Hivi Musa alikuwa Myahudi au Mwarabu?

Ww tatizo umekalili tu ila hufanyi uchunguzi uislam umeeanzishwa na Muhammad ila kwa kua we ni mfia din siwezi bishana na ww .Na km unaona waarabu ni bora kuliko sisi hujachelewa kaolewa huko na utumwa wako wa kukalilishwa upuuzi

Wakati wa Nabii Ibrahim Uislaam upo, na jufikiria Uislaam ni uarabu ni kwa mtu mpumbavu tu kama wewe ! Indonesia ina watu mil ±250 na wate ni waislaam na hamna mwarabu.
 
Safi kabisa kwa swali hilo ngoja tusikilize kitacholetwa tena.
 
.
 
Tusichanganye Biblia na quran ni vitabu viwili tofauti tusivifananishe tafadhali
Musa anayeongelewa na Biblia sio wa quran watu wawili tofauti na majira tofauti, habari ya Yesu na Isa bin mariam ni tofauti tusichanganye na kulazimisha ufanano wa hivi vitabu.
 
Sasa mbona kuna watu wanasema alikuwa Muislam

Kwa mujibu wa Uislamu Mussa (A.S) aliku ni muislamu.

Wanachoshindwa kufahamu watu wengine wasiokua waislamu ni kuwa wao wanahisi Uislamu umeletwa na Muhammad (S.A.W)

Kwa mujibu wa Uislamu Muhammad ni mtume wa mwisho katika mitume ya Allah. Na Mussa ni mmoja katika watume wa Mungu.
 
Je unafahamu kuwa Musa alikuwa Muisraeli kutoka kabila la lawi?
 
Majibu ya kweli yapo ndani ya Quran kitabu pekee Cha Mungu kilichobaki Duniani ambacho akina makando kando

Musu alikuwa Muislam

Quran 42:13 -
Amekuamrisheni Dini ile ile aliyo muusia Nuhu na tuliyo kufunulia wewe, na tuliyo wausia Ibrahim na Musa na Isa, kwamba shikeni Dini wala msifarikiane kwayo. Ni magumu kwa washirikina hayo unayo waitia. Mwenyezi Mungu humteua kwake amtakaye, na humwongoa kwake aelekeaye.

Na waliomfuata pia walikuwa waislam

Quran 7:121
- Wakasema: Tumemuamini Mola Mlezi wa viumbe vyote,
Quran 7:122
- Mola Mlezi wa Musa na Haarun.
Quran 7:123
- Akasema Firauni: Mmemuamini kabla sijakupeni idhini? Hizi ni njama mlizo panga mjini mpate kuwatoa wenyewe. Lakini karibu mtajua!
Quran 7:124
- Lazima nitaikata mikono yenu na miguu yenu mbali mbali. Kisha nitakutundikeni misalabani.
Quran 7:126
- Nawe hukuudhika nasi ila kwa kuwa tumeziamini Ishara za Mola Mlezi wetu zilipo tujia. Ewe Mola Mlezi wetu! Tumiminie uvumilivu na utufishe hali ni Waislamu.
 
kuwa kwake muisraeli hakumuondoi kutokua muislamu.
Nguzo za uislamu kipindi Cha Musa zilikuwa ngapi?

Zitaje kama zipo?

Zifafanue kama zipo?

Na je nguzo hizo za uislamu enzi za zamani ni sawa na za sasa?
 
wanakupotezea muda.. waulize Musa alizaliwa kipindi gani na uislamu umeanza lini? ni kama mashariki na kusini.. usipoteze muda wako kubishana na wanywa kahawa na stori zao.
Nyinyi wagalatia mmedanganywa sana
Wewe unajua uislam umeanza lini?

Sio Musa tu Hadi Babu zake akina Ibrahim Isaka na Yakobo wote walikuwa waislam

Quran 2:132
- Na Ibrahim akawausia wanawe, na pia Yaaqub: Enyi wanangu! Hakika Mwenyezi Mungu amekuteulieni Dini hii; basi msife ila nanyi mmekuwa Waislamu, wanyenyekevu.
Quran 2:133
- Je! Mlikuwapo yalipo mfikia Yaaqub mauti, akawaambia wanawe: Mtamuabudu nani baada yangu? Wakasema: Tutamuabudu Mungu
wako na Mungu wa baba zako, Ibrahim na Ismail na Is- hak, Mungu Mmoja tu, na sisi tunasilimu kwake.


Sasa kama Kuna mgalatia yoyote anaweza kutoa andiko katika kitabu chochote Cha Mungu litakalotaja dini ya Ibrahim Isaka na Yakobo kinyume na ilivuosema Quran kuwa walikuwa waislam aweke hapa hilo andiko

Na kama andiko hamuna jueni kuwa nyinyi mmedanganywa tena mmedanganywa mengi tu
 
Nguzo za uislamu kipindi Cha Musa zilikuwa ngapi?

Zitaje kama zipo?

Zifafanue kama zipo?

Na je nguzo hizo za uislamu enzi za zamani ni sawa na za sasa?

unaleta ubishi kwenye mambo ambayo ata uelewa nayo huna.
 
Nguzo za uislamu kipindi Cha Musa zilikuwa ngapi?

Zitaje kama zipo?

Zifafanue kama zipo?

Na je nguzo hizo za uislamu enzi za zamani ni sawa na za sasa?

Nguzo za uislam ni 5

1) kuamini Mungu ni mmoja na manabii wake

2) Kuswali swala 5

3) Kutoa zaka

4) Kufunga ramadhani

5) Kwenda kuhijo Maka

Hizo nguzo zote Musa alizifanya Kwa jinsi alivyoelekezwa na Mungu

Taja unayotaka hapo nikuonyeshe jinsi Musa alivyo ifanya kupitia kitabu Cha Taurati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…