Mgogoro kuhusu haki ya kuchinja kwenye mabucha limeshindikana kwa sababu kuna baadhi ya watu wameona hawatendewi haki. Watu hawa walikuwa wamewapa wenzao haki ya kuchinja kwa ajili tu ya ustaarabu; lakini baada ya kuona 'ustaarabu' wao unageuzwa na kufanywa ni sheria ndipo walipoamua kuidai haki yao.
Nashauri yafuatayo: kwa kuwa nchi yetu siyo ya kidini bali watu wake wana dini zao;
na kwa kuwa watu hawabaguliwi kwa dini (imani) zao;
kwa hiyo basi, wote wapewe haki ya kuchinja kwenye hayo machinjio na wauze nyama kwenye mabucha yao.
Kwa wale wenye mashaka ya kula vilivyochinjwa na wenye imani tofauti na yao - nashauri mabucha yao yaandikwe 'HALAL' ili kiwe ni kitambulisho cha wapi wanunue na wapi wasinunue. Huko ughaibuni, wale wanaohofia kula visivyochinjwa kwa imani yao huenda kwenye mabucha yaliyoandikwa 'HALA' na hakuna ugomvi wowote. Pia wale ambao ni wa imani tofauti ambao hawaoni kikwazo kula kilichochinjwa na wa imani nyingine huamua kununua watakapo.
Kwa hiyo, serikali itoe haki kwa wananchi wote kuchinja kwenye machinjio nchini na kuuza nyama mabuchani. Wale wanaotaka kula vilivyochinjwa kwa imani yao, mabucha yao waandike 'HALAL'.