Salaam wadau,
Tuendelee EPISODE 10C
Niliacha wiki ikate kisha nimtafute Recho kwa namna nyingine ingawa mara moja moja nilikua najaribu kupiga na majibu yalikua ni yaleyale 'blocked'. Hio haikuishia hapo tu nilipigwa tofali mpaka WhatsApp. Rasmi sioni tena status za Recho, meseji zipo 'single tick' na status zangu hazioni tena.
Baada ya wiki kukata niliona sina sababu tena ya kulazimisha mapenzi. Nilighaili kumtafuta tena Recho na kukubali maisha mapya. Hii haimaanishi sikuwa na mbinu mbadala, lah hasha. Kwa akili zangu nilikuwa na namna kibao za kumpata tena hewani lakini niliona haina maana kwani akishajua ni mimi haitabadilisha chochote.
Siku moja nikiwa nimepost status yangu WhatsApp ambayo sasa ni kila mtu anaona, miongoni mwa walio 'view' ni pamoja na Recho. Sikuamini hii kitu, ikabidi nimpigie. Simu kweli ikapokelewa, Mimi "Hello", akaitika " yes Z... mambo". Mimi " Dah! Siamini kama ni wewe umepokea simu yangu". Recho kwa sauti ya kawaida kabisa asiyo na shaka " Ni Mimi...kwani nimekuuliza we nani...najua naongea na Z". Mimi " Aisee, ok upo free tuongee". Recho we ongea tu nakusililiza".
Majibu ya Recho pamoja na 'tone' aliyokua akitumia ilinishangaza kidogo. Kwanini?. Kwasababu ni muda kidogo umepita zaidi ya mwezi mwezi na nusu toka ani 'block', ajabu ni alizungumza kama vile tunaongea kila siku.
Swali langu kwa Recho, " umeamua tuachane bila taarifa?". Recho " kwanini... mbona simu yako nimepokea!!". Mimi " nimeshangaa umeview status...ok kwanini ulinibock na ukapotea mazima". Recho "Nisikilize Z, Hapa katikati nimepitia mambo mambo... hivi tunavyoongea mume wangu kahamishwa kituo na sasa tupo tupo mkoa X".
Nikamdaka " Hivi kwa ukaribu tuliokuwa nao mbona hilo halizuii mawasiliano". Baada ya hilo swali kimya kidogo kikapita kisha, Recho " nisikilize Z, mume wangu alijua kuwa ninatoka nje na ndio kipindi hicho anapata uhamisho". Akaendelea " mambo mengi yalifata baada ya hapo mpaka tunaamia hapa ndio maana nikaamua nikuweke kando ili kurejesha amani ya ndoa yangu".
Mimi " Ni sawa Recho una hoja ila kwanini usingeniambia nijue kinachoendelea badala yake unaniblock". Recho "niliona ndio njia pekee ya kukaa mbali na wewe ili ni 'concentrate' na familia yangu".
Nikashusha pumzi. Kwa yale majibu yake Recho niliona kabisa kwake thamani yangu haipo tena, huyu ameshaamua lake. Nilitaka kufupisha mjadala nikate simu lakini Recho alikataa huku akiniregezea sauti. Ile niliyoizoea mwizi mimi.
Recho " Z nisikilize, ukiachilia mbali sasa nipo mkoa mwingine lakini ninajoina mbinafsi sana... sasa hivi unakazi, inatakiwa upate mwanamke mpambane mjenge maisha. Nikiendelea kukushikilia hutakuwa na familia". Hapa Recho aliongea kitu kikapenya flani hivi japo siku onesha kukubali Ile hoja
Mimi "Ooh! sasa ninakuelewa... kumbe tayari umeniacha ". Recho " hapana Z usichukulie hasira. Hujui nimemtumia nguvu kiasi gani kukubali nikuache uendelee na maisha yako. Hata Ile siku umepiga simu niliona nikublock tu maana nikiruhusu kukuwaza naumia".
Mimi "Recho ninayo mengi ya kusema juu ya jinsi nimeteseka na nateseka kwajili yako lakini haina maana tena kukwambia". Nikaendelea "Kumbe ulijiandaa kuniacha, poa". Palepale nikabadili mada kwani niliona nikama napata hasira na hisia za unyonge tena wa mapenzi.
Hatukuongea sana hata baada ya kubadili mada nikakata simu. Mpenzi msomaji, kwa sauti Ile ya mwanzo Recho alionekana ukurasa wa mapenzi na Z alishaufunga kilichobaki ilikua ni kunipa taarifa tu.
Mpaka wakati huo 'contact name' ya Recho katika simu yangu ilikua ni 'Amore' nikimaanisha mpenzi baada ya kunitoa ujinga kichwani nilibadili chap na kumsave kwa jina lake la NIDA.
Taarifa rasmi ya kuachwa maana kule sio kuachana haikuniumiza kwa level hio kwani nilisha iandaa saikolojia yangu toka awali. Sikuwahi kufuta ujumbe hata mmoja kutoka kwa Recho tangu nimeflash siku ya kwanza niliyoomba namba mpaka hio siku napewa rasmi taarifa.
Nilifuta Ile chat, kuhusu kufuta namba niliona haina maana kwani mbali na mapenzi huenda kuna siku atanifaa kwa ushauri wa kimaisha.
Recho yupo na familia yake mpaka leo. Z nipo na familia yangu mpaka leo. Hatuna mawasiliano sana lakini mara chache sana tunawasiliana na kushauri pale panauhitaji. Sina baya naye kabisa.
Katika simulizi hii nilijaribu kuongea na kila kundi katika jamii kwa kutoa vipande vya ushauri ndani ya kisa. Vijana na wanawake nili
wapendelea zaidi lakini kwa heshima na upendo nitatoa bonus Episode kufungua code fulani kwa wanaume walio ndani na hata Nje ya Ndoa.
Nimewaona kina Recho kadhaa kwenye comments na Z kama wawili lakini huu Uzi utawafaa wote. Nashukuru sana, Ahsanteni.