Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Licha ya mafanikio yao makubwa katika muziki, wasanii wa Bongo wamekuwa wakipiga hela kupitia biashara na miradi tofauti nje ya muziki:
1. Diamond Platnumz – Mbali na muziki, Diamond amejikita kwenye sekta ya habari akiwa na Wasafi TV na Wasafi FM. Pia, alianzisha lebo ya muziki WCB Wasafi, iliyotoa nyota kama Harmonize, Rayvanny, Zuchu, Lava Lava na wengina, pia ameingia kwenye biashara ya kubashiri kupitia kampuni ya Wasafi Bet.
2. Alikiba – Alikiba amewekeza kwenye vyombo vya habari pia, akiwa na redio na televisheni (bado haiko hewani). Vilevile, amejikita katika kilimo kama chanzo cha kipato chake nje ya muziki. King Kiba amewekeza kwenye kilimo cha mazao tofauti tofauti ya kibiashara ikiwemo mboga mboga, nyanya na vitunguu ambapo amesema amelichagua Mkoa wa Dodoma kwasababu kuna fursa za kilimo na anaamini atapata pesa nyingi.
3. Sugu (Joseph Mbilinyi) – Rapper mkongwe Sugu amewekeza katika sekta ya hoteli, akimiliki biashara inayomuingizia kipato nje ya tasnia ya burudani.
4. Shilole – Msanii huyu wa muziki na filamu ameanzisha biashara ya chakula kupitia mgahawa wake maarufu SHISHI FOOD, katika mikoa kadhaa hapa nchini na kuwa shughuli maalum ya kumuingizia kipato zaidi nje ya tasnia ya muziki na filamu.
5. Jux – Jux amepanua wigo wake wa mapato kwa kuanzisha na kuendesha biashara ya mavazi inayojulikana kupitia brand yake ya African Boy. Mavazi yenye chapa yake yanavaliwa na msataa na watu wa kawaidi ndani na nje ya Tanzania na ana maduka kadhaa kwenye nchi za Afrika Mashariki.
6. Billnass – Mbali na kuendelea na muziki, Billnass ameingia kwenye biashara ya simu za mkononi.
7. Nandy – Nandy, ambaye anajulikana kama ‘The African Princess,’ amejikita kwenye biashara ya urembo, akitoa bidhaa za vipodozi na huduma za urembo. Pia anamiliki lebo ya muziki ambayo inamsimamia msanii Yammi.
8. Ommy Dimpoz – Yeye ni Creative Director wa kampuni maarufu ya GSM Group, akisimamia ubunifu katika masuala ya mitindo na biashara.
Omary Nyembo maarufu Ommy Dimpoz ana-cheo kama Pharrell Williams, mwimbaji na rapa wa Marekani, cha "Creative Director", yaani Mkurugenzi wa ubunifu, mbeba maono ya kampuni kwa kuhakikisha kwamba mbinu na thamani za kampuni zinaakisiwa katika bidhaa, huduma, na matangazo. Anaongoza ubunifu na kuhakikisha matokeo yanaendana na malengo ya kampuni.
Ommy Dimpoz ambaye ni maarufu kwa muziki ni Creative Director wa kampuni ya GSM Group, iliyochini ya mdhamini wa mabingwa wa kihistoria Yanga SC, Ghalib Said Mohamed na Pharrell Williams wa Louis Vuitton au LV, kampuni maarufu ya bidhaa za kifahari ya Ufaransa, tangu Februari 2023, akiwa Men's Creative Director akivuta wastani wa dola milioni 25 kama Tsh. Bilioni 67.9 kwa mwaka.
Rayvanny pia alidokeza kuwekeza kwenye manukato kama ilivyo kwa Rapa Mwana FA na Fyn by Falsafa.
Ongeza list ya biashara/dili nyingine zinazowaingizia pesa wasanii wa bongo
Soma pia ==> Kesi ya diamond karanga, Wasafi na Kusaga ilivyofika mwisho mahakamani