Hivi ndivyo ninavyo ingiza kipato cha 30,000 kwa siku baada ya kubadili fikra zangu

30k per day ni baada ya kutoa gharama za siku husika au..?
Cost ya kutengeneza malighafi imekaaje hapa mkuu? Je, ni kila siku unapata wateja?
Unatengeneza lita ngap za dawa kwa siku?
Faida ya lita moja ya dawa ikoje?
Lita ngap za dawa kwa wastani unauza kwa siku?
Facebook una page makhsusi kwaajili ya biashara au unatumia personal?
Unatumia sponsored ads kujitangaza au ile kawaida?
Umesema hauna ofisi, what's ur future plans?
Ukubwa wa soko lako ukoje?
Competition kwny biashara yako ikoje?
Unautofauti gani kihuduma / kibidhaa na wafanyabiashara wengine wanaofanya biashara Kama yako?
 
Ndiyo mkuu hiyo 30k ni Baada ya kutoa gharama zote.

Cost ya Kutengeneza dawa inategemea na kiasi gani nahitaji Kutengeneza kwa wakati huo japo mtaji wake si mkubwa 32000 ina wezesha kupata mali ghafi za kutoa zaida ya Lita 60 za dawa.

Kuhusu wateja ni kila siku ndiyo maana mi mwenyewe nahakikisha naingiza wateja wapya 5 kila siku hata Kama sito wahudumia siku hiyo ni akiba ya siku nyingine wakati huo tayari nime pata mteja mmoja au wawili tu wa uhakika kwa siku.

Dawa sitengenezi kila siku kutokana na kwamba,mimi kwa sasa natumia kufanyia shughuri zangu za usafi japo wapo baadhi wanao nunua baada ya kumfanyia huduma almost ni mara 3 kwa wiki ndo natengeneza dawa.

Faida ya dawa niki uza ni 40% kwa Lita 1 japo faida ni kubwa zaidi niki fanya usafi maana natumia kidogo tofauti na nikiuza.

Kuhusu mauzo ya dawa,kwa sasa mkuu mimi najihusisha na usafi tu sija anza kuuza dawa kutokana na namna nnavo fanya kazi sina watu wengi asilimia kubwa nawauzia wateja nilio wafanyia huduma tu,na mwanzo nili wahi toa uzi kuwa vijana wenzangu tuungane kwenye ujasiriamali huu ili tuwe na team kubwa tuwekeze pakubwa na tugawane majukumu lakini muitikio ulikuwa mdogo wengi wali fananisha na Mr Kuku

Kuhusu Facebook,nna business page pia nafanya sponsored ili kuwafikia watu wengi zaidi.

Kuhusu ofisi mkuu,nna lengo la kusajili kampuni au business name then niwe na ofisi ambayo ipo kisheria that is my future plan kwahyo najikusanya kufanya yote hayo yawezekane.

Kuhusu ukubwa wa soko,kwa namna nnavo ona uhitaji ni mkubwa sana watu wana uhitaji na hii huduma kwa kiwango kikubwa maana huwa naitwa mpaka mikoani kwa sasa kwenda kufanya huduma hii ya usafi maalum hasa katika Viwanda, Hotel na shule.

Kuhusu Competition,ushindani upo kwa makampuni makubwa ya usafi yaliyopo kwenye soko muda mrefu hata kama hawana huduma hii ya kung'arisha Tiles na Masink huwezi pata tenda sehemu ambazo tayari wana toa huduma na baadhi ya sehemu wanazo fahamika kutokana na kwamba wao wana mitaji mikubwa wana uwezo kuji tangaza kwenye TV, Radio,Magazeti pia wana watu wa marketing wanao fanya hiyo kazi hata kama huduma zao si bora kwa kiwango lakini wao ndo tayari wame teka soko kutokana na uwezo wa kuji tangaza kwenye Media kwahyo mimi nabaki na wale wa majumbani,Hotel,Shule na Viwandani pia ni kwa one time service si kwa mkataba maana sina kampuni.

Kuhusu utofauti kihuduma na bidhaa,

1.Kuhusu huduma
Nna extra services ambazo wengine hawafanyi hivyo kutokana na kukosa utaalam kwenye eneo hilo
Mfano, makampuni mengi ya usafi haya fanyi huduma ya kung'arisha Tiles na Masink katika sehemu wanazo toa huduma mfano hospital na taasisi nyingi za umma ama binafsi.

Nna uwezo wa kung'arisha kurudisha mng'ao mpya kabisa kama material yalivyo toka dukani hata Vioo vya Alminium vilivyo shindikana kung'aa nna uwezo wa kung'arisha

2.Kuhusu bidhaa

Kwa upande wa bidhaa nnazo tengeneza zina utofauti mkubwa katika kufanya kazi tofauti na zile za dukani ambazo tayari zipo kwenye soko kutokana na brand yao kuwa kubwa,mfano wateja wengi nilio wapa bidhaa zangu wana sema dawa yangu ina ishinda hata Aro na Vim bidhaa kongwe za usafi maana mimi dawa zangu zina fanya kazi zaidi ya moja,mfano mtu aki chukua dawa ya kung'arisha Tiles ita msaidia pia kung'arisha Masink ambayo ina fanya kazi ndani ya dakika 15 tu,pia Dawa ya kung'arisha sofa ina uwezo wa kuondoa madoa yote mpaka michoro ya peni kwenye sofa ya kitambaa ama Leather ambayo pia ina uwezo wa kusafisha carpet.
 
Huko facebook page yako unatumia Jina gani?.

Harafu nisaidie kidogo kwenye hili la sponsored adds hivi unawalipaje?
 
Huko facebook page yako unatumia Jina gani?.

Harafu nisaidie kidogo kwenye hili la sponsored adds hivi unawalipaje?
Uki maliza tangazo lako baada ya hatua zote za uandishi kukamilika na Audience selection (Gander and Location) una takiwa uwe na MasterCard kwa ajiri ya kulipia (naongelea niliyo zoea kutumia mimi japo zipo nyingine) una chagua kwenye list pale

Uta bonyeza settle account ili ku add hiyo card number yako, Expire date ya card,CVV n.k.

Uki maliza hapo uta fuata maelekezo japo kulipia kwa badget ndogo kuanzia $1 unalipia bill mpaka tangazo liishe kwa badget kubwa una katwa before

Hatua zake una weka pesa kwenye account yako kama ni bank au simu

Kama Mimi natumia M-pesa MasterCard na Airtel MasterCard.

Siku ya kulipia iki fika wata kata pesa kwenye account yako ikiwa ume weka au kama hauna utakapo weka utaingia kwenye account yako ya biashara Facebook kisha kuna sehemu ya juu utaona maelezo ya deni lako na button ya pay now then uta bonyeza hapo pesa ita katwa automatically toka kwenye account yako.
 
Hongera sana kwa ubunifu na kazi njema unayoifanya. Mungu azidi kukubariki ktk kazi ya mikono yako, akupe watu wengi zaidi... Mafanikio mema!
 
Asante kwa maelezo.
Nyongeza ya swala je ukilipia kwa mfano 1$ hapo tangazo lina reach watu wangapi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…