Hivi mwanamuziki Senzo yu hai au alishafariki?

Hivi mwanamuziki Senzo yu hai au alishafariki?

Ni kweli Ila inasemekana kifo chake gari ilimgonga Ila inasemekana ilikuwa gari ya lucky dube. Jamaa senzo alivyojitenga na kuanza kuimba raggae mwaka ule kazi zake ziliongoza Kwa mauxo ya mziki wa raggae. Bifu ikawepo Kati yake na lucky dube.

Yawezekana kabisa Mkuu
 
Senzo amefariki muda mrefu na aliuwawa kwa kupigwa risasi na rafiki yake kipenzi aliyekuwa anampa drugs anaitwa LONGWE drugs zilikuwa zinamsaidia kupafomu muda mrefu.

Ugomvi ulianzia kwa mmoja wa rafiki yao anaitwa kelly dhidi ya Longwe kisa tu mwanamke sasa ikabidi aingilie Senzo na wakati huo alikuwepo mwanamke ambaye ni mama yake na kelly khumalo.

Longwe alimpiga risasi Senzo na baada ya kumpiga aliwatishia kelly na mama yake kuwa wakisema atawauwa nao.
Maneno ya mwisho aliyoyatamka senzo ulimwenguni ni "yini le oyenzayo mfethu" (What are you doing my brother)
Huyu Senzo wako alikuwa maarufu SA tu wengine tulimfahamu baada ya kuuwawa,anayeuliziwa ni yule mwanamziki wa Reggae ambaye yu ngali hai.
 
Ni kweli Ila inasemekana kifo chake gari ilimgonga Ila inasemekana ilikuwa gari ya lucky dube. Jamaa senzo alivyojitenga na kuanza kuimba raggae mwaka ule kazi zake ziliongoza Kwa mauxo ya mziki wa raggae. Bifu ikawepo Kati yake na lucky dube.
Wewe Mwongo. Unaleta story za vijiweni
 
Senzo mwanamuziki wa raggae yupo hai ila Senzo aliyefariki ni golikipa.
 
Senzo inasemekana alikuwa kwenye bendi ya lucky dube but. Aliachana na lucky dube na kuanza kuimba raggae ktk mwaka ule alimzidi lucky dube Kwa mauxo ya album zake katika raggae. Watu wanadai aligongwa na gari ya luck dube. Kwahiyo inasemekana aliuawa na lucky dube
Hii ilitamba sana kipindi cha katikati ya miaka ya 90. Ikatajwa amekufa kwa figisu zinazomhusisha rafiki yake yaani Luck Dube, na ni kitambo sana. Hata kifo cha Dube,ni nadharia ya kisasi cha wadau wa Senzo(ni nadharia ambazo ni ngumu kuthibitisha,ila zipo na hazina tofauti na zile za kifo cha Tupac na Notorious B.I.G)
 
Senzo Robert Meyiwa (1984 - 2014) huyu alikuwa mchezaji wa mpira wa miguu, katika nafasi ya ugolikipa wa timu ya Orlando Pirates na pia alikuwa akichezea timu ya taifa, ambaye alipigwa risasi na kufa katika tukio la unyang'anyi. Sasa kuna huyu Senzo Mhthethwa (??1983 -!!!) ambaye na mzidi kwa umri. Baada ya kifo cha Lucky Philip Dube (18 oktoba, 2007) kufariki kwa kushambuliwa na risasi alipokuwa akipeleka wanae shule, ndipo mashabiki wa Senzo nchini Malawi na kwingineko, walipo ibuka na hekaya za Senzo: ('the best selling reggae artist in South Africa; is still alive!') kwa mantiki hiyo wakati wa uhai wa Lucky Dube waliamini Senzo ni hayati (alisha kufa kitambo), na baada ya Kifo cha Lucky Dube, mashabiki wa Senzo wa kamfufua mpendwa wao, Senzo - Rasta wake up! Na katika fikira zao mpaka sasa yupo 'hai'. Yote kwa yote awe hai au alishakufa! Baki na imani hii moyoni mwako kwamba, RASTA HAFI, AKIFA HAOZI,AKIOZA HANUKI, AKINUKA UNUKIA MARASHI DAIMA NA MILELE! PEACE AND LOVE. Keep up, Rasta. GWAN!
 
Namzungumzia senzo reggae artist
Hapana bro,aliyekuwa na mahusiano na Kelly Kumalo ni Senzo Meyiwa ambaye alikuwa goalkeeper wa Orlando Pirates.

Kisa ulichokiongelea ni cha Senzo huyo na si Senzo reggae artist.
 
Hii ilitamba sana kipindi cha katikati ya miaka ya 90. Ikatajwa amekufa kwa figisu zinazomhusisha rafiki yake yaani Luck Dube, na ni kitambo sana. Hata kifo cha Dube,ni nadharia ya kisasi cha wadau wa Senzo(ni nadharia ambazo ni ngumu kuthibitisha,ila zipo na hazina tofauti na zile za kifo cha Tupac na Notorious B.I.G)
Je ni kweli senzo yu hai au marehemu?
 
Habari wadau, mie ni mshabiki muziki wa reggae,huyu mwanamuziki sifahamu taarifa zake mwenye uelewa nazo anijuze tafadhari.
Mnhhhh...!!

Haiwezekaniii...

Au ulikuwa jela!?
 
Back
Top Bottom