Nimesoma uzi kwa utulivu kabisa na baadhi ya comments za wadau.. naomba nikazie tena kwenye hoja ya mleta Uzi kuwa FOREX SIO UTAPELI ILA BAADHI YA WATU NDO WANAFANYA FOREX IONEKANE NI UTAPELI.
Kimsingi mimi nafanya forex na nilipata training pale pale kwa
ONTARIO ila kabla ya training nilishasoma vitabu kibao na hakuna kitu ambacho nilikisikia kwa Rea ambacho kilikuwa kigeni kwangu.
Naomba nimuongelee ontario kidogo..kwa kifupi tu mtu unayejua kusoma mtu ukikutana na ontario kwa mara ya kwanza tu huna hata haja ya mpaka ukae naye uongee nayo utajua tu kuwa ni mtu mwenye dharau. Dharau za ontario kwa mtazamo wangu zinaweza kuchangiwa na vitu kadhaa,,
- kwanza kabisa kabila lake ni watu wa kujisikia sana (nina mfano wa professor mmoja hv pale chuo kikuu hata chai ya ofisi alikuwa hanywi anakuja na chai yake. na ni mtu wa kujisikia kweli kweli yaani yeye ndo yeye hakuna mwingine)
- background yake na mafanikio yake kwenye umri mdogo,,,kama mnavojua ontario alishakiri hapa si mara moja wala mbili kuwa katokea kwenye familia maskini kabisa na kapambana sana kufika hapo alipo. Sasa basi kama wengi tujuavyo ukiwa umetokea kwenye familia maskini halafu ukaja kuzishika tena kwenye umri mdogo basi tutakukoma kama we ni limbukeni wa hela. Kwa hyo kinachomsumbua ontario ni background yake na ana ulimbukeni wa hela kiasi kwamba anaona wasio nazo kama mabwege fulani hivi.
- Ontario amejitahidi kujua mambo mengi sana akiwa bado mdogo kwa jinsi hyo anawaona wale ambao hawajui kama wanaijaza tu dunia bure. Najua amefanya bidiii sana kuyajua ayajuayo ila kisiwe kigezo cha kuwaona wasiojua kuwa hawafai.
Nirudi kwa TMT na biashara ya forex...Kwa kifupi
ONTARIO hakujipanga kuanzisha TMT...kimuonekano alijitahidi sana ila je wale aliowalete kutoa training na mentorship ni watu sahihi??? Nikianza na Rea sikuon tatizo lake maana alitahidi sana kumwaga material kadri ajuavyo yeye na kwa kikubwa alitoa basics za forex ilibaki tu mtu mwenyewe kujiongeza kwa kusoma vitabu na kufanya backtesting kwenye demo ila awe nondo zaidi.
Nije kwa Mentor Cre...Mungu wangu yule jamaa ni bure kabisa...yaani kwa kifupi nilianza kumwekea walakini week ya pili tu baada ya kumaliza training na kuanza kutrade live. Kwa kifupi Cre ni mchanga sana kwenye forex yaani jicho lake kwenye charts ni changa mno na kimsingi hajaiva kuwa mentor bado anatakiwa kuwa chini ya mentor na sio yeye kuwa mentor maana bado ni mchanga sana sana sana kwenye kuanalyze charts. Kuna baadhi ya jamaa zangu niliwaleza mwanzo kabisa kuwa Cre bado hajaiva ila wakaona kama najifanya najua sana ila kwa sasa wamekubaliana na mm kuwa kuna vitu niliona kwa Cre ambavyo walikuwa hawajaona. Kwa kifupi Cre sio mentor na asipokubaliana na hali na kukubali kuwa chini ya mentor ili apate ujuzi atawaumiza wengi.
Kuna ishu fulani ilijitokezaga mwezi wa 12 mwaka jana kuwa Cre alikuwa anaiba analysis za BFG wa south na kushare ana Mentees wake ila ile ishu Cre alikana na kusema alishajotoa kwenye group la BFG ila nashawishika 10000000000% kuwa Cre alikuwa anaiba analysis za BFG kwani baada tu ya kusema ameshajitoa kwenye group la BFG ndo alianza kumake call za ajabu ajabu (yaani loss tupu).
Ishu ya Cre kusema kuwa JPmarkets walikuwa wanawa B Book clients wake huo ni uongo wa kiwango cha lami maana mm mara ya mwisho kutrade call za Cre sikuwa na Jpmarkets ila nilipata loss kubwa tu kwa kuitika call yake. Sasa endpo call yake ilikuwa sahihi kwa vile mm nilikuwa na broker mwingine nilitakiwa kupata faidi na wale waliokuwa na JPmarkets ndo wangepata loss maana jpmarkets wanatrade against client wake kama alivosema Cre. Kwa kifupi Cre ni mweupe jamani......Khaaaaaaa....mpaka nakereka.
Nina mengi ya kuandika kuhusu huyu bwana Cre ila ngoja tu mengine niache maana huyu jamaa alishanikera sana sana maana loss nyingi nilizopata nilikuwa nawasiliana naye na kumweleza kabisa kuwa call aliyomake sio ila anakuwa mbishi. Na mm kwa kutojiamini inabidi nikubaliane naye halafu baadae inakuwa maumivu tu.
Ushauri kwa
ONTARIO
- Mkuu najua sana wewe ni mpambanaji sana sana ila kama alivyosema mleta mada tamaa imekuponza sana sana...sitaki kwenda ndani zaidi maana mleta mada ameshasema mengi...Ila ontario acha tamaa mdogo wangu.
- Umejishushia sana heshima yako ambayo umeijenga kwa muda sana kwa kwanza kuweka tamaa mbele ila kibaya zaidi watu ulioshirikiana nao kwenye kuleta forex tanzania sio watu sahihi maana ungeleta watu sahihi hata huu ujanja ujanja tuliogundua wala tusingegundua endapo mentor angekuwa sahihi na watu wanaona faida kwa kutrade forex. Sisemi kuwa hakuna loss kwenye forex trading ila hizi loss za Cre zimezidi mkuu wangu. Kwa kifupi jamaa ni mweupe sana sana sana.
- Kama una mpango wa kuendelea kutoa training ya forex trading na mentorship..Nakushauri achana na Cre tafuta mentors wengine...South kuna mentro kibao ambao wanaweza kurudisha hesima yako kwa mwezi mmoja tu. Watanzania sisi ni watu wa kusahau mapema ukituletea mentor mzuri tukapiga hela mwezi mmoja tu mbona haya yote tuliyopitia tunayasahau faster tu.
Namalizia kwa kuseme Ontario Cre sio professional trader na hatakaa awe. yule anatakiwa tu awe chini ya mentor baaasi na sio yeye kuwa mentor.