Hivi ndivyo Hayati Magufuli aliharibu Uchumi wa Tanzania. Takwimu huwa hazidanganyi

Hivi ndivyo Hayati Magufuli aliharibu Uchumi wa Tanzania. Takwimu huwa hazidanganyi

Magu alijenga uchumi wa machinga tu😅😅
Ujibiwe nini mjinga tu wala hujui mambo ya uchumi. Kwa kudhani unajua kuliko wataalam wa benki ya dunia waliyoitangaza tz kufikia gdp per capita usd 1086 na kua nchi ya uchumi wa kati unaonesha ujinga wako.
Eti growth rate 74%, 32% . Uliwaha kuona wapi annual growth rate za hivyo mjinga wewe.
Wakati wa jk tulikua na growth rate za 7.4% and then jpm akaanza ukuuaji mzuri kama huo kabla corona haijaingia na kuvuruga uchumi wa nchi nyingi. Nchi nyingi dunia zikawa na growth rate hazifiki hata 1% lakini tz kutokana na jpm alivyo handle corona uchumi wetu ukawa unakua kwa asilimia 3.2. jirani zetu kenya na uganga nadhani growth rate zilikua negative.
Mtahangaika kum demornise jpm hadi mnaonyesha ujinga wenu. Mtu uchumi hujui unajidai kuchambua kitu gani.
 
Habari zenu wanabodi..

Ushahidi wa Takwimu umebainisha jinsi Serikali ya Magufuli iliharibu Uchumi wa Tanzania Kwa kiwango Kikubwa.

Kwa mujibu wa jarida la Tanzania Business Insight likinukuu taarifa za Benki Kuu na Ofisi ya Taifa ya Takwimu limefanya ulinganisho wa ukuaji wa Uchumi Kwa awamu ya kwanza ya Rais Mkapa,Kikwete na Magufuli.

Takwimu zinabainisha kwamba licha ya GDP kuongezeka ila Kasi ya uchumi ilipungua kutoka wastani wa 74% awamu ya kwanza ya Kikwete Hadi Asilimia 32% awamu ya kwanza ya Magufuli..

Aidha Uchambuzi pia unaonesha awamu ya kwanza ya Marehemu Mkapa,Alikuza uchumi Kwa Asilimia 154% na ni katika awamu ya Mkapa ndipo Uchumi wa Tanzania ulikuwa Mkubwa kuliko wa Kenya.

My Take
Ukweli ni kwamba licha ya Majigambo,Magufuli alifeli sana kwenye uchumi na ndio chanzo Cha kuanzisha udikteta usio na msingi ikiwemo kutunga Sheria za kuzuia watu ku challenge takwimu za uongo na za kupika za Serikali yake. Na kawaida ya Uchumi,namba Huwa hazidanganyi.

Wafuasi wa Mwendazake njooni mtoe majibu Kwa nini mlihatibu Uchumi? Mlikuwa mnafanya kazi gani hasa?
Swali lililosalia ni Je awamu ya 6 itatuvusha? Ni suala la kusubiria.
[emoji116]

Ukweli ni kwamba, ukimwacha Mwalimu Nyerere, mpaka wakati huu, hakuna Rais aliyefanya mambo makubwa kwenye uchumi wa Tanzania kama Mkapa.

Ni kwa vile tu watanzania wengi wana vichwa vyepesi vinavyopenda kujadili na kusifia mambo mepesi, mambo mazito aliyoyafanya Mkapa, hawawezi kujua.

Record ya Mkapa, haijawahi kuvunjwa na utawala wowote Duniani. Record hiyo ni ya kushusha inflation toka 30% aliyoiacha Rais Mwinyi, mpaka 4%.

Mkapa ndiye aliyetengeneza mifumo ya uchumi, kodi na fedha.
 
Misukule ya Magufuli itasema kwa nini umamchafua mtu ambaye amelala hawezi kujitetea.

