Raphael Mtui
Member
- Nov 26, 2024
- 78
- 204
Ijumaa ya tarehe 27 September 2024, katikati ya makao makuu ya Hezbollah yaliyopo kwenye mtaa uitwao Danieh kwenye viunga vya jiji la Beirut nchini Lebanon:
Kikao cha kimkakati kilikuwa kikiendelea katika chumba kilicho ardhini kwenye handaki mahali hapo.
Chumba hiki kilikuwa chini umbali wa mita kumi na nane kutokea juu ya uso wa dunia.
Vyumba vya namna hii huwa vya kipekee kidogo: kwanza jina la vyumba hivi huitwa banker. Ni chumba ambacho kinakuwa kimejengwa kwa kutumia chumba kizito. Chuma hiki huwa kinene, lengo lake hasa likiwa ni kuwekewa uwezo wa kuhimili mashambulizi ya mabomu.
Zingatia, banker hili lilikuwa chini ardhini mita kumi na nane kutokea juu ya uso wa dunia uliojaa maghorofa yanayopamba jiji la Beirut.
Ni ndani ya chumba cha namna hii, kulikuwa na kikao cha kiongozi mkuu wa Hezbollah, ambaye hupewa cheo cha Katibu Mkuu (Secretary General), akiwa na maafisa wa ngazi za juu za kundi la Hezbollah.
Kiongozi huyu ni Hassan Nasrallah, mtu maarufu na mwenye ushawishi mkubwa sana kwenye ulimwengu wa Waarabu.
Jeshi la Israeli (IDF) lilikuwa limepata intelijensia muhimu sana. Mtu ambaye walikuwa wamemtafuta kwa muda mrefu, hatimaye wameambiwa kwa hakika alipo.
Mtu ambaye Israeli wamejaribu kumwua mara kadhaa lakini akawa akiponea chupuchupu!
Weledi ule ule uliotukuka wa shirika la Ujasusi la Israeli MOSSAD, ulikuwa umeweka mapandikizi (moles) ndani serikali ya Iran.
Mole ni 'pandikizi' ambao wapo kila mahali duniani.
Tukumbuke kwamba, rafiki mkuu wa Hezbollah ni Iran. Huyu Iran ndiye anayewatia nguvu Hezbollah tangu kuzaliwa kwake, na kulifanya kundi hili liwe ndio kundi namba moja la wanamgambo lenye utajiri wa silaha kuliko makundi yote ya namna hiyo duniani.
Huyu mole aliyepandikizwa na Israeli ndani ya Iran, anaonekana ni mtu wa ngazi za juu katika serikali ya Iran kiasi ambacho aliweza kupata taarifa za siri kubwa (classified information) kama hii ya kujua siku fulani, muda fulani na mahali fulani, kiongozi mkuu wa Hezbollah alikuwa anafanya kikao.
Kwa miaka isiyo michache, kiongozi mkuu wa Hezbollah, Hassan Nasrallah, hakuwa ameonekana hadharani. Hii ni kutokana na hofu ya kuuawa na Israeli.
Mara zote aliishi kwa uficho wa hali ya juu.
Hotuba yake ambayo aliongea hadharani mwaka huu ni ile aliyoitoa tarehe 13 February 2024 ambapo kupitia radio na television alionekana akihutubia. Ingine alitoa hapa mwezi wa tisa 2024, siku chache sana kabla hajauawa.
Hotuba za namna hii huwa ni kitu nadra sana sana kwa Hassan Nasrallah kufanya. Israel kupitia Mossad walikuwa wamemfuatilia na kumkosa-kosa kiasi ambacho isingewezekana tena kwake kuishi bila kuwa na hofu ya kuuawa. Alikuwa akiishi kwa usiri mkubwa sana.
Hata katika hotuba aliyoitoa siku hiyo ya 13 February, moja ya ajenda alizoongea kwa msisitizo ni kwamba 'simu za mkononi kwa wanachama wa Hezbollah ni hatari kuliko Mossad yenyewe!' Akawaagiza wanachama wote kabisa wa Hezbollah wasitumie tena simu za mkononi, kwani Israel wamezidukua na wanafuatilia kila hatua ya wanachama wa Hezbollah.
Hatimaye, ndipo ilionekana ni afadhali kutumia zile simu za zamani kama pagers, radio/walkie-talkies.
Hizi ni simu ambazo kwetu sisi hazikuwahi kutumika, maana tulihamia kwenye simu za mkononi moja kwa moja.
Katika hotuba hiyo, Hassan Nasrallah aliagiza kuwa wanachama wake watupe simu za mkononi, watumie hizi simu za kizamani, na wasiwe nazo mahali penye watu wengi kama kwenye vikao na mikusanyiko.
Pasipo kujua, kutupa kwao simu na kutumia hizi pagers ulikuwa mtego mahususi uliotengenezwa na Israeli.
Israeli walikuwa wamehakikisha wanazalisha hofu ya kutumia simu, ili wahamie kwenye hizo pagers, ambazo Israeli walikuwa wameshatengeneza mpango madhubuti na maridhawa mno!
Hii nayo ni stori ndefu ya kusisimua kweli-kweli, lakini acha tujikite kwenye hii mada husika. Fahamu tu kwa ufupi kwamba, Hezbollah walipoagiza maelfu ya pagers hawakujua wananunua 'mabomu' ya Israeli yanayokuja kuwalipukia wenyewe!
Ndio hapa tunaruka hadi ile Jumanne ya tarehe 17 Sept 2024. Siku hiyo, nchi nzima ya Lebanoni ilipigwa na mshangao wa kipekee, kwani maelfu ya simu za pagers zinazotumiwa na Hezbollah zililipuka kwa pamoja nchi nzima! Ingawa ni watu 12 pekee walikufa nchi nzima, lakini hospitali zilijaa watu waliojeruhiwa. Watu 2,800 walijeruhiwa.
Kesho yake, maelfu ya simu za walkie-talkies zililipuka nchi nzima, mitaani, misibani, masokoni, na kwenye supermarkets! Watu 25 walifariki, huku zaidi ya watu 450 wakijeruhiwa vibaya.
Tukio hili lilimfanya tena Hassan Nasrallah kuibuka na kuhutubia tena. Katika hotuba yake aliilaumu Israeli kwa uhusika wa tukio hilo, kwa kuweka vilipuzi kwenye maelfu ya pagers na radio handsets zinazotumiwa na wanachama wa Hezbollah. Akaongeza kwa kusema kwamba kitendo hicho kilimaanisha kwamba Israeli imevuka mistari yote myekundu!
Lakini tofauti na ilivyotegemewa, Israeli iliendelea 'kujikausha' kama vile hawajui kilichotokea.
Hebu turudi kwa mhusika wetu kwa makala haya, Hassan Nasrallah.
Hassan Nasrallah alizaliwa tarehe 31 Aug 1960 kwenye jimbo la kimaskini sana liitwalo Karantina lililopo upande wa Magharibi mwa jiji la Beirut nchini Lebanoni.
Yeye ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto tisa wa baba maskini aliyekuwa mmiliki wa 'grocery uchwara' hapo mtaani.
Tangu akiwa mtoto mdogo, Hassan alikuwa mwanafunzi mwenye bidii kubwa sana katika dini ya Uislamu.
Akiwa kijana mdogo tu wa miaka 15, alijiunga na kundi la wanamgambo la hapo Lebanoni lililoitwa Amal, ambalo lilikuwa na mafungamano na Iran.
Hakukaa muda, akaenda huko Iraq kujiunga na seminary ya dhehebu la Shia.
Mwaka 1978 wanafunzi wote wa Lebanoni walifukuzwa nchini Iraq, hivyo Hassan akarudi nyumbani Lebanoni kuendelea na kundi la Amal.
Aliungana na Hezbollah wakati ilipozaliwa mwaka 1982. Hii ina maana aliachana na Amal.
Nyota ya uongozi na kukubalika ilianza kuonekana mapema ndani ya Hezbollah. Mwaka 1992, akiwa mdogo tu wa miaka 32 Hassan alichaguliwa kuwa kiongozi mkuu wa Hezbollah.
