Hivi ndivyo Jimmy Carter alivyobaki. Ndiyo tujue sasa dunia haina urafiki

Hivi ndivyo Jimmy Carter alivyobaki. Ndiyo tujue sasa dunia haina urafiki

Basi kama ndo hivyo Kulikuwa na Umuhimu gani wa wewe kutuletea habari za Jimmy Carter wakati hakujui na huna uhusiano nae katika "kuumbwa kwake na mwisho wake"🤣

Naona bado unazidi kuonesha jinsi akili zako zilivyo mgando.
Mtoa mada anashangaza , anyway maybe anatimiza wajibu wake ktk JF
 
Yaani Kuna mtu asiyejua Kuna kuzeeka na kufa, ila wewe ndiye umefunuliwa siri hiyo ?
Watu wanajua tu kuzeeka na kufa lakini wengi hawafaidiki na kujua huko yawezekana ni pamoja na wewe.
 
Kwa sababu yeye alikuwa raisi wa nchi kubwa tungetaraji asipatwe na shida alizonazo sasa.
Mkuu hii ni kwa mujibu wa nani?

Rais wa USA anaweza kuwa mtu yeyote yule....... yaani rais ni binadamu tu kama binadamu wengine
 
Jimmy Carter ni rais wa Marekani wa 39 ambaye mnamo oktoba 1 mwaka 2023 alikuwa akisherehekea miaka yake 99 tangu kuzaliwa kwake mwaka 1924.

Rais huyo mstaafu alitwala Marekani kuanzia mwka 1977 mpaka 1981.

Miongoni mwa mafanikio ya utawala wake ilikuwa ni kufanikisha kutiiana saini ya kurejesha uhusiano kati ya Israe na Misri mnamo mwaka 1979.

Kwa sasa Raisi huyo amepelekwa kwenye nyumba zenye huduma za afya za kuhudumia wazee baada ya kupata maradhi ya saratani isiyotibika tena.

Katika umri huo Jimmy Carter ndiye raisi aliyewahi kuishi miaka mingi zaidi na aliyebaki hai muda mrefu zaidi baada ya kuondoka madarakani.

Muhimu kwa binadamu wengine ni kujifunza kwamba katika maisha inafika muda heshima zote zinaondoka na hata marafiki binafsi, urasimu wa kimadaraka vinaisha na kuonekana mzigo na familia na kutokuwa na umuhimu wowote wa kutafutwa ushauri kutoka ofisi uliyoihudumia.

Inafika wakati vyakula vyote vizuri unavimiliki lakini hata ukivitumia havibadilishi afya ya mwili.

Dawa zozote za kutibu za hali ya juu haziwezi tena kutibu maradhi yanayokupata.

View attachment 2977746View attachment 2977693View attachment 2977691
Hivi,ulifikiria kwa umakini kabla ya kuanzisha uzi?Unajua maana ya kuzeeka?Tafuta kamusi halafu ujifunze maana ya uzee.
NB:Sijui hata kama kusoma na kuelewa unajua.
 
Back
Top Bottom