Hivi ndivyo Israel walivyomuua Hassan Nasrallah, simba aliyeisuka Hezbollah kwa miaka 30

Wewe kwa akili yako unadhani huyo jàmaa Nasrallah aliuawa peke yàke?
Yeye, màkamanda wake nà mipango yao mingi viliangamizwa.
Wewe unafikiri kwanini Hezbollah wanakubali kuingià mkataba wa kuachà mapigano wakati vita huko Gaza hàijasitishwa?
Kapigwa sana
 
Kilichowauma Iran sio Kifo cha NASRA ila Kifo cha kamanda wao mwandamizi nirifourshan aliechomwa kama mshikaki kule ardhini... Hedhibollah wamepiga hatua sita kurudia nyuma.......Watu WA Lebanon wenye akili hawatapenda kuuona uwepo wa Hao panzi tena maana akili Yao haina tofauti na akili ya panya...
Wakati watu wakirejea Lebanon,walebanon hata wa madhehebu ya sunni ambao ni wapinzani wa hizbullah walikua wakigawa peremende(sweets) kwa watu na kushangilia hizbullah kaizuia israel kuingia Lebanon, hizbullah ndiyo jeshi pekee linaloweza ilinda lebanon, walebanon hujivunia hizbullah
 
Wewe kwa akili yako unadhani huyo jàmaa Nasrallah aliuawa peke yàke?
Yeye, màkamanda wake nà mipango yao mingi viliangamizwa.
Wewe unafikiri kwanini Hezbollah wanakubali kuingià mkataba wa kuachà mapigano wakati vita huko Gaza hàijasitishwa?
Gaza mapigano soon yanasimama,kambi za israel mpakani zinechakaa, telaviv pemepigwa,raia kaskazini wamehama, silaha israel zimeisha, wakitaka kuendelea hizbullah wapo tayari,na aliyepropose cease fire siyo hizbullah bali israel na bwanaake
 
Kilichowauma Iran sio Kifo cha NASRA ila Kifo cha kamanda wao mwandamizi nirifourshan aliechomwa kama mshikaki kule ardhini... Hedhibollah wamepiga hatua sita kurudia nyuma.......Watu WA Lebanon wenye akili hawatapenda kuuona uwepo wa Hao panzi tena maana akili Yao haina tofauti na akili ya panya...
Hapa ndo wabongo mnajidanganya hata hujui chochote cha maana kuhusu Lebanon na influence ya Hezbollah kwa Lebanon
 
Kama Lebanon ni Tawi la Iran nadhani Iran angewekeza nguvu kubwa kuliimarisha jeshi la Lebanon na sio kuijenga hedhibollah Kwa gharama ya kumuua Rafik harir aliekuwa waziri mkuu WA Lebanon..... Kingine unajua Kwa nini Saudi Arabia kakaa pembeni haisaidii Lebanon??.....Ni Kwa Sababu yeye alikuwa na nia njema kuisaidia lebanon kiuchumi akashtuka kwamba serikali dhaifu ya lebanon imekuwa rubber stamp na hao virusi wa hedhibollah ndio wanashika hatamu kwa msaada wa iran........Aliekuwa na nia njema na lebanon ni saud arabia tu kwa sababu Saudi kashavuka stage ya uanaharakati na focus yao ni maendeleo tu...
Huyo Iran Kwa Sasa Yuko uchi na Endelea kumuangalia Kwa bidii...Anaendelea kuharibika kuanzia ndani...Ni Kama chuma kinacholiwa na kutu ambayo Kwa nje bado haijaonekana.
Hata usa na isreli wanatamani iwe hivyo lakini Iran pamoja na purukushani na fitnes na mapandikizi wametoka kapa
 
kwahiyo na akili zote israeli wanazosifiwa ndo walihangaika hivi kumuua jamaa na kwa gharama zote hizo
Kwao gharama sio ishu maana stock ya silaha ikikaa bure itaexpire
 
Nashangaa hivi kwanini nchi kubwa kama Lebanon haina ata Air Defense Systems!? Wao kila mtwango unaingia tu dah!
 
Ijumaa ya tarehe 27 September 2024, katikati ya makao makuu ya Hezbollah yaliyopo kwenye mtaa uitwao Danieh kwenye viunga vya jiji la Beirut nchini Lebanon:

Kikao cha kimkakati kilikuwa kikiendelea katika chumba kilicho ardhini kwenye handaki mahali hapo.

