Hivi ndivyo Hayati Magufuli aliharibu Uchumi wa Tanzania. Takwimu huwa hazidanganyi

Hivi ndivyo Hayati Magufuli aliharibu Uchumi wa Tanzania. Takwimu huwa hazidanganyi

Mkimaliza kupambana na Legacy mje mtuambie kwa Nini huduma za kijamii ziliimbalika sana kuliko wakati wowote.
 
ni kweli ni mkapa pekee ndiye aliyeweza kukuza uchumi wa nchi hii hata kama watu walimlaumu vipi kwangu mimi mkapa ndo aliyekuwa mchapa kazi.Magufuli aliletwa na Mungu kuwanyoosha mafisadi sababu aliyaona mambo yote ya kishenzi yaliyofanyika huko nyuma wakati akiwa waziri.nchi ilikuwa ya wenye pesa,sheria zilikuwa hazifanyi kazi,uonevu ulipitiliza,wenye pesa walikuwa na uweza wa kufanya lolote na watoto wao ndo hao walioko humu JF wanaotukana au wanaomtukana JPM baada ya wazazi wao kunyooshwa kisawasawa na upuuzi huu unataka kuendelea ktk awamu hii.
Mwinyi ndiye mastermind wa ukuuaji wa uchumi na hasa sector binafsi.Mkapa angelimuanzishia nani hiyo mifumo ya ukusanyaji kodi kama walipa kodi wanatembea matako wazi na kula mlo mmoja?.
 
Anasemwa na ataendelea kusemwa kwa maovu aliyofanya, anavuna alichopanda. Kama Hitler, Mussolini, John Vosta, Idd Amin and so many other dictators waliokufa miaka iliyopita bado wanasemwa na pia wametungiwa vitabu sasa kwa nini dictator Jiwe asisemwe eti kwa kuwa hayupo alishafariki. What's the difference kati yake na hao dictators wengine? Hili liwe fundisho kwa marais wengine wataokuja wawe wakijua ya kuwa matendo yao ndiyo yatawahukumu na ndiyo yatayo-determine jinsi watakavyokumbukwa.
Andika kitabu chako basi tuje tusome uongo huo. Nani asiyejua hao jamaa ndie walioweka nchi zao kwenye pedestal za juu ??? nani Alijenga Autoban? nani Alijenga Workers Wagon? VW Nani Aliinua Fiat? Nani ali revolutionise ujengaji wa viwanda vikubwa kama cha Fiat?

Nenda Uganda mpaka leo wanamkubali, bila sera zake Mabilionea wa Uganda wa Leo hii wasingekuwepo...vilevile hao matajiri wakubwa Italy, Ujerumani.... n.k Wacha hizo leo hii mnawakataa babu zenu!
 
Kuegemea kule Kwa hayati kwenye ishu gani?

Mengine uliyoandika ni hadithi,hoja ilikuwa ni Magufuli kufifisha Kasi ya ukuaji wa uchumi Kwa 32% tuu,hiyo effects ya Miradi ya awamu ya 5 itaonekana baada ya Kukamilika kwenye awamu ya Samia lakini inasakia kuwa ni juhudi za Rais maana amepokea miradi karibu yote Iko chini ya 30% na by 2025 yote itakuwa imekamilika labda itasalia Sgr tuu ..

Mwisho Kwa miaka 2 tuu ya Rais Samia kuifungua uchumi rekodi zifuatazo zimewekwa..

TPA imevunja rekodi ya kuhudia makasha na mapato Kwa 1Tilioni

Banks Kwa mara ya kwanza zimefikia faida ya 1T

Kampuni za Bima mara ya kwanza zimefikia faida ya 1T

Tanzania Kwa mara ya kwanza imeizidi Kenya na EAC yote kwenye mauzo ya Nje yaani tuna exports zaidi ya tunavyo import,

TRA Kwa mara ya kwanza inakusanya wastani wa til.2 Kwa mwezi kutoka 1.2 Til.