I assure you kama Mwenfazake angekuwa hai tungekuwa kama Zimbabwe au Yemen au Somalia. Tuendelee kumshukuru Mungu kwa kutuondolea yule Shetani
Kwa sisi Wakristo Biblia Takatifu inasema, "msihukumu ili msije mkahukumiwa, kwasababu kipimo kilekile mnachowapimia wengine ndiyo kipimo hichohicho mtakachopimiwa".
 
Wewe unataka kujua kuwa Magufuli alikusanya hadi Trilioni 2 kwa mwezi kutoka billion 800 za Kikwete

Unataka kujua alijenga SGR , kununua ndege 11,kujenga stand ya mbezi Louis,Dodoma , Chato, kupanua uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Nyerere , kujenga Chato airport,kupanua kwanza airport,njia nne kibaha hadi kimara,kuhamishai serkali Dodoma,kujenga meli ziwa Victoria na nyasa, kuhakikisha elimu Bure, kujenga barabara za lami dar hasa kinondoni, kupambana na rushwa ,madawa ya kulevya , uhujumu uchumi, wafanyakazi hewa na vyeti fake na kununua majengo ya kibalozi na kuanzisha balozi mpya au kubuni vitambulisho vya machinga

Mimi nitakufunza kilaza wewe usiyemjua kuchambua ilaza za vyama

Wewe unataka nini nije nikujibu

USSR
Kwa hiyo kupanua barabara ndio kukuza uchumi? Lakini mbona husemi kuwa alikuwa jizi la plea bargain?
 
Hizo takwimu ameziandika tu kutoka kwa kiazi mmoja kama yeye Sia za BODI YA TAKWIMU YA KITAIFA

huyu dada ni kiazi kama viazi mbatata vingine

USSR
Jibu hoja, ameshakupa takwimu. Matusi hayasaidii kitu
 
Watu wasio na ajira hawampendi kbsa magufuli as if tatizo la ajira n Tanzania s mngehama tu mkatafute kwenye fursa
 
Yaan mtu mwenye akili timamu kbsa huwez mchukia magu sisi tunaoagiza vitu nje tumepata afueni hasa kwenye suala la AirPort mizgo inawah sababu ya magufuli jamaa alikua very straight sema ndo huwez kumpenda huwezi ona mazur yake kwenye reli dar folen imeisha huduma za jamii zipo almost dar nzima inafika weeknd dar hakuna folen huyo n magu ukienda kila sehem dar panamasoko watu wameacha kwenda mbali kununua bidhaa daaaah afrika sjui tulirogwa wapi aisee ndo maana hatufanikiwa tunaleta lawama z wakoloni kumbe sisi kwa sisi ndo tunarudishana nyuma
 
Magu alijenga uchumi wa machinga tu😅😅
Hao ndio watanzania halisi wanaotakiwa kuwezeshwa ili kufikia levels za juu kabisa na kushika njia zote za uchumi wa nchi.

Sio hawa wahindi na waarabu wanaotuibia na kwenda kuficha fedha huko makwao.
 
Always Huwa una excuses kama zote kujaribu kutafuta justifications for your failures..

Covidi ilikuwepo kuanzia 2015 Hadi 2020? By the way athari za covid zimeanza kuanzia mwaka 2021 Hadi Sasa Mwendazake akiwa kaburini.
Hebu rudia tena, Mwendazake akiwa ....! Kamata hapohapo tutaendelea tukirudi.
 
Takwimu Uchwara.

Zimepikwa.
Na wala....
Hazibadilishi Mtazamo halisi.

Hao waliopungukiwa Kiuchumi walikuwa walozi, wevi,majambazi, mafisadi, wala rushwa watoa rushwa, watakashishaji fedha, mebeberu na vibaraka vyao, Tundu Lissu na wengine.....

Aisee kuna yale mleta mada aliyomezeshwa😂, sitarudia kuyaweka....nitachangia, siku zikiwadia, halafu niwekwe kwenye takwimu za 'baby shower'

😂😂😂
 
Ukweli ni kwamba, ukimwacha Mwalimu Nyerere, mpaka wakati huu, hakuna Rais aliyefanya mambo makubwa kwenye uchumi wa Tanzania kama Mkapa.

