Ni kweli kabisa naonyesha hasira Kali kabisa kuna watu wamepoteza maisha, kazi, biashara ,vifungo na kuteswa na hata kupotea na wengine kulemaa kabisa tena walikua na nafasi ya kuwa na maisha mazuri na kufurahia amani na Uhuru wa bendera wa nchi hii lakini wamevikosa kwa sababu ya kutaka na kuipigania Demokrasia ya kweli.
Tuwe wa kweli kabisa bila kulinda mtu wala neno CHADEMA tu na kuendekeza urafiki na ukabila.
Hivi Mbowe aliyekua anasema Magufuli anatekeleza Sera za Chadema anaweza kuwaambia nini watu wa Mbeya au Kilombero au Temeke ,Masasi na kwingineko kuhusu Demokrasia na maendeleo?
Kama Magufuli alikua anatekeleza Sera za Chadema palikua na sababu gani ya kuanza kupinga Sera zao kila siku huku wakimshambulia Magufuli pekee badala ya mfumo mzima wa CCM?
Je, hatukushauri sana kwamba kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa Wapinzani hasa Mbowe aonane na Rais ili aweke bayana kuwa wako tayari kufanya naye kazi na kumuunga mkono kwa sharti la kuilinda Demokrasia ya nchi?
Hivi nani anayeumia kati ya Mbowe na Magufuli kwa kumtunishia Raid wa nchi misuli kwa sababu ya Chuki binafsi za kufyekwa kwa shamba lake na kulipishwa Kodi kwenye biashara zake.
Chuki zake za kubanwa ili afuate sheria amezigeuza na kuzifanya ni Sera za Chama.
Hivi kwa akili ya kawaida kabisa ni mwanasiasa gani atakubali kubaki ndani ya Chadema huku akiwa amefungwa mdomo kabisa wakati anawapiga kura wanaomuunga mkono anachokosa ni udhamini wa Chama tu!?
Kama ni kufungwa mdomo kwa maelekezo yasoyozingatia Demokrasia ni bora mtu arudi CCM ili afungwe mdomo kama Bashe lakini anawatumikia watanzania.
Leo hii Mbowe atamlalamikia nani kuhusu Demokrasia wakati ndani ya Chama chake watu wanapangiwa kila kitu bila kuhoji. ?
Ishu inawahusu wabunge kutoingia kwenye vikao kutimiza majukumu yao kwa nini isijadiliwe na wabunge wenyewe tena kwa kura?
Kunatofauti gani na wanayofanya CCM kuoitisha kila kitu kwa nguvu badala ya kura ?
Huo uwazi anaoupigania Mbowe anataka akaanze lini kuufanya kwa vitendo??
Umri wa Mbowe alipaswa aanze kurithisha vijana Demokrasia ya kweli na kwa vitendo kuanzia ndani ya choma.
Kwa umri wa Mbowe Over 60 years anajenga na kuwaachia vijana Chama cha kidikteta? Kweli !!!
Halafu anataka kuwaambia watu CCM ya Magufuli inaua Demokrasia.
Tumemshabikia mtu badala ya kujenga Chama imara chenye misingi ya Demokrasia ya kweli sasa Chama kinakufa huku damu za watu zikiwa zimemwagika kwa ajili ya kupigania Demokrasia . CUF kwa uroho wa Lipimba nayo inekufa sasa Mbowe naye anashindwa kujifunza.
TLP ,UDP , navyo pia vinakufa kwa sababu ya wenyeviti wanaoamua wanavyotaka.
Mrema anaangalia maslahi yake na kuendesha chama anavyotaka kwa manufaa yake na sasa TLP inapotea. Je, wanachama hawaoni ubovu wa katiba za Chama vyao vinavyomuenzi mtu badala ya taasisi ?
Miaka 60 Mbowe anaendelea tu kujichimbia kwenye Uenyekiti wakati Mwalimu 41 year alikua ameashakamilisha harakati za kupata Uhuru kidemokrasia bila kumwaga damu?
Nchi hii haitakuja kupata katiba mpya wala uchaguzi huru kama watu wenyewe ndio akina Mbowe? Hii nchi INA siasa za kistarabu tangu ukoloni . Watu wajashindana kwa hoja na kutafuta haki kwa ushawishi zaidi na sio kutumia nguvu. Chadema na Mbowe alipokua amefikia alipaswa kuingia Ikulu kila siku na kumbana Rais kwa mazungumzo tu huku pia akimbana spika mpaka hata nyumbani kwake kudai haki katika chaguzi na bungeni na kwenye siasa lakini sio kutumia mbinu za kibabe na kuwafukuza viongozi wenzake kila siku bila mafanikio zao ya wanaofukuzwa kupanda chati kimaisha na kisiasa baada ya kurudi CCM.
Hivi kwa akili ya kawaida kabisa mtu anaweza akasema kuwa Mbowe ni kiboko ya CCM wakati amemshindwa hata Sabaya tuu jimboni kwake?
Kwa nini hatuoni maandamano kule Hai kupinga anayofanya DC.
Kwa nini anakimbilia kwenye majimbo ya watu wengine kama sio ukabila kuhofia watu wa nyumbani kwake wasivunjwe miguu.!?
Nani amjengee Chama wakati ndiye mnufaika namba moja na ukoo wake?
Wajanja kama akina Selasini,Molell, Komu na kesho kutwa Jafari wote watamkimbia na kurudi CCM.
Hata Kileo wa Mwanga ajitafakari bora arudi CCM asaidie kwenye Kampeni zijazo ili atulie na sio kumpa kuchwa Mbowe asiyejali juhudi za mtu kwa tamko la kidikteta.
Sent using
Jamii Forums mobile app