Kwa mara ya kwanza tumeanza kuzalisha mbolea yetu wenyewe,mwaka huu Tume import Kwa sababu kiwanda kimeanza mwezi wa 7 ila.mwakani hakuna mfuko hata mmja utatoka Nje na infact Kunyaland wameanza ku import kutoka Tanzania,Tunajenga kiwanda kingine Pwani na kampuni ya Morocco..

In facts tuna vingi vya kuonesha mambo ni mengi mda ni mchanche,

Facts speak louder, agreed
 
Vipi wale walioporwa mali/biashara zao, waliodhulumiwa,

Walidhulumiwa kivipi majambazi na yamekiri?
waliotekwa na kuteswa,
Walijiteka?

na hao walioteswa waliweka mazingira yao...wateseke

walioshambuliwa kwa risasi na kujeruhiwa, Wangapi hao? Au unadai yule aliepigwa na water pelets?

waliobomolewa nyumba zao bila ya compensations,
Ndio wajifunze sheria. Nchi inaongozwa na Sheria na sio Huruma huruma.

waliotukanwa na kukashifiwa
Fiisadi ni Fisadi, wazembe ni wazembe waliostahili hayo walistahili
baada ya kupata madhara na hasara kutokana na natural disasters

Ushasema natural disasters! Kumuweka Hayati ndiye aliyeyafanya hayo ili iweje?

na ndugu wa wale waliouawa au 'kupotezwa' hao hawapo humu janvini?
Huna hata uhakika na hayo.

Punguza hasira basi usomeke wewe Monster au ndio hivyo wewe ni Baradhuli hilo
 
Wewe ni Mtanzania, upo ndani ya nchi na hukuona alichofanya JPM, watu wa nje waliona alichofanya na kumsifia, hebu funguka, piga maombi ili uone kazi nzuri aliyofanya JPM. Hakika JPM alikuwa mkombozi wetu kiuchumi ila basi tu! Mpaka sasa siamini! Huenda umejificha mahali, utarudi lini baba?

Kazi nzuri aliifanya Jiwe na moja hii hapa kwenye elimu

 
Mkimaliza kupambana na Legacy mje mtuambie kwa Nini huduma za kijamii ziliimbalika sana kuliko wakati wowote.
Nitajie Huduma mojawapo iliyoimalika na mie nikutajie mamia ya failures za awamu ya 5
 
Umesema Huduma ziliimarika nilotegemea Madarasa yawepo ya kutosha Ili Watoto wasikae chini kama hivyo kumbe hakuna alichofanya ila mnategemea Samia ndio afanye,hovyo kabisa..

Sasa ni hivi baada ya Rais Samia kumaliza tatizo la madarasa sekondari,kuanzia mwaka huu anaanza Mpango wa kumaliza Hilo tatizo shule za msingi,stay tuned
 
Umesema Huduma ziliimarika nilotegemea Madarasa yawepo ya kutosha Ili Watoto wasikae chini kama hivyo kumbe hakuna alichofanya ila mnategemea Samia ndio afanye,hovyo kabisa..

Sasa ni hivi baada ya Rais Samia kumaliza tatizo la madarasa sekondari,kuanzia mwaka huu anaanza Mpango wa kumaliza Hilo tatizo shule za msingi,stay tuned
Kwa hiyo wewe unataka akae tu ikulu asifanye kazi?. Kichwa mfuniko wwa shingo hiki.
 
Kwa hiyo wewe unataka akae tu ikulu asifanye kazi?. Kichwa mfuniko wwa shingo hiki.
Mradi huu hapa unaenda kumaliza hizo shida za madarasa shule za msingi, Mwendazake alishindwa,Til.1.1 zitafanga kazi hiyo.

 
Mradi huu hapa unaenda kumaliza hizo shida za madarasa shule za msingi, Mwendazake alishindwa,Til.1.1 zitafanga kazi hiyo.