Chumba hiki kilikuwa chini umbali wa mita kumi na nane kutokea juu ya uso wa dunia.

Vyumba vya namna hii huwa vya kipekee kidogo: kwanza jina la vyumba hivi huitwa banker. Ni chumba ambacho kinakuwa kimejengwa kwa kutumia chumba kizito. Chuma hiki huwa kinene, lengo lake hasa likiwa ni kuwekewa uwezo wa kuhimili mashambulizi ya mabomu.

Zingatia, banker hili lilikuwa chini ardhini mita kumi na nane kutokea juu ya uso wa dunia uliojaa maghorofa yanayopamba jiji la Beirut.

Ni ndani ya chumba cha namna hii, kulikuwa na kikao cha kiongozi mkuu wa Hezbollah, ambaye hupewa cheo cha Katibu Mkuu (Secretary General), akiwa na maafisa wa ngazi za juu za kundi la Hezbollah.

Kiongozi huyu ni Hassan Nasrallah, mtu maarufu na mwenye ushawishi mkubwa sana kwenye ulimwengu wa Waarabu.

Jeshi la Israeli (IDF) lilikuwa limepata intelijensia muhimu sana. Mtu ambaye walikuwa wamemtafuta kwa muda mrefu, hatimaye wameambiwa kwa hakika alipo.

Mtu ambaye Israeli wamejaribu kumwua mara kadhaa lakini akawa akiponea chupuchupu!

Weledi ule ule uliotukuka wa shirika la Ujasusi la Israeli MOSSAD, ulikuwa umeweka mapandikizi (moles) ndani serikali ya Iran.

Mole ni 'pandikizi' ambao wapo kila mahali duniani.

Tukumbuke kwamba, rafiki mkuu wa Hezbollah ni Iran. Huyu Iran ndiye anayewatia nguvu Hezbollah tangu kuzaliwa kwake, na kulifanya kundi hili liwe ndio kundi namba moja la wanamgambo lenye utajiri wa silaha kuliko makundi yote ya namna hiyo duniani.

Huyu mole aliyepandikizwa na Israeli ndani ya Iran, anaonekana ni mtu wa ngazi za juu katika serikali ya Iran kiasi ambacho aliweza kupata taarifa za siri kubwa (classified information) kama hii ya kujua siku fulani, muda fulani na mahali fulani, kiongozi mkuu wa Hezbollah alikuwa anafanya kikao.

Kwa miaka isiyo michache, kiongozi mkuu wa Hezbollah, Hassan Nasrallah, hakuwa ameonekana hadharani. Hii ni kutokana na hofu ya kuuawa na Israeli.

Mara zote aliishi kwa uficho wa hali ya juu.

Hotuba yake ambayo aliongea hadharani mwaka huu ni ile aliyoitoa tarehe 13 February 2024 ambapo kupitia radio na television alionekana akihutubia. Ingine alitoa hapa mwezi wa tisa 2024, siku chache sana kabla hajauawa.

Hotuba za namna hii huwa ni kitu nadra sana sana kwa Hassan Nasrallah kufanya. Israel kupitia Mossad walikuwa wamemfuatilia na kumkosa-kosa kiasi ambacho isingewezekana tena kwake kuishi bila kuwa na hofu ya kuuawa. Alikuwa akiishi kwa usiri mkubwa sana.

Hata katika hotuba aliyoitoa siku hiyo ya 13 February, moja ya ajenda alizoongea kwa msisitizo ni kwamba 'simu za mkononi kwa wanachama wa Hezbollah ni hatari kuliko Mossad yenyewe!' Akawaagiza wanachama wote kabisa wa Hezbollah wasitumie tena simu za mkononi, kwani Israel wamezidukua na wanafuatilia kila hatua ya wanachama wa Hezbollah.

Hatimaye, ndipo ilionekana ni afadhali kutumia zile simu za zamani kama pagers, radio/walkie-talkies.

Hizi ni simu ambazo kwetu sisi hazikuwahi kutumika, maana tulihamia kwenye simu za mkononi moja kwa moja.

Katika hotuba hiyo, Hassan Nasrallah aliagiza kuwa wanachama wake watupe simu za mkononi, watumie hizi simu za kizamani, na wasiwe nazo mahali penye watu wengi kama kwenye vikao na mikusanyiko.

