Wakati wa utawala wa awamu ya tatu tulimsikia aliyekuwa waziri wa fedha kipindi hicho akituambia kwamba hata tukila nyasi lazima ndege ya rais itanunuliwa.Kweli ndege hiyo aina ya Gulfstream Aerospace(5H-ONE) ilinunuliwa kwa mabilioni ya shilingi.swali langu ni kwamba,kwanini ndege hiyo haitumiki badala yake naona rais Kikwete anaendelea kutumia ndege ya mwanzo aina ya FOKKER 28(5H-CCM) badala ya hii tuliyonunua mabilioni ya shilingi? Je ndege hiyo ni nzima au mbovu?