Hivi ndivyo Israel walivyomuua Hassan Nasrallah, simba aliyeisuka Hezbollah kwa miaka 30

Kapigwa sana
 
Wakati watu wakirejea Lebanon,walebanon hata wa madhehebu ya sunni ambao ni wapinzani wa hizbullah walikua wakigawa peremende(sweets) kwa watu na kushangilia hizbullah kaizuia israel kuingia Lebanon, hizbullah ndiyo jeshi pekee linaloweza ilinda lebanon, walebanon hujivunia hizbullah
 
Gaza mapigano soon yanasimama,kambi za israel mpakani zinechakaa, telaviv pemepigwa,raia kaskazini wamehama, silaha israel zimeisha, wakitaka kuendelea hizbullah wapo tayari,na aliyepropose cease fire siyo hizbullah bali israel na bwanaake
 
Hapa ndo wabongo mnajidanganya hata hujui chochote cha maana kuhusu Lebanon na influence ya Hezbollah kwa Lebanon
 
Hata usa na isreli wanatamani iwe hivyo lakini Iran pamoja na purukushani na fitnes na mapandikizi wametoka kapa
 
kwahiyo na akili zote israeli wanazosifiwa ndo walihangaika hivi kumuua jamaa na kwa gharama zote hizo
Kwao gharama sio ishu maana stock ya silaha ikikaa bure itaexpire
 
Nashangaa hivi kwanini nchi kubwa kama Lebanon haina ata Air Defense Systems!? Wao kila mtwango unaingia tu dah!
 
Sawa, ila ni "bunker" sio "banker" na "bunker buster" sio "banker baster"
 
Yule Mbwa wa Ayatolah alikufa kifo cha Kinyama sana.😁😆
 
kwa hiyo kule mashariki ya kati mtu kuvamia na kuua most wanted wao ni kawaida na hao Israel wanapewa hayo mamlaka nani???
 
Vyumba vya chini ya ardhi ili kuepuka maahambulizi ni bunker; siyo banker.
 
HEZBOLLAH NI NINI HASA?


Kwa wale wanajukwaa wenzetu ambao hawajui kabisa kuhusu Hezbollah, tuseme hivi: ni chama cha siasa nchini Lebanoni, LAKINI, NI CHAMA CHENYE JESHI LENYE SILAHA!

Yaani, jenga picha mfano wa vyama vyetu hapa nchini.

Sasa, moja ya vitu ambavyo ni vya kawaida sana pale Mashariki ya Kati, ni chama kuwa na jeshi kama jeshi kabisa, lenye silaha, ndege za kivita, mabomu, makombora nakadhalika.

Mpaka hapo umepata ile picha rahisi na ya haraka.

Tukisema Hezbollah maana yake kwa Kiswahili tumesema 'chama cha Mungu' ambacho kinaundwa na Waislamu wa dhehebu la Shia.

Sasa, kuna maswali mengi, mfano:

Kama ni chama tu cha siasa, kwa nini kiwe na mabavu kiasi cha kupigana vita na nchi nyingine?

Sijui kama umeelewa?

Yaani mfano, tuseme vyama vyetu vya siasa hapa Tanzania viwe vina majeshi: sasa, inawezekanaje Red Brigade ya Chadema kwa mfano, iwe na mabavu ya kuanzisha vita dhidi ya Kenya? JWTZ watakuwa wako wapi? Red Brigade watakuwa wanatolea wapi huo 'ubavu' wa kupigana na nchi nyingine kama Hezbollah inavyopigana na Israeli mara kwa mara?

Jeshi rasmi la nchi ya Lebanoni linasemaje na serikali kwa ujumla?

Lakini kuna swali la pili: Hezbollah anapata wapi nguvu za kuwa na jeshi kubwa na imara la namna hii?

Wanapataje pesa za kujiendesha kiwango cha kutumia matrilioni ya fedha kununua silaha, kugharamia jeshi, na kugharamia vita?

Hebu tujibu haya maswali kwa kueleza historia fupi kabisa ya Hezbollah.

Siku ya Alhamisi, tarehe 3 mwezi June mwaka 1982 katikati ya jiji la London Uingereza, kulitokea tukio lililokuja kuleta mlolongo wa matukio makubwa ulimwenguni ikiwemo kuundwa kwa chama hiki cha Hezbollah.

Vijana watatu, Hussein Ghassan Said, Marwan al-Banna, na Nawaf al-Rosan walimvamia aliyekuwa Balozi wa Israeli nchini Uingereza akiwa ametoka kwenye sherehe iliyofanyika kwenye hoteli iliyoitwa Dorchester iliyopo mtaa wa Park Lane hapo London.

Hussein Ghassan alimvizia na kumsogelea Mheshimiwa Balozi Shlomo, kisha akatumia pistol yake (PM-63 machine Pistol), akamtandika Shlomo risasi ya kichwa.

Bahati iliyoje, balozi Shlomo hakufariki, lakini alikuwa ameumia vibaya mno.

Alikimbizwa hospitali, akafanyiwa upasuaji wa ubongo na hakuzinduka hadi miezi mitatu baadaye.

Vijana wale wote walikamatwa pale London, na ndipo ilipogundulika kuwa ni wafuasi wa kikundi kiitwacho Abu Nidal Organization.

Haraka, Israeli ikatangaza kitendo walichofanya vijana wale ni 'casus belli' (yaani ni tangazo rasmi la vita!)

