Hivi ndivyo tulivyotapeliwa na Ontario wa TMT kwenye Forex

Hivi ndivyo tulivyotapeliwa na Ontario wa TMT kwenye Forex

Kuna watu kibao humu JF walituasa kwamba Forex ni utapeli hilo kwanza napingana nalo kwa nguvu zote sababu sio kweli kwamba forex ni utapeli kabla sijafunguka mengine niwathibitishie nimejiridhisha bila hata lepe la mashaka kwamba Forex is real and its my future lifestyle na binafsi sijioni nikikoma kufanya Forex licha ya haya magumu ninayopitia bali mawazo yao ninayachukuliaga kama catalyst ya kutaka kuzidi kuijua hii biashara kwa mapana zaidi kujua weakness na strength zake na kujua potential scammer, wezi na matapeli wakoje maana wametawala hii biashara kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwa na money liquidity kubwa kuliko soko lolote duniani..more than 6 trillion USD is traded daily on the Global financial market..hiki ni kiasi kikubwa sana hivyo matapeli huwa wanazengea zengea kwenye magap Kama haya yenye mkwanja mrefu..my economic cake pie is in Forex that's why I wont quit it easily.

But changamoto kubwa ya Forex ni hawa brokers na trainers..ninaposema trainers nazungumzia mtu kama Ontario hawa waliochungulia fursa mapema na kuintroduce kwa watu nchini kwa kigezo cha kuitoa elimu kwa bei sawa na bure tusijue wana agenda yao ya siri na Wasauzi ya kutaka kuwaliza watanzania wenzao.

Ontario ni mtunzi mzuri wa story na ana kipawa cha kusimulia na kushawishi kwa ufasha na ni mtu mwenye uelewa mpana wa mambo but anakosa kitu muhimu sana katika maisha uwezo wa kusocialize na watu in harmony..he is not a leader he is a boss na ukiangalia there is a thin line between a leader and a Boss..Ontario ana dharau, kiburi, na kejeli mbaya sana bila kujalisha umri wa anaeongea nae. Hana attentive listening ukiongea nae anakuangalia kama Choo na hajali lolote najua wengi waliokutana nae watakiri huu ukweli mchungu kwake ukiona mtu ana urafiki na Ontario ujue huyo mtu analazimika kujishusha sana kwa huyu dogo ili waende along. Huwa nashangaa ni rafiki sana na Bold. Pole sana Bold..I know what you going through.

Wahenga humu walituhasa kwamba ukiitwa kwenye fursa tafakari mara mbili yaweza kuwa wewe ndio fursa.anyways tulipoitwa kwenye fursa mwanzoni mambo yalienda vizuri na humu tulikuwa tunavurumusha screenshot za profit tu kwa maelekezo ya Ontario ili tuwakoge haters hadi haters wakafyata but kadri siku zilivyoenda mambo yakawa kimya ikawa ni loss daily tu watu wamechukua viinua mgongo vyote vikafyekwa sokoni. Hakyamungu!

Saga lilianza around mwezi wa kumi baada ya Ontario kula njama ya siri na broker awe anampa pips 2 kwa kila kichwa na zikiwa zinatoka calls kibao kombo kwa siku na zote zilikuwa sio accurate hivyo na watu kutengenezewa mazingira ya kutrade more often inamaanisha wakitrade watu 1000 wakafungua position 7 kila mmoja na idadi ya spreads pips anazopewa kutoka kwa broker kwa mtu mmoja ni 2..kimahesabu anapata 1000×7×2= 14,000 pips hizi ni dola kibao kwa siku ..wandugu wanojua mahesabu zaidi wanajua ni madola kiasi gani jamaa kavuta, hili suala alituficha but aliwahi kusema "Bob Marley you can fool some people for sometime but you can't fool all the people all the time"... Tukashtuka..tukamuuliza..akakubali ila akakiri alituficha na hayo mamilion yanayopatikana ni kwa ajili ya kuendeshea ofisi ya TMT co Ltd iliyoko pale Jangid plaza.. Watoto wa maskini tukakubali tu kwa shingo upande ila tukawa tumeghafilishwa na kusikitishwa sana na hizi njama zao..hili likapita na tukajilazimisha kukimeza maana ukipenda boga upende na ua lake.

