Hivi ndivyo Sheikh Hassan bin Aameir alivyoweza kuiingiza Daawat – ul – Islamiyya Burundi kusaidia ukombozi dhidi ya ukoloni wa Wabelgiji

Hivi ndivyo Sheikh Hassan bin Aameir alivyoweza kuiingiza Daawat – ul – Islamiyya Burundi kusaidia ukombozi dhidi ya ukoloni wa Wabelgiji

Mtoto...
Jibu lako nimeitoa kutoka kwa ndugu yangu Hamisi Hababi hilo hapo chini:

"Sheikh Mussa Rehani Makuka alipewa Kadi ya TANU msikiti wa Ijumaa Kitongoni Ujiji na Sheikh Hassan Bin Ameir siku ya Ijumaa baada ya Sala.

Sheikh Hassan Bin Ameir akiwa katika juhudi za kuhuisha TANU na Harakati za Uhuru.

Hata Bwana Kambarage Nyerere alipokuja Ujiji kwa Mara ya Kwanza walikuja na Barua maalum aliyokuja nayo Sheikh Suleiman Taqadir toka kwa Sheikh Mohamed Ramia wa Bagamoyo kuwaomba wazee wa Ujiji wawapokee vijana wao."

Sent using Jamii Forums mobile app
Sheikh Hassan bin Ameir alikuwa mwanasiasa.

Mwaka wa 1950 baada ya mapinduzi ya uongozi wa TAA yaliyofanywa na Hamza Mwapachu na Abdul Sykes kumtoa madarakani Thomas Plantan, ikatengenezwa TAA Political Subcommittee wajumbe wakiwa hawa wafuatao:

Dr. Vedasto Kyaruzi, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia.

Hii kamati ndiyo iliyotengeza mapendekezo ya katiba ya Tanganyika yaliyopelekwa kwa Gavana Edward Twining.

Lakini kubwa ni kuwa hotuba ya TANU iliyosomwa UNO na Mwalimu Nyerere inatoka kwenye waraka huu uliosainiwa na hii Political Subcommittee na sahihi ya Sheikh Hassan bin Ameir ipo kwenye hiyo document.

Ukinidai ushahidi wala sitakupeleka kwa Nyaraka za Sykes nitakurejesha kwa Cranford Pratt katika kitabu chake, "Critical Phase in Tanzania..." (1976).

Sheikh Hassan bin Ameir ana mengi sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ingeleta maana kama historia ya wazee wako ingekuwa imeandikwa , halafu ikafutwa, lakin kulalamika tu eti imefutwa, wakati haijawah kuandikwa, haileti maana, mfano, waasisi wa TANU walikuwa 17, lakini mpaka leo kuna wengine hawajulikani kabisa, mfano Geremano Pacha, Joseph Kamalando, Milinga, Kisunguta Gabara, Patrick Kunambi, bora hao akina Sykes wanajulikana kidogo
Laki...
Si nia yangu kushusha mchango wa waasisi wa TANU katika kundi lile la watu 17.

Katika kundi lile nitakutajia mtu mmoja ambae aliisaliti TANU na akasababisha Ally Sykes aliyepelekwa uhamisho wa kazi Moshi kushitakiwa kwa kosa la rushwa.

Joseph Kimalando baada ya kurudi Moshi kutoka ule mkutano ulioasisi TANU akakataa kufungua ofisi ya TANU pale Moshi mjini.

Hii ikasababisha msuguano mkubwa baina yake na Yusuf Olotu.

Olotu akahangaika sana na kwa kushirikiana na wazalendo wengine na wengi wao akina mama kama Mama bint Maalim, Halima Selengia, Lucy Lameck, Melkezedik Samuel kwa kuwataja wachache wakafungua tawi la TANU.

Joseph Kimalando alipoona kashindwa katika juhudi zake za kuhujumu TANU akajiunga na chama cha wakoloni United Tanganyika Party (UTP).

Baada ya kuhamia UTP Joseph Kimalando ndipo akala njama na Waingereza dhidi ya Ally Sykes aliyekuwa anamtia hima Yusuf Olotu afungue tawi la TANU bila ya Kimalando.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom