Hivi ndivyo Hayati Magufuli aliharibu Uchumi wa Tanzania. Takwimu huwa hazidanganyi

Hivi ndivyo Hayati Magufuli aliharibu Uchumi wa Tanzania. Takwimu huwa hazidanganyi

Habari zenu wanabodi..

Ushahidi wa Takwimu umebainisha jinsi Serikali ya Magufuli iliharibu Uchumi wa Tanzania Kwa kiwango Kikubwa.

Kwa mujibu wa jarida la Tanzania Business Insight likinukuu taarifa za Benki Kuu na Ofisi ya Taifa ya Takwimu limefanya ulinganisho wa ukuaji wa Uchumi Kwa awamu ya kwanza ya Rais Mkapa,Kikwete na Magufuli.

Takwimu zinabainisha kwamba licha ya GDP kuongezeka ila Kasi ya uchumi ilipungua kutoka wastani wa 74% awamu ya kwanza ya Kikwete Hadi Asilimia 32% awamu ya kwanza ya Magufuli..

Aidha Uchambuzi pia unaonesha awamu ya kwanza ya Marehemu Mkapa,Alikuza uchumi Kwa Asilimia 154% na ni katika awamu ya Mkapa ndipo Uchumi wa Tanzania ulikuwa Mkubwa kuliko wa Kenya.

My Take
Ukweli ni kwamba licha ya Majigambo,Magufuli alifeli sana kwenye uchumi na ndio chanzo Cha kuanzisha udikteta usio na msingi ikiwemo kutunga Sheria za kuzuia watu ku challenge takwimu za uongo na za kupika za Serikali yake. Na kawaida ya Uchumi,namba Huwa hazidanganyi.

Wafuasi wa Mwendazake njooni mtoe majibu Kwa nini mlihatibu Uchumi? Mlikuwa mnafanya kazi gani hasa?
Swali lililosalia ni Je awamu ya 6 itatuvusha? Ni suala la kusubiria.
👇

Mliotaka JPM awagonge washeli akawakataa mnazidi kumiminika kila kukicha.
 
Magufuli angekusanya hizo pesa angeshindwa kuajiri? Miradi aliyoiqnzisha ingekuwa inasuasua?

Ndio maana nakwambia wewe ni useless umebeba kichwa kama mzigo, Waziri wa Fedha ambae ni VP wa Sasa anasema kabisa mapato Kwa mwezi aliacha 1.2 Til na Sasa ndio Yako 2.0 Tilioni wewe unaleta hadithi za kutunga?

Tangu nchi hii tupate uhuru ngwigulu nchemba ni moja ya mawaziri wawili wa fedha bogus kabisa. Mwingine alikua yule mwana mama sikumbuki jina.
 
Hata Mimi ni Mkristu halafu Mkatoliki niliyesoma Seminari. Ila nakuambia usijifiche kwenye Biblia kutaka kumtetea Magufuli. Magufuli alikuwa hata kanisa analitumia vibaya kutengeneza UDIKTETA wake.

Hivi alipokuwa anaua akina Ben Saanane kuna kifungu cha Biblia kilimruhusu?

Hukumu yangu ipo Wala Sina wasiswasi
Mbona wewe hajakuua toa ushahidi
 
Tangu nchi hii tupate uhuru ngwigulu nchemba ni moja ya mawaziri wawili wa fedha bogus kabisa. Mwingine alikua yule mwana mama sikumbuki jina.
Ni kweli kabisa Waziri bogos ndio amekuza mapato kutoka 1.2T kuwa 2T 😜😜😜😜

Haya yote yamefanyika Katikati ya Changamoto za uviko na Vita ya Ukraine..

Kwenye management ya Uchumi Rais Mkapa,Kikwete na Samia ndio watakuwa kwenye historia na bila shaka Rais Samia kama atakuwa Rais awamu ya pili ndio atawafunika hao wote..

Miradi 2 tuu inatosh kuwafunika wote.

-Kwala Industrial complex Dola bil.6
-Lindi LPG dola bil.30.

Hapo sijazungumzia miradi aliyoacha Mwendazake na utitiri wa miradi mipya Kila sekta na Kila Kona ya Tanzania
 
Sasa huyo Magufuli Mingi ya miradi yake ni hasara ukiacha bwawa la umeme..mradi kama reli,mabandari ya Ziwa Tanganyika hayawezi kuleta Tija licha ya Kukamilika Kwa sababu hayana linkages..