Tamaa ni mbaya sana..licha ya kuchukua mamilion kutokana na hizo pips hawakuridhika..bado tena walikuwa wanachukua pesa kibao kwa siri kwa ajili ya IB link kwa affiliate program waliotuunga nayo siku tunamaliza mafunzo kutoka kwa broker kwa sisi tukipata loss sokoni wao wanapata chochote maana broker wao ni market marker. Hakyamungu! People are heartless.

Kama ilivyo asili ya watu wenye tamaa mbaya wakivurugana basi wao hukimbilia kutafuta sympathy ya Wateja..juzi wakavurugana broker na TMT kama ilivyo tabia ya wezi na matapeli kugeukana.. Majuzi wenyewe wanakuja na habari kwamba yule Broker ni market Maker na mwizi..kweli? Wakati wewe mentor umeishi South afrika na umekuwa Trader kwa miaka kibao bado hujui status ya broker unae trade nae? Na inakuwaje mrecomend broker mwenye walakini na competency na efficiency yake? Broker nae anajitetea kwa kutuma texts kwa Wateja privately akimtuhumu huyo mentor kuwa ni batili na mbabaishaji na kuwasihi watu wamuignore!? Blalifuli!

Tangu mwanzo mchakato uligubikwa na walakini mkubwa uliokuwa unaendelea..kwanza kumlazimisha mtu afungue real account baada ya siku tano tu za kumaliza mafunzo na aweke laki tano kuanza kutrade ilikuwa ni ishara ya wizi wa wazi sema tulikuwa na trust na maneno sukari ya Ontario, thus we were blind and fear of missing out easy Money.. Hatukujua!

Kutoa calls zaidi ya 7 kwa siku ni ishara mbaya ya kuwafanya clients waovetrade then wao wapige hela. Wizi huu.

Kuwaambia watu waongeze position ilhali wako in deep red ilikuwa ishara ya wizi, kuwataka watu waburn account zao wao wanufaike.

Kudiscourage matumizi ya stop loss ilhali ndio silaha ya kukinga mtaji wako kwenye Forex ilikuwa ishara ya wizi.

Watu wapoteze zaidi ili mpate zaidi maana kila ijumaa ilikuwa tunapunwa hela yote ya wiki nzima.

Mungu sio Sholo Mwamba, Yule broker market maker aliekuwa anatupiga sisi kwa tamaa kapitiliza kawafanyia mtimanyongo hadi kampuni ya TMT kaipuna zaidi ya nusu billion mapema mwezi wa kwanza. Imagine kampuni hii Changa ya huyu dogo imewazaje kupata nusu billion kwa muda mfupi hivi? Ni mikwanja aliyotuibia sisi misukule wake. But in life! "easy come..easy go"..ukikipata kiwepesi..kitaondoka kiwepesi pia. Nusu billion gone in a single month. Kweli JP Market broker ni hayawani!

Nitoe Rai kwa Ontario...sio kwamba namchukia hapana Bali naamini biashara inayohusisha watu moja kwa moja haiwezi kutokana na tabia yake mbaya ya asili..biashara na dharau, kebehi, utapeli na matusi havichangamani milele. Ni vyema akaendela na kilimo apate mil 19 zake kwa siku. Ameharibu kitu muhimu sana katika maisha yake ya biashara "Brand" and trust ya watu wengi aliowavuta kwa maandishi matamu humu JF..Trust ya watu pekee ni mtaji mkubwa kuliko hata mtaji wa fedha.

Namshukuru kwa kutuletea fursa hii adhimu lakini isiwe sababu ya kutuibia, kututapeli na kutunyanyasa economically and emotionally.