Israeli hakuwa inatania, kwani siku tatu baadaye Israeli ilivamia nchi ya Lebanoni kuwasaka maadui wa namna hiyo nchini humo.

Huo ukawa ni uvamizi wa pili Israeli kufanya nchini Lebanoni baada ya ule wa kwanza wa miaka michache iliyokuwa imepita, mwaka 1978.

Uvamizi uligharimu maisha ya maelfu ya watu Lebanoni, maana Israeli 'ilimwaga moto' kwa hasira kali.

Israeli walitandika Lebanoni kwa miezi mitatu, ambapo watu elfu kumi na tisa waliuawa.

Israeli wakaita vita vile 'Operation Peace for Galilee'.

Sasa basi, wakati vita vile vikiendelea, kuna kikundi cha viongozi wa dhehebu la Shia waliwaza jambo.

Walipanga kuanzisha chama ambacho malengo yake makuu yatakuwa kwanza ni KUANGAMIZA TAIFA LA ISRAELI.

Lengo la pili, KUONDOA USHAWISHI WA NCHI ZA MAGHARIBI HASA MAREKANI ENEO LA MASHARIKI YA KATI NA KUDHIBITI USHAWISHI WA SAUDI ARABIA PIA.

Tatu, KUANZISHA TAIFA LA KISHIA NDANI YA LEBANONI.

Kama utani, Hezbollah ikawa inazaliwa hivyo.

Chama hiki kilipoanzishwa kilifadhiliwa kwa kupewa msaada mkubwa na Iran.

Tangu kuanzishwa kwake hadi leo, chama hiki kikiwa kina umri wa miaka karibu arobaini, Iran imekuwa mshirika mkuu wa Hezbollah.

Kwa nini Iran?

Kwa sababu kwanza taifa la Iran ni taifa la Waislamu wa dhehebu la Shia. Lakini pia chama cha Hezbollah kilijitanabaisha kufuata siasa zile zile za Iran za Ayatola Khomeini.

Hakika Hezbollah na Iran wakashibana, wakajazwa misaada mingi sana kiasi ambacho Hezobollah imekuwa na nguvu kubwa pengine kuliko serikali ya nchi yenyewe ya Lebanon.

Fikiri kwa mfano Hezbollah ilivyoanzishwa, ilipata msaada wa wataalamu wa kijeshi wapatao 1,500 kutoka Islamic Revolutionary Guard Corps (IRGC)!

Kuna wakati Hezbollah huitwa ni 'nchi ndani ya nchi'.

Ukiangalia nembo ya Hebollah, moja ya alama zilizopo ni pamoja na mchoro wa bunduki, ambayo imeandikwa mstari uliotolewa kwenye Quran usemao 'Hakika chama cha Mungu kitadumu'

Tangu Hezbollah ianzishwe, imekuwa ikisuguaga na Israeli mara nyingi, kwa kuwa lengo kuu la Hezbollah limekuwa kuiangamiza Israeli: 'destruction of the State of Israel.'


Raphael Mtui 0762731869.
 
Nenda kasome historia ya Lebanon kuanzia 1970 kuja sasa .
Haikataliki kuwa Iran anaitumia Hizbollah Kwa maslahi yake.
Ila usisahau pasi na hiyo Hizbollah basi wakristo wenzako wangekua wameshamalizwa na sunni,Kuna vita ilizuka sunni hasa kutoka Syria waliwachinja sana wakristo wenzako hapo Lebanon.
Aliyewatetea ni Hizbollah huyo mshia unayemsea anatakiwa aondoke.
Lebanon iliingia katika political crisis zaidi ya mara mbili na kupelekea kumegwa Kwa ardhi,leo hii kama sio Hizbollah basi Lebanon ingeipoteza sehemu kubwa sana ya Kusini pamoja na nusu ya ukanda wa bahari wenye utajiri wa gesi asilia.
Hujui hao Hizbollah wameiokoa mara ngapi Lebanon na wakristo wenzako.
Vita ya 2006 wakristo wenzako hawakuwa wajinga kuwaunga mkono Hizbollah dhidi ya Israel Kusini mwa Lebanon/Bint Jubeir.

Sawa Iran anaitumia Hizbollah ila tambua Iran hiyo hiyo ndio ilisaidia kufanikisha yote hayo nilokutajia hapo juu,no free lunch in this world.
Ni sawa na wewe tu muAfrika unayeambiwa ili upewe msaada wa kimataifa kubali LGBTQ.
 
Ila Hizbollah kasambaratishwa. Sijui atainukia wapi Tena.
 
Ila Hizbollah kasambaratishwa. Sijui atainukia wapi Tena.
Waisraeli wameunda unit nyingine golan iliyokuwepo iliepelekwa kuzimu yote na hizbo. Sahau hzb kusambaa bila ground oparation ya maana kitu ambacho hamukiwezi, hapo mashariki ya kati hakuna nchi ina utalaam wa ground force Kama hzb ukitoa Iran ambayo ndio mwalimu wa hizb..............


The IOF decided to create a new special unit to operate in the Golan in order to "improve the operational response in the area, to "double the strength of the division and serve as an operational reserve," formed as a "lesson from October 7th."

This comes following numerous successful attacks by the Lebanese and Iraqi resistances on zionist military sites in the Golan over the last year.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…