Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #21
Sheikh Hassan bin Ameir alikuwa mwanasiasa.Mtoto...
Jibu lako nimeitoa kutoka kwa ndugu yangu Hamisi Hababi hilo hapo chini:
"Sheikh Mussa Rehani Makuka alipewa Kadi ya TANU msikiti wa Ijumaa Kitongoni Ujiji na Sheikh Hassan Bin Ameir siku ya Ijumaa baada ya Sala.
Sheikh Hassan Bin Ameir akiwa katika juhudi za kuhuisha TANU na Harakati za Uhuru.
Hata Bwana Kambarage Nyerere alipokuja Ujiji kwa Mara ya Kwanza walikuja na Barua maalum aliyokuja nayo Sheikh Suleiman Taqadir toka kwa Sheikh Mohamed Ramia wa Bagamoyo kuwaomba wazee wa Ujiji wawapokee vijana wao."
Sent using Jamii Forums mobile app
Mwaka wa 1950 baada ya mapinduzi ya uongozi wa TAA yaliyofanywa na Hamza Mwapachu na Abdul Sykes kumtoa madarakani Thomas Plantan, ikatengenezwa TAA Political Subcommittee wajumbe wakiwa hawa wafuatao:
Dr. Vedasto Kyaruzi, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia.
Hii kamati ndiyo iliyotengeza mapendekezo ya katiba ya Tanganyika yaliyopelekwa kwa Gavana Edward Twining.
Lakini kubwa ni kuwa hotuba ya TANU iliyosomwa UNO na Mwalimu Nyerere inatoka kwenye waraka huu uliosainiwa na hii Political Subcommittee na sahihi ya Sheikh Hassan bin Ameir ipo kwenye hiyo document.
Ukinidai ushahidi wala sitakupeleka kwa Nyaraka za Sykes nitakurejesha kwa Cranford Pratt katika kitabu chake, "Critical Phase in Tanzania..." (1976).
Sheikh Hassan bin Ameir ana mengi sana.
Sent using Jamii Forums mobile app