Rai kwa traders waliopigwa za uso na ndugu yao.."if you want to be strong learn how to fight alone" kwa kuwekeza Kwenye skills and self learning tunaweza kuwa self consistency profitable traders..let's ignore TMT they are scammer and predators and I don't recommend anyone to trust them.

Oooooopsiiii! Finally misukule wa Ontario tuko huru but tuko nyang'anyang'a kiuchumi. But it feels good kuwa huru.

Forex sio utapeli, matapeli ni mawakala wake.

Ni bora walimkavu...kuliko walimwengu!

Freedom!.
Sikuwahi kuwa na Imani na huyu mtu.
 
Ila mliopitia TMT na nyinyi ni wajinga wa kiwango cha 5G! Wewe unatrade na JP Markets lakini ukitaka kudeposit au kuwithdraw unapitia TMT what the f**ck! Halafu tangia lini uchaguliwe brocker? Tangia lini uwe trained kwa siku tano then unaambiwa uweke 200$ na wewe unakubali?

Poleni sana
We trusted our brother then he sold us out.

Trust.
 
Watu tumeandika sana kuhusu TMT na ONTARIO miezi mingi sana nyuma huko ila still watu wanaibiwa tu na mtu huyo huyo.
Nyie mnaoliwa sasahivi ni kwa kujitakia na ONTARIO endelea tu kuwala kwasababu hawawezi kutrade pasipo nyie.
Sasa TMT Na ONTARIO sasa sio wa kulaumiwa ila wakujilaumu ni hawa walioziba masikio na kusema "Watu wanachuki binafsi na ONTARIO" na wengine wakasema "FOREX DAR ndio wanasambaza habari za chuki kumharibia mshindani wao ,ONTARIO".
ONTARIO endelea tu kuwala wote wanaoendelea kufanya FOREX na nyinyi.

Watu waliandika sana mkaanza kuwaharibia thread zao kwa kukanunsha kila kilichoandikwa mda ule.Hakuna kipya hapo alichokindika Mleta mada ambacho toka mwezi wa 10 mpaka jan hakikuandikwa humu na vyote vilikanushwa na watea wake kindakindaki.

Watu wameona NANDI kaenda FOREX kwa ONTARIO akapiga picha na ONTARIO akaipost humu watu wakaanza kusema mbona NANDI kaenda bhana,hawa wengine ni chuki twendeni(Great thinkers wenzetu wakavutwa na NANDI hahahah).

ONTARIO kama utasoma hii comment ujue tu mimi sina kesi wala tatizo na wewe hata kidogo maana tofauti yangu na wewe nilimalizia kwenye thread hii SHAHIDI: Majibu kwa Ontario kuhusu kuitwa tapeli wa Biashara ya Forex kupitia TMT (II)

Myahudi Jr II ni muelewa sana sikuhizi huwa hafuati upepo na hatokuja kukukandia mleta mada kama alivyokuwa akifanya kwenye thread hii SHAHIDI: Majibu kwa Ontario kuhusu kuitwa tapeli wa Biashara ya Forex kupitia TMT (II)
 
mkuu, mimi nafanya folex, na sijawahi kuwa na mentor na profit na make, na sijawahi pigwa lost. by now nipo na ma broker wa 3, forex.com, etoro.com na hawa templerfx.com... naishi mwanana tu, sijawahi hata ku attend training zaidi ya kujisomea mwenyewe

Nakuhakikishia Forex sio utapeli ukipata watu sahihi wa kukuguide..its the future. Mbaya upate watu wenye tamaa kama ya Ontario.

Umekwisha!
 
niko fresh sana kwenye demo ila sasa kwenye live huwa presha inapanda najikuta na lose. kuna siku kidogo nivunje lap top zaidi ya 1800 dollar zilipotea ghafla in 10hrs na account ikasoma 2.7 $
Una haja ya kupanick umekosa discipline and proper risk management inaonyesha.
Na huko too emotional.

Tafiti mapungufu yako learn more you will be good.

