Hivi nchi hii inashindwa kuwakaribisha Spain/Brazil/ England/ France kujenga academy hapa nchini ili kuvumbua, kulea na kukuza vipaji vya football?

Hivi nchi hii inashindwa kuwakaribisha Spain/Brazil/ England/ France kujenga academy hapa nchini ili kuvumbua, kulea na kukuza vipaji vya football?

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Kwann kama taifa hatuna mikakati?? Nakasirika sana kuona serikali inadandia treni ya mafanikio ya mpira kwa mbele.

Nchi za Senegal, Mali, na Burkina Faso serikali za nchi hizi zimefanya uwekezaji mkubwa ktk soka. Na ndiyo tunayaona mafanikio yao.

Badala ya kuwategemea vijana waliokulia chai na maandazi, kisha wakaanza na kuvuta bangi kndipo wakajiingiza kwenye mpira, ni vema tuwaandaye tangu utotoni.

Hawa wa sasa hawanyumbuki, hawana nguvu na hata akili ya mpira hawana. Huyo tunayemuita star wetu wa taifa nje ya nchi ni kidampa tu.
 
Yani mkuu uwajengee academy hawa vijana na malnutrition zao, na natural lack of seriousness hamna mwekezaji wa kuchezea pesa zake hapo bongo!
Duuh! Basi tuachane mpira tu.

Tujenge vyuo vikuu vya umbea, uchawa na udangaji tu.
 
Daah! Kila kitu kinaharibiwa na siasa chafu nchi hii.
Amini kabisa. Unadhani hawajui tunakwamia wapi? Tutabaki tu tunasema wale tulikuwa level moja miaka 20 iliyopita sasa hivi wanasumbua huko duniani.
 
Kwann kama taifa hatuna mikakati?? Nakasirika sana kuona serikali inadandia treni ya mafanikio ya mpira kwa mbele...
Sijawahi kuona kazi ya wizara ya Michezo, utamaduni na sanaa zaidi ya kufungia nyimbo za wasanii kupitia basata.

Hao vijana unao waita wavuta bangi wamepambana kwa juhudi zao binafsi from scratch. Wamepitia changamoto lukuki wakifukuzia ndoto zao za soka. Leo ndio taifa linategemea kubebwa na wao. Wewe unawaita wavuta bangi. Viongozi wako waliwakumbuka jioni, wakawafanyia harambee haraka haraka. Shame.
 
CCM waoga sana wa changamoto. Kila kitu wanajihofia. Diaspora hawataki, uraia pacha hawataki, na kujenga academy hawataki. Daah!
Ni woga ukichanganya na ubinafsi na wamejiaminisha woga na ubinafsi wao ndiyo uzalendo kwa hiyo hauwezi kuwaambia kitu.
 
nikivoangia ile mechi kibanda umiza watu wote wakataka kunipiga maana nlikua nakia kwa uchungu wa taifa letu 😭😭 michezaji haijitumi kabsa
 
Nchi inaogozwa na watu wanao waza kuiba kodi tu na kubakia madarakani halafu ndio wafikirie kuendeleza vipaji? Utakuwa unaota wewe. Miaka 65 ya uhuru hata kuwa na sewage pipe kwenye mji hata mmoja wameshindwo. Wewe fikiria hayo sky scrap za majiji yote ni septic tank za Mavi. Yaani kuchimbia pipe ya kisafirisha Mavi na wange weza kupata hela za kutosha kuendesha kuondowa mafuliko
 
Duuh! Basi tuachane mpira tu.

Tujenge vyuo vikuu vya umbea, uchawa na udangaji tu.

Mwekezaji anategemea faida kaka/dada na kwa attitude ya wabongo una uhakika wa 100% loss. Watu ambao tangu uongozi wa juu kabisa hawaheshimu mikataba na makubaliano ndio kijana wa mbagala na matombo ataheshimu contract ya miaka 5-10 kumjenga hadi afikie kureturn investment? Tusidanganyane wakuu labda ccm ikiondoka na tuanze kujenga mtazamo mpya kabisa wa kuwa serious na vitu tunavyofanya!
 
Kwann kama taifa hatuna mikakati?? Nakasirika sana kuona serikali inadandia treni ya mafanikio ya mpira kwa mbele.

Nchi za Senegal, Mali, na Burkina Faso serikali za nchi hizi zimefanya uwekezaji mkubwa ktk soka. Na ndiyo tunayaona mafanikio yao.

Badala ya kuwategemea vijana waliokulia chai na maandazi, kisha wakaanza na kuvuta bangi kndipo wakajiingiza kwenye mpira, ni vema tuwaandaye tangu utotoni.

Hawa wa sasa hawanyumbuki, hawana nguvu na hata akili ya mpira hawana. Huyo tunayemuita star wetu wa taifa nje ya nchi ni kidampa tu.
lazima kwanza wajue nani kawaleta hao spain/england/brazil naanatoka chama gani? naanataka kuwa rais baadae ? huyu atatusumbua, wanazuia.wanaangalia maslahi yao kwanza ndio ya wananchi yaje.
 
Nakubaliana na mtoa mada kuwa kadri muda unavyokwenda ndio akili ya mpira na kasi kwa wachezaji ndio hupungua. Miaka ya 80 na 90 tulipata kushuhudia vipaji halisi vya mpira. Wachezaji walikuwa na vipaji halisi na walikuwa wanakasi sana uwanjani tofauti na leo. Zamani ilikuwa rahisi kuona mchezaji akipiga shuti mita 35-40 na kujaa wavuni ila leo hii ni jambo nadra sana. Wachezaji hawana akili kabisa ya mpira.

Jana nilikuwa naangalia mechi ya stars ila japo ya kuongoza bado aibu nilikuwa naipata mimi maana wachezaji wanachojua ni kurudisha mpira nyuma aka back pass na kukaa nyuma kuwaruhusu wapinzani wajenge mashambulizi.

Na makocha waliopewa timu ni vilaza tu...hivi unamtoaje kibu denis dk ya 68 ilihali yeye ndiye alikuwa hatari golini mwa zambia?
 
Kwann kama taifa hatuna mikakati?? Nakasirika sana kuona serikali inadandia treni ya mafanikio ya mpira kwa mbele.

Nchi za Senegal, Mali, na Burkina Faso serikali za nchi hizi zimefanya uwekezaji mkubwa ktk soka. Na ndiyo tunayaona mafanikio yao.

Badala ya kuwategemea vijana waliokulia chai na maandazi, kisha wakaanza na kuvuta bangi kndipo wakajiingiza kwenye mpira, ni vema tuwaandaye tangu utotoni.

Hawa wa sasa hawanyumbuki, hawana nguvu na hata akili ya mpira hawana. Huyo tunayemuita star wetu wa taifa nje ya nchi ni kidampa tu.
Wewe si mwananchi? Anzisha kiytuo kiwe mfano wa kuigwa. Unangoja nini?
 
Tusitegemee mabadiliko chini ya CCM, Chadema , CUF na vyama vingine vya upinzani , hapa ni mwendo wa kujilimbikizia mali
 
Back
Top Bottom