Hivi naweza kujenga nyumba kwa mshahara wa laki 5 kwa mwezi?

Ni hivi,jibane kwa miaka miwili au mitatu save ata laki 3 kwa mwezi,pia jifunze kutafuta kipato nje ya mshahara,ukiweza iyo assignment ndo unajenga,usikope ufanye biashara,au kulima,Anza biashara/kilimo kwanza kabla ili ujifunze vitu,wengi wanaokopa kujenga nyumba hua zinaishia kwa lenta
 
Unachopata ni mbegu.....
Watu wanapata elfu themanini kwa mwezi na wanajenga
 
Utajenga tu hata bila kukopa jitahidi uanze mapema kabla dogo hajaanza mambo ya shule
 
Unajenga kabisa na kuhamia. Laki moja ni Sawa na bati 4 za Simba dumu. Kwa mwaka una bati 48 ambazo zinatosha vyumba 3 na sebule.
Laki ni to tofali 100 za bloc kwa mwaka una tofali 1200 ambazo zinatosha nyumba hadi kwenye renta.
Hivyo jibane matumizi yasizidi laki 2 kwa mwezi. Alaf kila mwezi weka laki na nusu SACCOS au kikoba cha kazini kwenu.

Usioe mtumishi wa ofisini, oa binti mchakalikaji anayeweza kutumia mtaji mdogo kufanya biashara ya genge. Angalau kidato cha nne au VETA.
Kila la kheri
 
Walimu na kujenga ni kama mmelogelezewa vile.
Asilimia kubwa huwa mnawaza kujenga tu na sio kua huru kiuchumi, ni kujenga tu.

Unakopa 15M then unajenga huku ukipokea laki 3 sijui 2 ambayo wala haikutoshelezi kwa mahitaji ya familia.
Hii mentality ipo kwa watumishi wote mkuu. Siyo walimu pekee. Mtumishi anacho kiwaza ni kujenga na kununua usafiri pekee.
 
Mshahara laki tano alafu asave laki tatu, na anafamilia. Huwezi kuwa serious
 
Mafanikio siku zote huenda kwa wale wanaochunga wakati wao wotee piaa kuchukua hatua bila kujari mazingira yapojee, utaweza kujenga kama utaamua kuchukua hatua naa kujinyimaa pamoja na uvumilivu mkubwa mnoo katika wakati ambao upoo nao sasa,, jiwekeee kidgo hichohicho ulichonacho na upange mikakati ya kujenga,, na kuifatilia siku baada ya siku
 
Hapa mamlaka husika waangali jambo hili Kwa jicho la tatu, inasikitisha kukata tozo zote hizo, na unit wangeoneza sasa ili ziendane na kiasi Cha pesa chenye mteja anatoa.

Yaani nchi yetu kumekuwepo na tozo nyingi za ajabu ajabu lakini maendeleo duni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…