Lord Denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 23,491
- 57,973
Tanzania kwa sasa inafahamika rasmi kama nchi ya uchawa, ujinga, umasikini, rushwa, ufisadi, pamoja na ubabe wa dola dhidi ya Wananchi. Haya yote hayajafanikiwa kwa mara moja. Ni matokeo ya mfululizo wa masuala kadhaa yaliyofanywa na dola ya CCM yaliyolifikisha Taifa letu hapa.
Kama ulikuwa hufahamu ilikuwaje Tanzania ikafika hapa ilipo leo, naomba nikupeleke taratibu kwenye masuala yaliyofanywa na CCM mpaka kulifikisha hapa Taifa.
1. Kuua Mifumo imara ya Utendaji na Uwajibikaji kwa kukataa Mabadiliko ya Katiba tangu mwaka 1992 ili kuondoa mamlaka makubwa aliyopewa Rais Kikatiba: Kupitia hili CCM walifanikiwa kuteua watu kwenye nafasi kadhaa za utendaji na utaalam Serikalini ambao kimsingi hawakuwa na sifa za kiutaalamu na kiutendaji bali ni makada wa Chama na kuwa na undugu/ urafiki na Viongozi.
Matokeo ya hili ni kwamba nchi imekuwa na kasi ndogo ya maendeleo kutokana na kuwa na watu wasiostahili kwenye nafasi za Maamuzi. Endapo Rais asingekuwa na haya mamlaka wakuu wa mashirika na vitengo mbalimbali Serikalini wangepatikana na njia za ushindani hivyo kupata watu sahihi na wenye uwezo wa kulivusha Taifa na kulipatia maendeleo ya kweli.
2. Kuuweka Mhimili wa Mahakama chini ya imaya yao kwa kutunga Sheria ya Mahakama ya mwaka 2011 iliyowaweka Wakuu wa Wilaya na Mikoa kuwa Wenyeviti wa Kamati za Nidhamu za Mahakimu. Kupitia hili CCM walifanikiwa kuwaweka makada wao ambao ni wakuu wa Mikoa na Wilaya kuwa wawajibishaji wakuu wa Mahakama. Kuanzia mwaka huo, nchi ilianza kuona Mahakama ikianza kukengeuka na kutoa maamuzi ambayo yanakiuka misingi ya haki na ustawi wa Wananchi. Hili limeleta madhara makubwa zaidi kwa kuzuia uwekezaji mkubwa na wa kudumu nchini kwa sababu Wawekezaji wengi hawana imani na Mahakama zetu kama ilivyo kwa Wananchi.
3. Kuendelea kuwatumia Wanajeshi katika nafasi za kisiasa hasa Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambazo kimsingi zinawafanya kuwa makada wa Chama cha Mapinduzi. Ikumbukwe Wakuu wa Mikoa na Wilaya pia ni wenyeviti wa Kamati za Siasa za Mikoa na Wilaya chini ya Chama cha Mapinduzi. Wanajeshi wanapopewa vyeo hivi wanaondoka kuwa sober na kuanza kuwa makada wa Chama cha Mapinduzi. Matokeo yake hakuna wa kukiwajibisha Chama cha Mapinduzi hata pale kinapowakosea Wananchi.
4. Kuhodhi ajira za vyombo vya Ulinzi na Usalama hasa TISS kwa kuwapenyeza makada wao. Kwenye hili baada ya kuondoka mfumo wa vyama vingi, CCM waliendelea kuinasibisha TISS na chama chao. Kuingiza makada wengi wa Chama cha Mapinduzi hadi kufikia kuchanganya maslahi ya CCM/Viongozi wake na maslahi ya Taifa.
5. Kuzuia fikra huru kwa Kutunga Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015 iliyolazimisha Takwimu zote kufanywa kwa ridhaa ya Serikali. Kwenye hili CCM wameua fikra huru katika kufanya Tafiti huru ambazo kimsingi ndizo chimbuko la maendeleo ya kweli ya Jamii yeyote ile. Kukosekana Tafiti huru sio tu kunanyima ajira kwa vijana ila kunalifanya Taifa kutokujua nini chanzo hasa cha matatizo yanayowakabili na namna ya kuyatatua
6. Kutompa Mkurugenzi wa TAKUKURU kinga ya Kikatiba ya kutoondolewa Madarakani na Rais. Sote tunajua kuwa kansa kuu iinayorudisha nyuma maendeleo ya Taifa hili ni rushwa na ufisadi hasa Rushwa kubwa zinazofanywa na Viongozi wa juu na Wanasiasa. CCM kwa sababu Viongozi wao hawataki kuacha rushwa waligoma kumpa Mkurugenzi wa TAKUKURU hadhi na kinga ya Kikatiba hivyo kuweza kuihodhi taasisi hii. Matokeo ya hili ni kushamiri kwa rushwa ambayo kumeendelea kuimaliza Tanzania kila siku kama kansa.
7. Kukataaa hoja ya Mgombea Binafsi na Tume Huru ya Uchaguzi. Haya mawili yamewafanya CCM kuhodhi siasa za Taifa hili na wao kuwa ndo wenye sauti ya mwisho juu ya nani awe kiongozi na nani asiwe kiongozi. Hili limewanfanya wao kutoogopa kuwajibika kwa Wananchi kwa namna yeyote ile kwa sababu wanaloliamua wao ndilo linalokuwa na sio wanaloliamua Wananchi.
Ujumbe wangu kwenu Watanzania.
CCM wameshaliua hili Taifa. Ili tuanze upya hatuna budi kupambana sana na No Reforms No Election.