Pasipo kujua, kutupa kwao simu na kutumia hizi pagers ulikuwa mtego mahususi uliotengenezwa na Israeli.

Israeli walikuwa wamehakikisha wanazalisha hofu ya kutumia simu, ili wahamie kwenye hizo pagers, ambazo Israeli walikuwa wameshatengeneza mpango madhubuti na maridhawa mno!

Hii nayo ni stori ndefu ya kusisimua kweli-kweli, lakini acha tujikite kwenye hii mada husika. Fahamu tu kwa ufupi kwamba, Hezbollah walipoagiza maelfu ya pagers hawakujua wananunua 'mabomu' ya Israeli yanayokuja kuwalipukia wenyewe!

Ndio hapa tunaruka hadi ile Jumanne ya tarehe 17 Sept 2024. Siku hiyo, nchi nzima ya Lebanoni ilipigwa na mshangao wa kipekee, kwani maelfu ya simu za pagers zinazotumiwa na Hezbollah zililipuka kwa pamoja nchi nzima! Ingawa ni watu 12 pekee walikufa nchi nzima, lakini hospitali zilijaa watu waliojeruhiwa. Watu 2,800 walijeruhiwa.

Kesho yake, maelfu ya simu za walkie-talkies zililipuka nchi nzima, mitaani, misibani, masokoni, na kwenye supermarkets! Watu 25 walifariki, huku zaidi ya watu 450 wakijeruhiwa vibaya.

Tukio hili lilimfanya tena Hassan Nasrallah kuibuka na kuhutubia tena. Katika hotuba yake aliilaumu Israeli kwa uhusika wa tukio hilo, kwa kuweka vilipuzi kwenye maelfu ya pagers na radio handsets zinazotumiwa na wanachama wa Hezbollah. Akaongeza kwa kusema kwamba kitendo hicho kilimaanisha kwamba Israeli imevuka mistari yote myekundu!

Lakini tofauti na ilivyotegemewa, Israeli iliendelea 'kujikausha' kama vile hawajui kilichotokea.

Hebu turudi kwa mhusika wetu kwa makala haya, Hassan Nasrallah.

Hassan Nasrallah alizaliwa tarehe 31 Aug 1960 kwenye jimbo la kimaskini sana liitwalo Karantina lililopo upande wa Magharibi mwa jiji la Beirut nchini Lebanoni.

Yeye ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto tisa wa baba maskini aliyekuwa mmiliki wa 'grocery uchwara' hapo mtaani.

Tangu akiwa mtoto mdogo, Hassan alikuwa mwanafunzi mwenye bidii kubwa sana katika dini ya Uislamu.

Akiwa kijana mdogo tu wa miaka 15, alijiunga na kundi la wanamgambo la hapo Lebanoni lililoitwa Amal, ambalo lilikuwa na mafungamano na Iran.

Hakukaa muda, akaenda huko Iraq kujiunga na seminary ya dhehebu la Shia.

Mwaka 1978 wanafunzi wote wa Lebanoni walifukuzwa nchini Iraq, hivyo Hassan akarudi nyumbani Lebanoni kuendelea na kundi la Amal.

Aliungana na Hezbollah wakati ilipozaliwa mwaka 1982. Hii ina maana aliachana na Amal.

Nyota ya uongozi na kukubalika ilianza kuonekana mapema ndani ya Hezbollah. Mwaka 1992, akiwa mdogo tu wa miaka 32 Hassan alichaguliwa kuwa kiongozi mkuu wa Hezbollah.

Aliyekuwa kwenye cheo hicho, Abbas al-Musawi alikuwa ameuawa kwa kudunguliwa na majeshi ya Israeli.

Hassan alivyoingia tu madarakani, kazi yake ya kwanza alitafuta namna ya kuilipa Israeli kisasi kwa mauaji yale.

Akaamuru wanamgambo wake wavurumishe makombora kwenda Israeli, yakamwua msichana mmoja.

Pili, akamwua askari mmoja wa ubalozi wa Israeli nchini Uturuki kwa kumtegeshea bomu kwenye gari. Tatu, akamtuma mtu aliyejitoa mhanga, akavaa mabomu na kulipua ofisi za ubalozi wa Israeli nchini Argentina ambapo watu 29 waliuawa.

Katika uongozi wake, Hassan Nasrallah alipendwa na wanachama wake. Alikuja kuwa moja ya watu wanaojulikana zaidi na wenye ushawishi zaidi eneo lote la Mashariki ya Kati.

