2) Kuswali/ kuabudu
Kuhusu kufanya Ibada Kwa nabii Musa hilo halina mjadala labda je alikuwa anaabudu vipi
Kutoka 34:8
Musa akafanya haraka, akainamisha kichwa chake hata nchi, akasujudu.
Kutoka 34:9
Akasema, Ikiwa sasa nimepata neema mbele zako, Bwana, nakuomba, Bwana, uende kati yetu, maana ni watu wenye shingo ngumu; ukasamehe uovu wetu na dhambi yetu, ukatutwae tuwe urithi wako.
3) kufunga
Kumbukumbu la Torati 9:9
Na hapo nilipokwea mlimani kwenda kuzipokea mbao za mawe, nazo ni mbao za agano BWANA alilofanya nanyi, ndipo nikakaa mle mlimani siku arobaini usiku na mchana; sikula chakula wala kunywa maji.
Yoeli 1:14
Takaseni saumu, iteni kusanyiko la dini, Wazee na wakusanye wenyeji wote wa nchi; Waende nyumbani kwa BWANA, Mungu wenu, Na kumlilia BWANA,
4) Kuhiji
Kumbukumbu la Torati 12:5
Lakini mahali atakapochagua BWANA, Mungu wenu, katika kabila zenu zote, apaweke jina lake, maana, ni makao yake, elekezeni nyuso zenu hapo, nawe wende huko;
Kumbukumbu la Torati 12:6
pelekeni huko sadaka zenu za kuteketezwa, na dhabihu zenu, na zaka zenu, na sadaka ya kuinuliwa ya mikono yenu, na nadhiri zenu, na sadaka zenu za hiari, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ng’ombe na ya kondoo;