Pilia miradi Mingi ya aliyoacha Magufuli ilikuwa chini ya 30% lakini Mwenzie Samia mbona anaikimbiza Kwa speed sana? Ndio kusema by 2025 Rais Samia atakuwa amemaliza miradi Mingi sana na akiwa Rais awamu ya pili Na uhakika uchumi Wetu utakuwa mkubwa kuliko wa Kenya Kwa sababu Kuna LNG,kwala, Bagamoyo,Eacop,Mkonga sez nk

Pili Mwendazake yeye kazi yake ilikuwa ni kuanzisha miradi bila Kuimaliza au ndio ilikuwa mbinu ya kutaka kutawala milele Kwa visingizio vya kwamba hakuna Rais atakayemaliza miradi aliyoanzisha?

Pigia msumari,Rais Samia akiendelea kuwa Rais awamu ya pili Tanzania ndio itakuwa baba wa Uchumi EAC maana by that time tutakuwa tunajitosheleza Kwa Sukari,mbolea,mafuta ya kula,nafaka zote ikiwemo ngano na pia Nchinitakuwa imefunguka sana kimiundombinu hasa ya Barabara ,maji na umeme.
Miradi mingi ya sasa ni ya Upigaji. Ni kinuyume kabisa na unavyofikiria usidanganyike na PDF kabisa na takwimu za makaratasi.

Miradi mingi ya sasa itakayoanzishwa na Makamba na genge lake ni ya kujipigia 10%...Mtu anakula 7Trillion zake anasainisha mkataba wa 70 Trillion biashara inaishia hapo. Mjiandae kufukuZwa kupisha ujenzi bila kupewa hata fidia ya sh. 100.

Mikataba itakuwa ya Tz kupewa 3% huku mwekezaji anakula 97% kwa miaka 100.
 
Kama ipi hiyo ya kipagaji nitajie miradi 3 tuu
 
Hayo yakuwa looser ni chuki zako binafsi....hauwezi kupima hiyo "Looser" haina Takwimu yakhe
Mradi huu wa Eacop Mwendazake alikuwa anaenda kuzindua hewa mara 3 pale Tanga 😁😁😁😁

Ila nyie Mwendazake alikuwaga na fix sijawahi ona,sijui ule usanii alikuwa anafanya Ili kumfool nani..

Mradi mwingine ambao aliendaga kuzindua hewa ni uwanja wa ndege wa Msalato na Dom Ring Road hata mia haikuwepo na Wala Wakandarasi kuwa procured ila alienda kuweka Jiwe la Msingi 😜😜😜😜
 
Mimi nimejibu kisatarabu sana kulinda legacy

USSR
.
IMG_20230223_074654.jpg
 
Ni kweli kabisa Waziri bogos ndio amekuza mapato kutoka 1.2T kuwa 2T 😜😜😜😜

Haya yote yamefanyika Katikati ya Changamoto za uviko na Vita ya Ukraine..

Kwenye management ya Uchumi Rais Mkapa,Kikwete na Samia ndio watakuwa kwenye historia na bila shaka Rais Samia kama atakuwa Rais awamu ya pili ndio atawafunika hao wote..

Hapo alipo ni miendelezo wa Awamu ya tano. Subiri achagulike ndiyo uje umtetee

Miradi 2 tuu inatosh kuwafunika wote.

-Kwala Industrial complex Dola bil.6
-Lindi LPG dola bil.30.

Hapo sijazungumzia miradi aliyoacha Mwendazake na utitiri wa miradi mipya Kila sekta na Kila Kona ya Tanzania
Ni hivi, haiwezekani usizungumzie miradi ya Hayati katika hizo takwimu, wewe peke yako na chuki na propaganda has zako binafsi ndio umechagua iwe hivyo, tena kwa kujifanya Ati "sijazungumzia"
Shauri yako hiyo.

Watanzania tunajua, Ulimwengu unajua, na baadhi za Nchi duniani zimeenda kuegemea kule alipoegemea Hayati Raisi....sio lazima kuwa na maamuzi yanayopendwa na 'Watchdogs institution" yaani its not all laissez faire

Haujiulizi kwa nini Denmark nao waliondoa fedha kutoka katika mifuko ya 'Sherehe" na kuzipeleka katika mifuko ya maendeleo? Unafikiri, walifikiria tu? Hapo ndipo utajua ni Ushawishi gani aliokuwa nao hapa Ulimwenguni.
Nyie endeleeni na hayo machafuzi. Hayabadilishi mitazamo na uhalisia mitaani.
 
Back
Top Bottom