Aliimarisha sana mahusiano na Iran. Iran amekuwa mfadhili mkuu wa Hezbollah tangu kuundwa kwa kwake.

Wakati wa uongozi wake, Hezbollah imewasaidia sana kimafunzo wapiganaji wa ki-Palestina Hamas, lakini pia wamesaidia wanamgambo waliopo nchi za Iraq na Yemen.

Iran imekuwa ikiwapa Hezbollah silaha nyingi, mabomu na makombora ili wayatumie kuipiga Israeli.

Hassan ameifanya Hezbollah iwe jeshi kubwa kuliko jeshi rasmi lenyewe la nchi ya Lebanoni.

Sasa, turudi kwenye kile kikao kilichokuwa kinaendelea ardhini, kikiongozwa na Hassan Nasrallah.

Nilisema kwamba, Israeli ilikuwa imepata intelijensia muhimu kuhusu uwepo wa huyu 'most wanted' Hassan Nasrallah, mahali alipo na anachofanya.

Jeshi la Anga la Israeli likakaa 'mguu pande' tayari kwenda 'kuua mtu.' Linaitwa Israeli Air Force (IAF).

Jeshi la Israeli likakaa na kuchora mchoro, wakaipa 'operation' hii jina mficho la 'New Order'.

Kama kawaida, zikaandaliwa zile ndege zao za F-15I. Wakaweka 'kibindoni' mabomu 80, yote yanatakiwa yadondoshwe pale.

Lakini walijua kuwa Hassan na wenzake wako kwenye 'chuma cha banker' pale ardhini. Anaweza akapona wasipochukua hatua maalum kidogo. Wakaingia 'store' ya silaha za ki-Marekani, wakachukua mabomu maalumu yenye uwezo wa 'kupurungunyua' banker za ardhini. Mambomu yenyewe huitwa banker baster bombs.

Kipenga kikalia, ndege zikanyanyuka. Ule mtaa wa Danieh ukawekwa kati, ile sehemu husika (Haret Hreik) ikaanza kupokea 'mvua ya moto'. Ardhi ikakorogwa kweli-kweli, majengo yaliyokuwa jirani yakaporomoshwa!

Eneo lile likachakazwa, Israeli wakaamka Jumamosi wakiutangazia ulimwengu kuwa wamemwua Hassan Nasrallah, kiongozi mkuu wa Hezbollah.

Hezbollah wakaamka wakifukua vifusi, na hatimaye wakaupata mwili wa Hassan na wenzake, nao wakauambia ulimwengu kwamba 'Hassan Nasrallah amekwenda kuungana na mashahidi wenzake.'

Hassan aliuawa na wenzake, ingawa miili mingine haikupatikana.

Narudi punde kati uzi huu kuchambua kuhusu kundi hili la Hezbollah, tujue ilikuwaje likazaliwa, lilianzishwaje, na je, Lebanoni ina jeshi rasmi la nchi? Lina mahusiano gani na hili kundi la Hezbollah?

Raphael Mtui 0762731869
Sawa, ila ni "bunker" sio "banker" na "bunker buster" sio "banker baster"
 
Yule Mbwa wa Ayatolah alikufa kifo cha Kinyama sana.😁😆
 
kwa hiyo kule mashariki ya kati mtu kuvamia na kuua most wanted wao ni kawaida na hao Israel wanapewa hayo mamlaka nani???
 
Raphael Mtui 0762731869 au
Vyumba vya chini ya ardhi ili kuepuka maahambulizi ni bunker; siyo banker.
 
HEZBOLLAH NI NINI HASA?

Kwa wale wanajukwaa wenzetu ambao hawajui kabisa kuhusu Hezbollah, tuseme hivi: ni chama cha siasa nchini Lebanoni, LAKINI, NI CHAMA CHENYE JESHI LENYE SILAHA!

Yaani, jenga picha mfano wa vyama vyetu hapa nchini.

Sasa, moja ya vitu ambavyo ni vya kawaida sana pale Mashariki ya Kati, ni chama kuwa na jeshi kama jeshi kabisa, lenye silaha, ndege za kivita, mabomu, makombora nakadhalika.

Mpaka hapo umepata ile picha rahisi na ya haraka.

