Hivi ndivyo Katiba ya CHADEMA inavyosema kuhusu Wabunge wake kuchangia chama

Hivi ndivyo Katiba ya CHADEMA inavyosema kuhusu Wabunge wake kuchangia chama

Na mimi nauliza kukatwa 10% ya mshahara na kukatwa 10%ya posho kupi kuna afadhali?
Je chama twawala kina hilo swala la wanachama wake kuchangishwa?
Na kwa nini malalamiko dhidi ya chadema yamekuwa mengi haswa baada ya hamahama kutokana na kusumbuliwa na chama twawala? Yaani kila anayeondoka anasababu yake....

Nahitimisha kwa kuuliza
JE CHADEMA INA JIMALIZA YENYEWE AU INAMALIZWA NA UKANDAMIZAJI WA CHAMA TWAWALA.? Wataalamu wa siasa nisaidieni katika hili.



MÊmENtO HoMO
Chadema haijimalizi ila, ni kwamba hao wote walikua kwetu lakini hawakua wetu, wangekua wetu tungepigana vita pamoja.
Kufa kwa chadema ni kutokubaliwa na wananchi ila Sio hao wachumia tumbo tuliokua nao..

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Hapo wamesema posho na sio mshahara, tofautisha hilo, posho unaweza usiwe bungeni hivyo hiyo haipatikani kuchangia lakini mshahara upo na ni kiwango sahihi, bado kuna dhuruma hapo,

Maana mbunge anaweza asichangie endapo hatakuwa na shughuli za kibunge kwa hiyo kukata kwenye mshahara ninuonevu.
 
Alichotaka kuonesha kuwa Mh.supika yuko sahihi alipokuwa anamshambulia Mbowe kuwa anawanynyasa wabunge, anawalata mishahara kimabavu......!!!
Kumbe Lijuha halijui katiba ya chama chake au ameamua tu kujifanya juha!

Sent using Jamii Forums mobile app

Ni kweli kwa sababu kwenye sheria hiyo wamesema posho na sio mshahara, kwa hiyo kuwakata kwenye mshahara ni kuwaonea,

Nilichogundua kumbe huko ufipa akili zote ni matope hamjui sheria, kitu kimeandikwa posho nyie mnashabikia kukatwa mshahara,
 
Alisoma katiba akakubaliana nayo........kaka hata hujiulizi kwamba haya anayaona dakika ya 89?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuyaona dakika ya 89 sio kigezo kwamba hayapo na hayana mantiki ya kufanyiwa kazi.

Watu wanaongelea katiba ya CDM bila ya kuongelea ujumbe wote wa yule mbunge.

Katumwa na watu halafu anaambiwa tu kwa amri asihudhurie vikao vya bunge, hatuioni dharau ya chama kimoja kwa wananchi ambao ndio wanampa ridhaa mbunge ya kuwemo mle bungeni.
 
Posho ni mshahara we kilaza? katiba inasema watakatwa posho na si mshahara kama ambavyo inafanyika, huo ni ukiukwaji mkubwa wa katiba ya chama.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kasema (Lijualikali) wanakatwa 500000 kila mwezi-hakusema zinatoka kwenye mshahara wala posho. Katiba inasema posho. Issue hapa je katiba ya CDM inaruhusu makato ya kuchangia chama? Supika anataka kutuambia makato hayo ni haramu wakati katiba inaruhusu. Kwangu mimi hii ndiyo issue Supika anapotosha full stop. Hizo 500000 wanazipataje mimi hainihusu wao ni watu wazima waulizane huko huko CDM.
 
Baada ya muda mfupi nitaweka hapa hela alizolipwa Lijuakali pamoja na A/C namba iliyotumika , nasubiri ushauri wa mwanasheria wangu

Wewe una roho ngumu mkuu, mimi nisingesubiri ushauri wa mwanasheria kwa mpuuzi anayelia kudai kaonewa kumbe mnunuzi amefika bei. Bandika hiyo skendo hapa mkuu
 
Wewe una roho ngumu mkuu, mimi nisingesubiri ushauri wa mwanasheria kwa mpuuzi anayelia kudai kaonewa kumbe mnunuzi amefika bei. Bandika hiyo skendo hapa mkuu
Nakumbuka mlivyokuwa mkimsifia kuwa ni kamanda kipindi mnamtia kichwa hadi kufungwa. Hiyo ndiyo hasara ya kukurupuka kusifia kila ujinga. Sasa kawaumbua. Analiaaaaaaaaaa!!!!

Mkumbuke hao wote mnaowasifia kuna wakati mtawesemea hayohayo.
 
shida sio kuchanga shida ni pesa zinafunwa na mbowe na familia yake.
mbowe katafuna zaidi ya bilioni mbili.pesa hazitumikii chama bali zina mnufaisha mtu mmoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom