Hivi ndivyo tulivyotapeliwa na Ontario wa TMT kwenye Forex

Fid Q aliwahi kusema neno lenye utamu siku zote halina ukweli na neno lisilo na utamu ndio lenye ukweli ndani yake. Tuwe makini sana na maneno matamu ya watu wa kariba ya Ontario.

Kwenye ile thread yake ya Namna alivyopiga milion 19 alipata kusema hivi "shika akili zao waachie mioyo yao" ndio kauli mbiu yake guys tuwe makini dogo asishike akili zetu kirahisi.

Kama Juma Nature vile alivyosisitiza kwenye ngoma yake ya mshikemshike ndege tunduni..sisi wajanja tumekimbia...! Ahahaha!
 
Mbona huyu dogo alikuwa pale na watu wazito sana yani kwaiyo max ruge mtahaba na ujanja wake kala za uso Ay kwa kweli Ontario ni mtu hatari
Sifa ya tapeli ni kukupofusha na maneno sukari ili uingie kingi akukamue!

Ila ndio maana hata sijutii kupigwa kama hadi watoto wa mjini akina Ruge, AY wamepigwa Mimi ninaetoka Ikungu lya mbeshi nina ujanja gani zaidi wa kuruka kiunzi cha Ontario?

Thus, shit happen bru!
 
Ulitaka awe anatumia nini mkuu??? Ninavyojua mimi true forex trader ni yule atumiae candlestick,resistance and support, kuchambua soko.....Yaani kuwa pure price action trader.


Nijibu kwanza nilichokuuliza kabla sijaongea ninachotaka kuongea


Ngoja nimsaidie kujibu mkuu wangu...uko sahihi kabisa kusema kuwa true forex trader ni yula anayetumia candlestics, resistance and support kuchambua soko....labda niongeze na chart patterns pamoja na trend..Kama unavojua cardinal rule number 1 ya forex is Trend is your friend Never go against the trend. Sasa mzee baba Cre mara nyingi sana huwa anaenda against the trend na ukimstua ukamwambia mbona labda trend ni down ila yeye anatoa call ya buy huwa anakuwa tu mbishi na kang'ang'ania kuwa endelea kuhold buy trades wakati trend inaruhusu sell.

Kingine sio mzuri sana kwenye kusoma candlesticks na chart patterns kuna vitu huwa analazimisha...kwa mfano anaweza sema kuna double top au double bottom kwenye tf FULANI wakati kimsingi haipo'

Kingine huwa haheshimu support and resistance...kwa mfano mnaweza kuwa mnatrade pair fulani e.g GBPJPY sell labda na mnakuwa mnamake profit kabla haijafika kwenye support anasema tp halafu atamake call nyingine baadaye,,,,hyo baadaye akimake calll anasema buy kwa hyo hyo pair ambayo bado haijafika kwenye support...sasa mkuu hapo ndo kilio kinaanza. Kwa kifupi jamaa bado hajaiva kuwa mentor analazimisha tu.
 


Mkuu wangu simtetei Ontario ila najua kabisa nafsi yake inaumia sana kwa hiki kilichotokea..Ujanja ujanja kwenye biashara ni kitu cha kawaida sana na hata mm nafanya biashara na natumia ujanja ujanja sana..Sema tu ujanja wenyewe unaotumia usije siku moja wateja wako wakaung'amua maana ndo itakuwa mwisho wa hyo biashara. Alichobugi sana ontario ni kufanya biashara na watu ambao sio sahihi..Kusingekuwa na huku kupoteza hela consintently wala haya malalamiko unayosikia sasa usingeyasikia..Hata wewe usingeleta huu uzi hapa endapo tangia uanze kutrade ungekuwa umepata labda loss mbili tatu. Kilichosababisha haya yote yanaibuka ni loss za kila siku zilizosababishwa na call za Cre ambaye kimsingi hajaiva kuwa Mentor bali analazimisha tu. Kimsingi Ontario kwenye kutafuta mentor hapo ndo alibugi big time.
 