Tukisema Hezbollah maana yake kwa Kiswahili tumesema 'chama cha Mungu' ambacho kinaundwa na Waislamu wa dhehebu la Shia.

Sasa, kuna maswali mengi, mfano:

Kama ni chama tu cha siasa, kwa nini kiwe na mabavu kiasi cha kupigana vita na nchi nyingine?

Sijui kama umeelewa?

Yaani mfano, tuseme vyama vyetu vya siasa hapa Tanzania viwe vina majeshi: sasa, inawezekanaje Red Brigade ya Chadema kwa mfano, iwe na mabavu ya kuanzisha vita dhidi ya Kenya? JWTZ watakuwa wako wapi? Red Brigade watakuwa wanatolea wapi huo 'ubavu' wa kupigana na nchi nyingine kama Hezbollah inavyopigana na Israeli mara kwa mara?

Jeshi rasmi la nchi ya Lebanoni linasemaje na serikali kwa ujumla?

Lakini kuna swali la pili: Hezbollah anapata wapi nguvu za kuwa na jeshi kubwa na imara la namna hii?

Wanapataje pesa za kujiendesha kiwango cha kutumia matrilioni ya fedha kununua silaha, kugharamia jeshi, na kugharamia vita?

Hebu tujibu haya maswali kwa kueleza historia fupi kabisa ya Hezbollah.

Siku ya Alhamisi, tarehe 3 mwezi June mwaka 1982 katikati ya jiji la London Uingereza, kulitokea tukio lililokuja kuleta mlolongo wa matukio makubwa ulimwenguni ikiwemo kuundwa kwa chama hiki cha Hezbollah.

Vijana watatu, Hussein Ghassan Said, Marwan al-Banna, na Nawaf al-Rosan walimvamia aliyekuwa Balozi wa Israeli nchini Uingereza akiwa ametoka kwenye sherehe iliyofanyika kwenye hoteli iliyoitwa Dorchester iliyopo mtaa wa Park Lane hapo London.

Hussein Ghassan alimvizia na kumsogelea Mheshimiwa Balozi Shlomo, kisha akatumia pistol yake (PM-63 machine Pistol), akamtandika Shlomo risasi ya kichwa.

Bahati iliyoje, balozi Shlomo hakufariki, lakini alikuwa ameumia vibaya mno.

Alikimbizwa hospitali, akafanyiwa upasuaji wa ubongo na hakuzinduka hadi miezi mitatu baadaye.

Vijana wale wote walikamatwa pale London, na ndipo ilipogundulika kuwa ni wafuasi wa kikundi kiitwacho Abu Nidal Organization.

Haraka, Israeli ikatangaza kitendo walichofanya vijana wale ni 'casus belli' (yaani ni tangazo rasmi la vita!)

Israeli hakuwa inatania, kwani siku tatu baadaye Israeli ilivamia nchi ya Lebanoni kuwasaka maadui wa namna hiyo nchini humo.

Huo ukawa ni uvamizi wa pili Israeli kufanya nchini Lebanoni baada ya ule wa kwanza wa miaka michache iliyokuwa imepita, mwaka 1978.

Uvamizi uligharimu maisha ya maelfu ya watu Lebanoni, maana Israeli 'ilimwaga moto' kwa hasira kali.

Israeli walitandika Lebanoni kwa miezi mitatu, ambapo watu elfu kumi na tisa waliuawa.

Israeli wakaita vita vile 'Operation Peace for Galilee'.

Sasa basi, wakati vita vile vikiendelea, kuna kikundi cha viongozi wa dhehebu la Shia waliwaza jambo.

Walipanga kuanzisha chama ambacho malengo yake makuu yatakuwa kwanza ni KUANGAMIZA TAIFA LA ISRAELI.

Lengo la pili, KUONDOA USHAWISHI WA NCHI ZA MAGHARIBI HASA MAREKANI ENEO LA MASHARIKI YA KATI NA KUDHIBITI USHAWISHI WA SAUDI ARABIA PIA.

Tatu, KUANZISHA TAIFA LA KISHIA NDANI YA LEBANONI.

Kama utani, Hezbollah ikawa inazaliwa hivyo.

Chama hiki kilipoanzishwa kilifadhiliwa kwa kupewa msaada mkubwa na Iran.

Tangu kuanzishwa kwake hadi leo, chama hiki kikiwa kina umri wa miaka karibu arobaini, Iran imekuwa mshirika mkuu wa Hezbollah.