Madarasa yatatosha tu iwapo watu wataanza kuzaa kwa mpango.

Sasa hivi ajenge tu baada ya 2030 atakae ingia atajenga zaidi. Kichwa chako sijui kinawaza umbali gani, nahisi kinaishia hapo ulipo.

Population inaongezeka kila siku, huwezi viongozi walio pita kwa upungufu wa madarasa.

Tozo mtutoze, sifa ya ujenzi mpate nyie, ebo.
 
Madarasa yatatosha tu iwapo watu wataanza kuzaa kwa mpango.

Sasa hivi ajenge tu baada ya 2030 atakae ingia atajenga zaidi. Kichwa chako sijui kinawaza umbali gani, nahisi kinaishia hapo ulipo.

Population inaongezeka kila siku, huwezi viongozi walio pita kwa upungufu wa madarasa.

Tozo mtutoze, sifa ya ujenzi mpate nyie, ebo.
Miaka yote yalishindwa kutosha licha ya Majigambo Kwa sababu kuu Moja, upungufu ulikuwa zaidi ya 75% wakati uwezo wa Serikali kuyajenga kuendana na Kasi ya ongezeko la Watoto ni 50% .

So Rais Samia atafuta hiyo gap Ili budget za kawaida ziweze kuhimili,ndivyo amefanya huko Sekondari chini ya Mradi wa Sequip na madarasa ya tozo na ndivyo anataka kufanya chini ya mradi wa Boost .
Screenshot_20230224-090551.jpg
 
Miaka yote yalishindwa kutosha licha ya Majigambo Kwa sababu kuu Moja, upungufu ulikuwa zaidi ya 75% wakati uwezo wa Serikali kuyajenga kuendana na Kasi ya ongezeko la Watoto ni 50% .

So Rais Samia atafuta hiyo gap Ili budget za kawaida ziweze kuhimili,ndivyo amefanya huko Sekondari chini ya Mradi wa Sequip na madarasa ya tozo na ndivyo anataka kufanya chini ya mradi wa Boost .View attachment 2528172
Naelekeza CHAWA Pro. Halielewi hata chanzo cha upungufu wa madarasa.
 
Habari zenu wanabodi..

Ushahidi wa Takwimu umebainisha jinsi Serikali ya Magufuli iliharibu Uchumi wa Tanzania Kwa kiwango Kikubwa.

Kwa mujibu wa jarida la Tanzania Business Insight likinukuu taarifa za Benki Kuu na Ofisi ya Taifa ya Takwimu limefanya ulinganisho wa ukuaji wa Uchumi Kwa awamu ya kwanza ya Rais Mkapa,Kikwete na Magufuli.

Takwimu zinabainisha kwamba licha ya GDP kuongezeka ila Kasi ya uchumi ilipungua kutoka wastani wa 74% awamu ya kwanza ya Kikwete Hadi Asilimia 32% awamu ya kwanza ya Magufuli..

Aidha Uchambuzi pia unaonesha awamu ya kwanza ya Marehemu Mkapa,Alikuza uchumi Kwa Asilimia 154% na ni katika awamu ya Mkapa ndipo Uchumi wa Tanzania ulikuwa Mkubwa kuliko wa Kenya.

My Take
Ukweli ni kwamba licha ya Majigambo,Magufuli alifeli sana kwenye uchumi na ndio chanzo Cha kuanzisha udikteta usio na msingi ikiwemo kutunga Sheria za kuzuia watu ku challenge takwimu za uongo na za kupika za Serikali yake. Na kawaida ya Uchumi,namba Huwa hazidanganyi.

Wafuasi wa Mwendazake njooni mtoe majibu Kwa nini mlihatibu Uchumi? Mlikuwa mnafanya kazi gani hasa?
Swali lililosalia ni Je awamu ya 6 itatuvusha? Ni suala la kusubiria.
👇



Hivi mtu una akili unaandika kitu kama hiki kweli! Inasaikitisha
 
Back
Top Bottom