mcTobby
JF-Expert Member
- Feb 16, 2018
- 7,894
- 22,679
Je, umewahi kusikia kuhusu mtu anayepanda ndege leo, lakini akatua mahali anapoenda tarehe ya jana yake?
Inaonekana kama muujiza au filamu ya kubuni, lakini huu ni ukweli halisi unaotokea kila siku katika usafiri wa anga ulimwenguni.
Siri kubwa haitokani na kasi ya ajabu ya ndege, bali inatokana na jinsi dunia yetu ilivyogawanywa katika kanda za muda na kuwepo kwa Mstari wa Kimataifa wa Tarehe (Intenational Date Line) unaopatikana katikati ya Bahari ya Pasifiki.
Ukivuka mstari huu wa kijiografia kuelekea upande wa kulia, yaani Mashariki, unakuwa umerudi nyuma saa 24 kamili kwenye kalenda. Kwa sababu muda unakuwa umeenda mbele sana upande wa Asia na Australia kuliko kule Marekani, tofauti hii ya masaa inakuwa kubwa kuliko masaa ambayo ndege inatumia ikiwa angani.
Katika mfano wa kwanza, msafiri anayepanda ndege jiji la Tokyo nchini Japani siku ya Jumapili saa 11:00 jioni atatumia masaa 10 angani, cha kushangaza ni kwamba atatua jiji la Los Angeles nchini Marekani siku ya Jumamosi, ambayo ni jana yake, saa 11:00 jioni hivyo kupata nafasi ya kuishi saa zile zile na siku ile ile mara mbili.
Muujiza huu pia unajidhihirisha katika safari ya kutoka Sydney nchini Australia kwenda Honolulu kule Hawaii, Marekani.
Ndege inapoondoka Sydney siku ya Jumatano saa 6:00 mchana na kuruka kwa muda wa masaa 10, inatua Hawaii siku ya Jumanne saa 11:00 alfajiri, ambapo kule inakuwa bado ni jana yake kabisa.
Hali hii imekuwa fursa ya kipekee kwa watu wanaotaka kusherehekea Mwaka Mpya mara mbili kwa kukodisha ndege binafsi kwa kuanza kusherehekea Auckland nchini New Zealand usiku wa manane, kisha wanapanda ndege haraka kuvuka mstari wa tarehe na kutua visiwa vya Cook au Hawaii ambako bado ni mchana wa tarehe 31 Desemba, na hivyo kusubiri kuamkia Mwaka Mpya kwa mara ya pili.
Kusafiri kwenda jana si uchawi wala sayansi ya kubuni, bali ni hesabu tu za kijiografia.
Dunia inapozunguka, maeneo ya Mashariki yanaona jua mapema zaidi kuliko maeneo ya Magharibi, na hivyo ukikimbizana na mzunguko wa dunia kwa kutumia ndege, unakuwa unashinda muda na kurudi nyuma kwenye kalenda.
Cc.Aviation media