Hivi nani anayeweza kuamini kwamba katika kipindi cha 1998-2017 tulistahili bilioni 700 tu katika makinikia?

Hivi nani anayeweza kuamini kwamba katika kipindi cha 1998-2017 tulistahili bilioni 700 tu katika makinikia?

RNA

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2013
Posts
1,647
Reaction score
2,803
Habari wana JF, nimeipitia hii ripoti kwa umakini nlichogundua ni kweli kuna uwezekano mkubwa data zilikuwa zinaongezwa kidogo tukawa hatustahili 360 trilioni ,Lakino ukichukulia makinikia haiwi na thahabu tu bali kuna madini mengine pia bilioni 700 inafikirisha.

Lakini pia kwa watu ambao wamekaa sehemu zenye madini 1998-2017 ndiyo miaka ambayo madini yalikuwa yanapatikana kiurahisi na kwa wingi kiasi kwamba ni Ngumu kukubali kwa tulistahili hiyo 700bilioni tu.

Mwisho kabisa Siasa ni mchezo mchafu na kuna propaganda nyingi sana kuna uwezekano tunaaminishwa kitu ambacho sicho na watu washalamba asali.

Ukweli kamili inawezekana anao JPM mwenyewe ,nauliza tena hivi JF katika mazingira ya 1998-2017 na hii riport ni na anaweza kuamini tulistahili 700 bilioni tu?
 

Attachments

Inawezekana tulistahili nyingi zaidi ya hiyo lakini tulibanwa na masharti ya kwenye mikataba husika tuliyoingia na wazungu, ubinafsi wa viongozi wetu uliliumiza taifa.

Chanzo cha haya yote ni serikali zilizopita kusaini mikataba ya madini bila kuweka maslahi ya taifa mbele, zipo mpaka taarifa kuna mikataba ya madini ilisainiwa hotelini Ulaya.

Kama viongozi waliopita walikuwa na akili hizo za kwenda nje kusaini mikataba ya madini, kwangu yule aliyekuja na kuanza kuipitia upya hiyo mikataba alikuwa bora zaidi ya wote waliomtangulia, huu ndio ukweli, na haijalishi kama aliipata hiyo bil.700 kweli au hakuipata.
 
Back
Top Bottom