Been there, done that.
 
We trusted our brother then he sold us out.

Trust.
Halafu mkuu nimeona umesema kuwa eventually TmT wakawaambia kuwa JP Markets ni tapeli na JP Markets nae akasema TmT awe ignored kuwa naye ni Tapeli.... Kwahiyo sasa TmT anatumia brocker yupi???

Kuna siku nilieleza watu humu kuwa ipo siku itatokea conflict of interest kati ya JP Market na IB wake TmT watu wakawa wanareply kwa blue screenshots!!! Haya sasa watu wameunguza viinua mgongo[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Una haja ya kupanick umekosa discipline and proper risk management inaonyesha.
Na huko too emotional.

Tafiti mapungufu yako learn more you will be good.

Been there, done that.
umekosa discipline and proper risk management inaonyesha.
Na huko too
emotional.
emotional.
emotional.
emotional.
emotional.

TRUE MAANA kwenye demo sikosei ila LIVE.
mkuu wewe uko maeneo gani dar labda tunaweza shar idea one day
 
niko fresh sana kwenye demo ila sasa kwenye live huwa presha inapanda najikuta na lose. kuna siku kidogo nivunje lap top zaidi ya 1800 dollar zilipotea ghafla in 10hrs na account ikasoma 2.7 $
Tupe sababu zilizopelekea kuunguza account yako...


Forex ni knowledge, ila kuwa na knowledge si kigezo cha wewe kufanikiwa.. Soma sana psychology of trading
 
niko fresh sana kwenye demo ila sasa kwenye live huwa presha inapanda najikuta na lose. kuna siku kidogo nivunje lap top zaidi ya 1800 dollar zilipotea ghafla in 10hrs na account ikasoma 2.7 $
Mkuu I have noticed that forex is all about skills and experience not capital

Binafsi nilishapoteza almost 300 usd lakn namshkuru Mungu noe nimeanza kuona mwanga

Yesterday night I deposited 6 usd lets see nitafika wapi next week
Screenshot_2018-04-06-08-31-37.png
 
umekosa discipline and proper risk management inaonyesha.
Na huko too
emotional.
emotional.
emotional.
emotional.
emotional.

TRUE MAANA kwenye demo sikosei ila LIVE.
mkuu wewe uko maeneo gani dar labda tunaweza shar idea one day
Unajua robot wanaweza kupata faida sana Kwenye Forex maana hawana emotional na adui mkubwa wa Forex ni emotional pekee.

Jaribu kutafuta best ways to handle emotions then you will be fine. Huu mtihani Mimi nilishaupita..emotions nilishazinyofoa zamani.

Kwa sasa siko Dar mkuu.
 
Exactly na kwa sasa Mimi siko kama nilivyo nimejifunzia na kumaster hiki kitu.

Na na ninaamini its the good things i have ever came across with.
Exactly mkuu.

Hii kitu nitajifunza mbeleni Mungu akipenda kwa sasa nazidi kujifunza zaidi jinsi ilivyo uhalisia wake.

Ningekuwa na muda wa kutosha ningeshajitosa kwenye training ila sikuweza sababu ya muda.

Niwapongeze wote mliofanya training ya hi kitu hatimaye mkagundua kilichomo humo na kutupa mwanga na njia sahihi wengine tuliochelea lakini tuna ndoto ya kujifunza.

ONTARIO tumwambie ukweli bila kumung'unya maneno katika mazuri yake na mabaya yake.

Daima ukweli unatuweka huru!!
 
hawa templerfx, nao wana changa moto yao. mie hawa nawatumia kwa ajiri ya matumizi madogo madogo maana hawa eleweki vizuri.

sehemu ya investment nimefanya etoro na forex

Mkuu Humble African kuna hawa templer Fx wanasema wana fanya trade za training kwa dola moja!! Yaani inakuwa kama demo acc ila ni real! Mi nataka hiyo ili niwe tu kama nacheza game huku naji brush!
 
Back
Top Bottom