Ni kwa vile tu watanzania wengi wana vichwa vyepesi vinavyopenda kujadili na kusifia mambo mepesi, mambo mazito aliyoyafanya Mkapa, hawawezi kujua.

Record ya Mkapa, haijawahi kuvunjwa na utawala wowote Duniani. Record hiyo ni ya kushusha inflation toka 30% aliyoiacha Rais Mwinyi, mpaka 4%.

Mkapa ndiye aliyetengeneza mifumo ya uchumi, kodi na fedha.
Ulivyoandika "duniani" tu ukanivuruga, ingawa umeongea vizuri sana.
Kuongeza tu Mkapa aliamsha uchumi ndiyo maana unaona percent ilkuwa 154% kama msemaji wa kwanza alivyosema; alitengeneza macro economy na baadaye akaonyesha way to micro. TZ Vision 2025 ambayo ilifanya mwelekeo kuwa na direction baada ya Azimio la Arusha na Azimio la Zanzibar kefeli.

Issue ya kukua uchumi (acha siasa); ambayo ina-reflect kwenye GDP bado tunampa Mkapa; ingawa kwa Kikwete kuliongezeka billioni 14 almost zile zile alizoziacha Mkapa 13 billioni, na kwa Magufuli 15 billion; lakini reflection ya kazi za Mkapa zinaonekana Zaidi mwaka wa kwanza na wa pili wa Kikwete. Reflection ya Kikwete ilionekana kuanzia mwaka wake wa tatu na kuendelea hadi mwka wa pili wa Magu. Watu mna beza sana Magufuli, kwenye mwaka ujao mtashangaa sana GDP itakapo reflect kwa Samia, investment kama Bwawa la Nyerere, SGR, meli, Ndege, viwanja vya ndege, nk nk itampaisha Samia,

Kwa hiyo kusema kuwa Magufuli ndiyo aliharibu uchumi wa Nchi si ukweli
 
Mojawapo ya juhudi ni pamoja na kipunguza kuajiri na kuwapanga waliopo waweze kufanya kazi kwa bididoooo
Hii imekaaje kwa ustawi wa jamii? Ni jukumu la serikali kutengeneza fursa za ajira kwa kuajiri au kuwezesha mazingira ya watu kujiajiri.
 
Juzi rais Samia akiongea kwa msisitizo alisema "nchi yetu uchumi wake haukuteteleka sana kama majirani zetu kutokana na sera na maamuzi mazuri ya hayati Magufuli kutokufungan nchi kipindi cha COVID 19 , uchumi wetu upo imara kuzidi majirani zetu na Afrika"
mimi nawaamini zaidi wataalam kuliko wanasiasa.
 
Ninapokaaa maji yalikuwa ni mda wote na kipindi chote, kumbe kukua kwa uchumi ni kama ivi sasa Maji hamna kabisa mtaani na ndoo au dumu linauzwa 500. Nakuombea kwa mwenyezi Mungu uwe maskini wa kutupwa duniani na kesho mbinguni ili uonje shubiri ya Ugumu na changamoto za maisha.

siku zote furaha ipo nami.
 
Takwimu Uchwara.

Zimepikwa.
Na wala....
Hazibadilishi Mtazamo halisi.

Hao waliopungukiwa Kiuchumi walikuwa walozi, wevi,majambazi, mafisadi, wala rushwa watoa rushwa, watakashishaji fedha, mebeberu na vibaraka vyao, Tundu Lissu na wengine.....