Dahh ila Ontario anajua kuandika bana acha kabisa, anajua kushawishi yaani kipaji chake cha kushawishi akikitumia vizuri kitamfikisha mbali ila sio kwa hapa JF manake pameshachafuka. Nilihamasika kabisa na mimi ningekuwa mmoja wenu sasa hivi. Mungu amenisaidia, nikajisemea moyoni ngoja nisubiri awamu ijayo kumbe Mungu ananiongoza. Asante Mungu [emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Zile call alikuwa anafanya makusudi,BB broker hawezi fanya uhuni wake bila msaada wa mtu wake ataepotosha newbies. Mission accomplished


Mzee baba Singo upooooo...nakumbuka kwenye uzi wa mwanzo wa forex tulikuwa tunaelimishana sana kuhusu hii mambo na kupeana maujuzi kibao kibao...Kwa kifupi sio kuwa Cre alikuwa anafanya makusudi kwa zile call zake ni kwamba jamaa bado ni mchanga sana kwenye forex sema tu analazimisha mambo. Na kwa mwanzoni tulimake hela maana alikuwa naiba analysis za watu anatuletea..alipogundulika akajitoa kwenye hilo group alilokuwa anaiba analysis na kubaki yeye kama yeye....baada ya hapo ndo dhahama la loss likaanza...Cre bado sana mkuu wangu...bado sana yaani.
 
Umeandika kwa uchungu sana toka moyoni..... huyu Ontario kipaji chake n kuandika tu story.. ila sio professional trader... hata zile story humu JF za yeye kupiga PESA nying through FOREX n za kutunga tu.
 
Chief wewe unadhan Ontario alikuwa hajui janja janja ya cre... alikuwa najua kila kitu... anajua cre n mweupe hajui kitu.. kimsingi Ontario alidhamiria kbsaaa kupiga watu PESA... ujanja ujanja mwingi kumbe mpigaji tu....
 
Chief wewe unadhan Ontario alikuwa hajui janja janja ya cre... alikuwa najua kila kitu... anajua cre n mweupe hajui kitu.. kimsingi Ontario alidhamiria kbsaaa kupiga watu PESA... ujanja ujanja mwingi kumbe mpigaji tu....
Yeye mwenyewe Ontario alikuwa hatumii call za Cre iweje sisi hatuache tutumie call za cre kwa zaidi ya miezi 6?

Scammer murfaka!
 
Chief wewe unadhan Ontario alikuwa hajui janja janja ya cre... alikuwa najua kila kitu... anajua cre n mweupe hajui kitu.. kimsingi Ontario alidhamiria kbsaaa kupiga watu PESA... ujanja ujanja mwingi kumbe mpigaji tu....


Sina uhakika sana na hilo ila huwa najua kumsoma sana mtu na kimsingi simuoni ontario kama tapeli ila namuona kama kijana ambaye ni very ambitious yaani anataka kuwa mtu fulani hapa tanzania. Na kama lengo lake ni kuwa mtu fulani sidhani kama anaweza kukubali kuonekana tapeli waziwazi maana ndoto yake ya kuwa mtu fulani itayeyuka. Kimsingi namuona kama mtu anayetaka kuachieve a lot ila sio tapeli wala mpigaji. Namuona kama mtafutaji na katika utafutaji ujanja ujanja ni sehemu yake. Ile ishu ya kuongeza spread na kulazimisha watu watrade na jpmarkets ili wawe IB hyo ndo sehemu ya ujanja ujanja kwenye biashara ila ili la kusema kuwa call za Cre za loss zilikuwa za makusudi ili wakagawane pesa na broker traders wanapopoteza hela hilo sidhani kama ni kweli (Siwezi kuapa ila intuition yangu hainitumi hvyo).

Ishu hapa ni kwamba Cre ni mweupe na ndo maana baada ya kuona maji yamefika shingoni anaanza kutaka kuwashawishi watu kuwa broker ndo anawa B book ila kimsingi tatizo ni Cre...Hzo allegations za B Booking amezileta tu ila kujinasua kwenye lawama ila tatizo ni yeye na weupe wake.
 
Frankly speaking kama ulisoma vitabu na ukatrade hata kwa demo na bado unaona forex ni kama sport betting basi hakika hukuelewa wakati unasoma
 
Pole sana kiongozi take time jifunze mwenyewe taratibu utaweza kutrade very successful Tafuta kitabu kinaitwa intelligence investor I think nikizuri kuliko maelekezo ya hao wapigaji
 
Frankly speaking kama ulisoma vitabu na ukatrade hata kwa demo na bado unaona forex ni kama sport betting basi hakika hukuelewa wakati unasoma
Subir uzi utakuja.... "kilicho jificha nyuma ya FOREX" .. kila kitu ntaweka hapa... narudia tena usitegemee retailer kama wewe FOREX itakutoa never never........
 
Frankly speaking kama ulisoma vitabu na ukatrade hata kwa demo na bado unaona forex ni kama sport betting basi hakika hukuelewa wakati unasoma


Forex ni kama sport betting????....huyu le professeri vipii...hv kwenye spot betting unaweza tumia stop loss....hv kwenye sport betting unaweza take partial profit???yaani kwa mfano labda umebet match kati ya ManU Vs Mancity kuwa ManU watashinda na akishida labda utapata 100,000 ikafika half time ManU akawa kashampiga Mancity 1:0...hv unaweza kwenda kwa muhindi ukamwambia kuwa akupe 50,000 yako kuwa hutaki kuendelea mpaka mwisho wa match???

Kwenye forex unaweza take partial profit yaani kama lengo lako labda kwenye hyo trade ulikuwa unataka utengeneze pips 50 zinaweza fika pips 20 na ukaona kama kuna kitu kinataka kwenda kinyume na wewe ukaamua kuchukua profit ya zile pips 20 na kukaa pembeni. Sasa hapa sijui mtu analinganishaje forex na sport betting.
 
Sema chief unakosea one thing kumtetea Ontario.. na kumponda cre while wote wapo kwenye boat moja ya kuwapiga PESA watanzania masikin wenye kutegemea mlo mmoja kuishi.. imagine nasikia kuna mtu aliweka kiiinua mgongo chake kwa call za cre na kimekwenda wengine waliuza mpk viwanja, mashamba wapate mtaji.. vyote wahuni.. matapel hawa wamebebaa
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] uwiii nimecheka aisee poleni kwa kupigwa hakuna utajiri wa hivyo, mjifunze siku nyingine.
Labda tu niwaambie kitu. Huyo jamaa kaharibu brand name yake kwa kujifanya IB but kafungua sana watu. kwa sasa watu wanatrade forex like no other, na watu wamejiunga mafunzo ya online kutoka south africa, USA, etc. Wanazidi kuingia kila siku, and amini usiamini miaka 2, 3 ijayo college dropout zitakuwa nyingi na zitakuwa zinaongezeka.
Unasema hakuna utajiri wa hivyo, kwa fikra zako upo sahihi, lakini kwangu mimi kama watu walioanza December sasa wameanza kutengeneza atleast dollar 300 kwa siku consistently things are not bad.
 


Sijamtetea mkuu wangu ila nina taarifa za ndani kuwa Ontario waliwakiana sana na Cre kuhusu call zake zinazofanya watu wapoteze hela....ila nimesema siwezi kumwapia Ontario kuwa si sehemu ya watu kupoteza hela (yeye ndo anajua na Mungu wake na kama alileta hii kitu ili akawatapeli watu basi itamrudi big time maana kweli watu wamepoteza hela walizozipata kwa jasho sana sana sana na hilo haliwezi kwenda hv hv). Na kimsingi hzo allegations za jpmarkerts kuwa B book client wake sidhani kama zina ukweli maana endapo client watagundua kuwa broker anawa B book watamkimbia huyo broker na ndo utakuwa mwisho wake maana broker faida yake ipo kwenye spread, Swap na commission kama anacharge maana kuna broker wengine hawacharge commission.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…