Aliyekuwa kwenye cheo hicho, Abbas al-Musawi alikuwa ameuawa kwa kudunguliwa na majeshi ya Israeli.
Hassan alivyoingia tu madarakani, kazi yake ya kwanza alitafuta namna ya kuilipa Israeli kisasi kwa mauaji yale.
Akaamuru wanamgambo wake wavurumishe makombora kwenda Israeli, yakamwua msichana mmoja.
Pili, akamwua askari mmoja wa ubalozi wa Israeli nchini Uturuki kwa kumtegeshea bomu kwenye gari. Tatu, akamtuma mtu aliyejitoa mhanga, akavaa mabomu na kulipua ofisi za ubalozi wa Israeli nchini Argentina ambapo watu 29 waliuawa.
Katika uongozi wake, Hassan Nasrallah alipendwa na wanachama wake. Alikuja kuwa moja ya watu wanaojulikana zaidi na wenye ushawishi zaidi eneo lote la Mashariki ya Kati.
Aliimarisha sana mahusiano na Iran. Iran amekuwa mfadhili mkuu wa Hezbollah tangu kuundwa kwa kwake.
Wakati wa uongozi wake, Hezbollah imewasaidia sana kimafunzo wapiganaji wa ki-Palestina Hamas, lakini pia wamesaidia wanamgambo waliopo nchi za Iraq na Yemen.
Iran imekuwa ikiwapa Hezbollah silaha nyingi, mabomu na makombora ili wayatumie kuipiga Israeli.
Hassan ameifanya Hezbollah iwe jeshi kubwa kuliko jeshi rasmi lenyewe la nchi ya Lebanoni.
Sasa, turudi kwenye kile kikao kilichokuwa kinaendelea ardhini, kikiongozwa na Hassan Nasrallah.
Nilisema kwamba, Israeli ilikuwa imepata intelijensia muhimu kuhusu uwepo wa huyu 'most wanted' Hassan Nasrallah, mahali alipo na anachofanya.
Jeshi la Anga la Israeli likakaa 'mguu pande' tayari kwenda 'kuua mtu.' Linaitwa Israeli Air Force (IAF).
Jeshi la Israeli likakaa na kuchora mchoro, wakaipa 'operation' hii jina mficho la 'New Order'.
Kama kawaida, zikaandaliwa zile ndege zao za F-15I. Wakaweka 'kibindoni' mabomu 80, yote yanatakiwa yadondoshwe pale.
Lakini walijua kuwa Hassan na wenzake wako kwenye 'chuma cha banker' pale ardhini. Anaweza akapona wasipochukua hatua maalum kidogo. Wakaingia 'store' ya silaha za ki-Marekani, wakachukua mabomu maalumu yenye uwezo wa 'kupurungunyua' banker za ardhini. Mambomu yenyewe huitwa banker baster bombs.
Kipenga kikalia, ndege zikanyanyuka. Ule mtaa wa Danieh ukawekwa kati, ile sehemu husika (Haret Hreik) ikaanza kupokea 'mvua ya moto'. Ardhi ikakorogwa kweli-kweli, majengo yaliyokuwa jirani yakaporomoshwa!
Eneo lile likachakazwa, Israeli wakaamka Jumamosi wakiutangazia ulimwengu kuwa wamemwua Hassan Nasrallah, kiongozi mkuu wa Hezbollah.
Hezbollah wakaamka wakifukua vifusi, na hatimaye wakaupata mwili wa Hassan na wenzake, nao wakauambia ulimwengu kwamba 'Hassan Nasrallah amekwenda kuungana na mashahidi wenzake.'
Hassan aliuawa na wenzake, ingawa miili mingine haikupatikana.
Narudi punde kati uzi huu kuchambua kuhusu kundi hili la Hezbollah, tujue ilikuwaje likazaliwa, lilianzishwaje, na je, Lebanoni ina jeshi rasmi la nchi? Lina mahusiano gani na hili kundi la Hezbollah?
Raphael Mtui 0762731869