Aisee kuna yale mleta mada aliyomezeshwa😂, sitarudia kuyaweka....nitachangia, siku zikiwadia, halafu niwekwe kwenye takwimu za 'baby shower'

😂😂😂
Na nyie pikeni za kwenu Mzee mtuletee 😁😁😁

Kila siku nawaambia Mwendazake alikuwa looser huelewi.Kwamba NBS na BoT na WB wamepika takwimu kama zama zenu au? 😜😜
 
Ninapokaaa maji yalikuwa ni mda wote na kipindi chote, kumbe kukua kwa uchumi ni kama ivi sasa Maji hamna kabisa mtaani na ndoo au dumu linauzwa 500. Nakuombea kwa mwenyezi Mungu uwe maskini wa kutupwa duniani na kesho mbinguni ili uonje shubiri ya Ugumu na changamoto za maisha.

siku zote furaha ipo nami.
Huo ni uongo wa mchana kweupe? Kwa hiyo kama yalikuwa mda wote yamekauka ghafla au? 😁😁😁😁

Ukitaka kudanganya uwe na logic
 
Kwa sisi Wakristo Biblia Takatifu inasema, "msihukumu ili msije mkahukumiwa, kwasababu kipimo kilekile mnachowapimia wengine ndiyo kipimo hichohicho mtakachopimiwa".
Hata Mimi ni Mkristu halafu Mkatoliki niliyesoma Seminari. Ila nakuambia usijifiche kwenye Biblia kutaka kumtetea Magufuli. Magufuli alikuwa hata kanisa analitumia vibaya kutengeneza UDIKTETA wake.

Hivi alipokuwa anaua akina Ben Saanane kuna kifungu cha Biblia kilimruhusu?

Hukumu yangu ipo Wala Sina wasiswasi
 
Ulivyoandika "duniani" tu ukanivuruga, ingawa umeongea vizuri sana.
Kuongeza tu Mkapa aliamsha uchumi ndiyo maana unaona percent ilkuwa 154% kama msemaji wa kwanza alivyosema; alitengeneza macro economy na baadaye akaonyesha way to micro. TZ Vision 2025 ambayo ilifanya mwelekeo kuwa na direction baada ya Azimio la Arusha na Azimio la Zanzibar kefeli.

Issue ya kukua uchumi (acha siasa); ambayo ina-reflect kwenye GDP bado tunampa Mkapa; ingawa kwa Kikwete kuliongezeka billioni 14 almost zile zile alizoziacha Mkapa 13 billioni, na kwa Magufuli 15 billion; lakini reflection ya kazi za Mkapa zinaonekana Zaidi mwaka wa kwanza na wa pili wa Kikwete. Reflection ya Kikwete ilionekana kuanzia mwaka wake wa tatu na kuendelea hadi mwka wa pili wa Magu. Watu mna beza sana Magufuli, kwenye mwaka ujao mtashangaa sana GDP itakapo reflect kwa Samia, investment kama Bwawa la Nyerere, SGR, meli, Ndege, viwanja vya ndege, nk nk itampaisha Samia,

Kwa hiyo kusema kuwa Magufuli ndiyo aliharibu uchumi wa Nchi si ukweli
Sasa huyo Magufuli Mingi ya miradi yake ni hasara ukiacha bwawa la umeme..mradi kama reli,mabandari ya Ziwa Tanganyika hayawezi kuleta Tija licha ya Kukamilika Kwa sababu hayana linkages..

Pilia miradi Mingi ya aliyoacha Magufuli ilikuwa chini ya 30% lakini Mwenzie Samia mbona anaikimbiza Kwa speed sana? Ndio kusema by 2025 Rais Samia atakuwa amemaliza miradi Mingi sana na akiwa Rais awamu ya pili Na uhakika uchumi Wetu utakuwa mkubwa kuliko wa Kenya Kwa sababu Kuna LNG,kwala, Bagamoyo,Eacop,Mkonga sez nk

Pili Mwendazake yeye kazi yake ilikuwa ni kuanzisha miradi bila Kuimaliza au ndio ilikuwa mbinu ya kutaka kutawala milele Kwa visingizio vya kwamba hakuna Rais atakayemaliza miradi aliyoanzisha?

Pigia msumari,Rais Samia akiendelea kuwa Rais awamu ya pili Tanzania ndio itakuwa baba wa Uchumi EAC maana by that time tutakuwa tunajitosheleza Kwa Sukari,mbolea,mafuta ya kula,nafaka zote ikiwemo ngano na pia Nchinitakuwa imefunguka sana kimiundombinu hasa ya Barabara ,maji na umeme.
 
Back
Top Bottom