Panya road ni vijana wadogo sana, wengi wao ni watoto wa mtaani kwa maana wamekuja kusaka maisha wakitokea mikoani ama wameshindikana majumbani mwao hivyo wameamua kuingia kitaa.
Mchana wanaomba na kuosha vioo vya magari pale ubungo na mwenge, wengine wanazunguka kule feri na coco munawaita beach boy, sijui kama kuna mmoja wetu hapa keshabahatisha kuona wakipigana wenyewe kwa wenyewe baada ya kuzulumiana, hautatizama mara mbili, viwembe, visu na mawe ndio silaha.
Sasa jiulize wakikuvamia wewe kwako unadhani kukucharanga na mapanga kwao ni ishu?
Polisi wasituzuge, hawa watoto wapo na watajibu mapigo muda sio mrefu, ondoeni hawa vijana barabarani, ni bomu.