Hivi ndivyo Hayati Magufuli aliharibu Uchumi wa Tanzania. Takwimu huwa hazidanganyi

Hivi ndivyo Hayati Magufuli aliharibu Uchumi wa Tanzania. Takwimu huwa hazidanganyi

Habari zenu wanabodi..

Ushahidi wa Takwimu umebainisha jinsi Serikali ya Magufuli iliharibu Uchumi wa Tanzania Kwa kiwango Kikubwa.

Kwa mujibu wa jarida la Tanzania Business Insight likinukuu taarifa za Benki Kuu na Ofisi ya Taifa ya Takwimu limefanya ulinganisho wa ukuaji wa Uchumi Kwa awamu ya kwanza ya Rais Mkapa,Kikwete na Magufuli.

Takwimu zinabainisha kwamba licha ya GDP kuongezeka ila Kasi ya uchumi ilipungua kutoka wastani wa 74% awamu ya kwanza ya Kikwete Hadi Asilimia 32% awamu ya kwanza ya Magufuli..

Aidha Uchambuzi pia unaonesha awamu ya kwanza ya Marehemu Mkapa,Alikuza uchumi Kwa Asilimia 154% na ni katika awamu ya Mkapa ndipo Uchumi wa Tanzania ulikuwa Mkubwa kuliko wa Kenya.

My Take
Ukweli ni kwamba licha ya Majigambo,Magufuli alifeli sana kwenye uchumi na ndio chanzo Cha kuanzisha udikteta usio na msingi ikiwemo kutunga Sheria za kuzuia watu ku challenge takwimu za uongo na za kupika za Serikali yake. Na kawaida ya Uchumi,namba Huwa hazidanganyi.

Wafuasi wa Mwendazake njooni mtoe majibu Kwa nini mlihatibu Uchumi? Mlikuwa mnafanya kazi gani hasa?
Swali lililosalia ni Je awamu ya 6 itatuvusha? Ni suala la kusubiria.
👇



Inasikitisha sana kwa wafuasi wa Magufuri kupendelea ngojera badala ya takwimu halisi na hali ya maisha ya wananchi wote katila utawala huo.
 
Wewe ni Mtanzania, upo ndani ya nchi na hukuona alichofanya JPM, watu wa nje waliona alichofanya na kumsifia, hebu funguka, piga maombi ili uone kazi nzuri aliyofanya JPM. Hakika JPM alikuwa mkombozi wetu kiuchumi ila basi tu! Mpaka sasa siamini! Huenda umejificha mahali, utarudi lini baba?
Mharibifu wa uchumi wa Tanzania namba one alikuwa Magufuri.
 
Samia hana hata miaka miwili😆,vuta subra,
Jpm aliimarisha uchumi sana🤷🏾‍♂️
Magufuri alikuta kila kitu na nakwambia kama Magufuri angelikuwa rais wa awamu ya tatu basi Tanzania ingekuwa nchi ya mwisho Afrika kimaendeleo.
 
Juzi rais Samia akiongea kwa msisitizo alisema "nchi yetu uchumi wake haukuteteleka sana kama majirani zetu kutokana na sera na maamuzi mazuri ya hayati Magufuli kutokufungan nchi kipindi cha COVID 19 , uchumi wetu upo imara kuzidi majirani zetu na Afrika"

Hoja yako imekaa kizushi na kihiyo, kwa mujibu wa bank ya dunia uchumi wa dunia umeshuka kutokana na janga la COVID 19,vita vya Ukraine na mabadiliko ya tabia nchi.

Jana rais Biden akihutubia maelefu ya watu mjini Warsaw Poland amesema vita ya Ukraine imeleta tatizo kubwa la kiuchumi duniani hasa Afrika .

Mleta mada utakuwa na mimba kubwa ya Magufuli inakutesa tulia uzae tu

USSR
Mimba aliyokuachia Magu bado hujazaa tu? Naona bado unatema mate
 
Back
Top Bottom