Kwa nini Iran?

Kwa sababu kwanza taifa la Iran ni taifa la Waislamu wa dhehebu la Shia. Lakini pia chama cha Hezbollah kilijitanabaisha kufuata siasa zile zile za Iran za Ayatola Khomeini.

Hakika Hezbollah na Iran wakashibana, wakajazwa misaada mingi sana kiasi ambacho Hezobollah imekuwa na nguvu kubwa pengine kuliko serikali ya nchi yenyewe ya Lebanon.

Fikiri kwa mfano Hezbollah ilivyoanzishwa, ilipata msaada wa wataalamu wa kijeshi wapatao 1,500 kutoka Islamic Revolutionary Guard Corps (IRGC)!

Kuna wakati Hezbollah huitwa ni 'nchi ndani ya nchi'.

Ukiangalia nembo ya Hebollah, moja ya alama zilizopo ni pamoja na mchoro wa bunduki, ambayo imeandikwa mstari uliotolewa kwenye Quran usemao 'Hakika chama cha Mungu kitadumu'

Tangu Hezbollah ianzishwe, imekuwa ikisuguaga na Israeli mara nyingi, kwa kuwa lengo kuu la Hezbollah limekuwa kuiangamiza Israeli: 'destruction of the State of Israel.'

Raphael Mtui 0762731869.
 
History haibadiliki tena ila Lebanon inaweza kuamua kujijenga kuanzia Sasa.Waivunje hedhibollah na wanachama wake wajione ni waislam Tu wa dhehebu la Shia la Lebanon.....waamue wawaheshimu wasunni,, wakristo na wapagani na waunganishe Nia kuijenga Lebanon kwenye mafanikio na waache kujiona migambo rahisi WA kutumiwa na Iran...yenye Nia binafsi ya kuwa mtawala wa middle east ambayo ni ndoto ya mchana.... Lakini pia waelewe Irani anawatumia kama ngazi kufikia malengo yake hata kama ni kwa gharama ya vifo vyao...Hata wafe laki Iran anaangalia hela alowapa wameitumia kupiga hatua gani na malengo yapi!!!
Nenda kasome historia ya Lebanon kuanzia 1970 kuja sasa .
Haikataliki kuwa Iran anaitumia Hizbollah Kwa maslahi yake.
Ila usisahau pasi na hiyo Hizbollah basi wakristo wenzako wangekua wameshamalizwa na sunni,Kuna vita ilizuka sunni hasa kutoka Syria waliwachinja sana wakristo wenzako hapo Lebanon.
Aliyewatetea ni Hizbollah huyo mshia unayemsea anatakiwa aondoke.
Lebanon iliingia katika political crisis zaidi ya mara mbili na kupelekea kumegwa Kwa ardhi,leo hii kama sio Hizbollah basi Lebanon ingeipoteza sehemu kubwa sana ya Kusini pamoja na nusu ya ukanda wa bahari wenye utajiri wa gesi asilia.
Hujui hao Hizbollah wameiokoa mara ngapi Lebanon na wakristo wenzako.
Vita ya 2006 wakristo wenzako hawakuwa wajinga kuwaunga mkono Hizbollah dhidi ya Israel Kusini mwa Lebanon/Bint Jubeir.

Sawa Iran anaitumia Hizbollah ila tambua Iran hiyo hiyo ndio ilisaidia kufanikisha yote hayo nilokutajia hapo juu,no free lunch in this world.
Ni sawa na wewe tu muAfrika unayeambiwa ili upewe msaada wa kimataifa kubali LGBTQ.
 
Ila Hizbollah kasambaratishwa. Sijui atainukia wapi Tena.
 
Waisraeli wameunda unit nyingine golan iliyokuwepo iliepelekwa kuzimu yote na hizbo. Sahau hzb kusambaa bila ground oparation ya maana kitu ambacho hamukiwezi, hapo mashariki ya kati hakuna nchi ina utalaam wa ground force Kama hzb ukitoa Iran ambayo ndio mwalimu wa hizb..............

The IOF decided to create a new special unit to operate in the Golan in order to "improve the operational response in the area, to "double the strength of the division and serve as an operational reserve," formed as a "lesson from October 7th."

This comes following numerous successful attacks by the Lebanese and Iraqi resistances on zionist military sites in the Golan over the last year.
 
Back
Top Bottom