoni?

Km vile ambavyo ukikaa karibu na kinyesi unahisi kabisa hapa kuna mtu amekunya
 
Kwani we ni Mungu? Una uhakika gani Mungu ana mtazamo kama wako juu ya hizo unazoita kelele?

Je labda yeye haoni hicho unachoona wewe? Inawezekana kwako ni kelele kumbe kwake ni kawaida sana! Pengine kwake ni sauti ya chini kiasi hata hawasikii na anatamani hata waongeze sauti!

Zitakuwa kelele pale zinapokuwa si takatifu mbele zake! Kama ni za kinafiki hapo kweli ni kelele hata Kama wananena kimoyomoyo! Mawazo ya Mungu si sawa na mawazo ya mwanadamu! Wewe siyo Mungu, acha kumsemea Mungu!
Mbona hata na wewe ulichoandika hapa "Umemsemea Mungu""

#YNWA
 
Kwani we ni Mungu? Una uhakika gani Mungu ana mtazamo kama wako juu ya hizo unazoita kelele?

Je labda yeye haoni hicho unachoona wewe? Inawezekana kwako ni kelele kumbe kwake ni kawaida sana! Pengine kwake ni sauti ya chini kiasi hata hawasikii na anatamani hata waongeze sauti!

Zitakuwa kelele pale zinapokuwa si takatifu mbele zake! Kama ni za kinafiki hapo kweli ni kelele hata Kama wananena kimoyomoyo! Mawazo ya Mungu si sawa na mawazo ya mwanadamu! Wewe siyo Mungu, acha kumsemea Mungu!
Mbona Sasa ndicho unachofanya hapa, unamsemea Mungu

Sent from my Infinix X665 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom