Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutajirika Kwa Kuanza Na Shilingi Elfu Moja

Moja ya sababu kubwa ambayo watu wengi husema kwamba inawazuia kufanya biashara ni mtaji. Mimi huwa nakataa sana sababu hii kwa sababu haiwezekani leo huna mtaji, mwaka kesho huna mtaji na hata miaka mitano ijayo huna mtaji. Nasema mtaji ni kigezo tu ambacho watu wengi hutumia kuficha sababu halisi ya kutokuingia kwenye biashara ambayo ni kutokujipanga na kutokuwa tayari.

Leo nakushirikisha siri moja ambayo itakuwezesha kufikia mafanikio makubwa sana japo utaanza kidogo. Kupitia siri hii unaweza kuanza na tsh elfu moja na baadae ukapata mtaji ambao utakuwezesha kufanya biashara kubwa. Pia tutaangalia kama ukianza na kiasi kikubwa kidogo itakavyokuwa bora zaidi.

ANGALIZO; Mambo utakayoyasoma hapa yatabadili kabisa maisha yako kama ukiyatumia. Ila kama utayasoma na kupita utaendelea kuwa na maisha magumu huku ukilalamika bila ya msaada wowote. Hivyo chukua hatua, huu ndio ukombozi wako.
Siri kubwa nitakayoizungumzia hapa ni kuweka akiba kidogo kidogo kila siku na kwa muda mrefu ili kuweza kuondoka kwenye tatizo la fedha uliloko nalo sasa. Na akiba hii hitaiweka benki ambako utawafaidisha sana na hela yako kuliwa na mfumuko wa bei, bali utaiweka kwenye mfuko wa dhamana ambao una uhakika wa kukua kwa asilimia sio chini ya kumi kwa mwaka. Mfano wa mfuko wa dhamana ni Umoja Fund wa UTT(Unit Trust of Tanzania) maarufu kama mfuko wa umoja au vipande vya umoja.

Kupitia mfuko huu unanunua vipande ambavyo vinakua kwa thamani kadiri muda unavyokwenda. Kwa mwaka vinakua sio chini ya asilimia kumi na mara nyingi inakuwa zaidi ya hapo. Hivyo hii ni njia nzuri sana ya wewe kukuza mtaji wako hata kama unaanzia sifuri.

Sasa tuone maajabu ya kuweka fedha kwa muda mrefu.

1. Kama utaanza kuweka tsh elfu moja kwa siku.

Naamini kama unasoma hapa huwezi kukosa tsh elfu moja kila siku. Hata uwe ni mmachinga, mama ntilie, au mpiga debe unaweza kupata tsh elfu moja kila siku. Usiidharau elfu moja hiyo maana ni njia yako ya kuelekea kwenye utajiri.

Kama kila siku utaweka tsh elfu moja, kwa mwezi itakuwa tsh elfu 30, kwa mwaka itakuwa tsh 360,000/=. Kama utaweka fedha hii kwenye mfuko unaokua kwa asilimia 10 kwa mwaka, kwa miaka mitano itakuwa tsh 2,997,403.20 hii ni sawa na tsh milioni tatu. Hiki ni kiasi ambacho huenda hujawahi kukipata kutoka kwenye vyanzo vyako mwenyewe ndani ya miaka mitano iliyopita.

Kama utaweka elfu moja hiyo kila siku kwa miaka kumi itakuwa tsh 7,244,967.43, milioni saba ni fedha ambayo huenda hujawahi kuota kuishika.

Kama bado ni kijana na ukaiweka fedha hii kwa miaka 20 itakuwa tsh 25,102,799.78(milioni 25) na ukiiweka kwa miaka 30 itakuwa tsh 71,421,417.80(milioni 71). Yaani kama wewe una miaka 35 au chini ya hapo, kama utaanza kuweka tsh elfu moja kila siku na ukaiweka fedha hii kwenye mfuko wa umoja utakapokuwa na miaka 60 utakuwa na tsh milioni sabini.

2. Kama utaanza na tsh elfu hamsini kwa mwezi.

Kama unafanya kazi ila una mshahara kidogo sana bado unaweza kujikusanya na kupata mtaji wa kutosha kukuondoa hapo ulipo. Kwa mfano kama mshahara wako uko kati ya laki mbili mpaka laki tano, kwa njia yoyote ile unaweza kujikaza na ukaweka pembeni tsh elfu 50 kila mwezi. Kama fedha hii utaiweka kwenye mfuko wa umoja, kwa miaka mitano itakuwa tsh 4,995,672.00(milioni 5), miaka kumi tsh 12,074,945.71, miaka 20 tsh 41,837,999.64 na miaka 30 tsh 119,035,696.34. Milioni tano kwa miaka mitano, 12 kwa miaka kumi, 41 kwa miaka 20 na 119 kwa miaka 30 ni fedha ambazo unaweza kuanzia nazo na ukafanya mabadiliko makubwa kwenye maisha yako.
3. Kama utaanza na laki moja kwa mwezi.
Kama unafanya kazi na mshahara wako ni kati ya laki tano na milioni moja kwa mwezi, unaweza kujibana na kuweka pembeni tsh laki moja kila mwezi. Kama utaiweka fedha hii kwenye mfuko wa umoja unaokua kwa asilimia 10 kwa mwaka mambo yatakuwa hivi; Miaka mitano tsh 9,991,344.00(milioni 10), miaka 10 tsh 24,149,891.43, miaka 20 tsh 83,675,999.27 na miaka 30 tsh 238,071,392.67. Milioni kumi kwa miaka 5, 24 kwa miaka 10, 83 kwa miaka 20 na hata milioni mia mbili na arobaini kwa miaka 30 ni fedha ambayo inaweza kubadili kabisa maisha yako kama utaanza kuweka tsh laki moja kila mwezi.

Hii ndio siri kubwa ninayokushirikisha leo na kama utaanza kuitumia leo, namaanisha leo hii utaona mabadiliko makubwa sana. Kama usipoitumia naomba unitafute tarehe 10/10/2019 (miaka mitano ijayo) na uniambie ni kipi kikubwa ulichofanya. Miaka mitano sio mingi kabisa rafiki yangu, kama unafikiri ni mingi kumbuka ni lini ulifanya uchaguzi mkuu na mwaka kesho ni uchaguzi mwingine.

Hoja yangu kubwa ni kwamba kama umeweza kuteseka kwenye kazi kwa miaka zaidi ya kumi na huoni mabadiliko makubwa kwa nini usijipe miaka kitano tu au kumi tu na uweke kiasi fulani cha akiba na baada ya hapo upate mtaji wa kuanzia?

Na katika miaka hii mitano au kumi ambayo mtaji wako unakua na unaendelea kuuweka, jifunze kuhusu biashara unayotaka kufanya. Jifunze kwa kujisomea, jifunze kwa kufanya utafiti na pia jifunze kwa kufanya kazi inayohusiana na biashara unayotaka kuja kufanya. Kama kila siku kwamiaka motano au kumi utajifunza kuhusiana na kitu unachotaka kufanya utaona fursa nyingi sana za wewe kutoka.

Uanzie wapi?
1. Leo hii nenda katika ofisi za UTT(kama upo dar nenda sukari house ghorofa ya kwanza, unaweza kutembelea tovuti yao www.utt-tz.com), jiandikishe kuwa mwanachama na watakupa utaratibu wa kuwa unatuma fedha zako hata kwa mpesa, hivyo huna haja ya kwenda benk au ofisini kila mara. Ukisema unasubiri jumatatu au mwisho wa mwezi tayari fursa hii imekupita, na miaka mitano ijayo utajuta sana.
2. Baada ya hapo weka tsh elfu moja pembeni kila siku, unaweza kuwa unaiweka kwenye mpesa halafu kila mwisho wa mwezi unatuma UTT tsh elfu 30. Pia unaweza kutuma zaidi ya hapo kulingana na mipango yako, hiyo 30 kwa mwezi ni kiwango cha chini ambacho kila mtu ambaye yuko makini na maisha yake anaweza kukiweka. Kama unataka kuweka kiwango tofauti na nilivyotumia hapo juu au kwa miaka tofauti bonyeza maandishi haya na utakuta fomula niliyotumia.
3. Wakati unaendelea kuweka fedha hizi na kuzikuza endelea kujifunza kuhusiana na biashara unayotaka kufanya. Unaweza kukaribia kwenye kundi letu la TANZANIA VORACIOUS READERS ambapo tunapanga kusoma vitabu 500 kwa miaka mitano(nitumie email kujua zaidi kuhusu kundi hilo, amakirita@gmail.com). Kama kwa miaka hii 5 utasoma vitabu 500 na wakati huo unaendelea kukuza mtaji, mambo yataanz akufunguka kabla hata hujafika miaka hiyo mitano.

Chukua hatua sasa hivi, kama unafikiri haiwezekani kaendelee kulalamika. Kama umechoka kulalamika huu ndio wakati wa kushika hatamu ya maisha yako.
Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kufikia mafanikio makubwa.
TUKO PAMOJA.
Endelea kutembelea AMKA MTANZANIA ili kujifunza zaidi.

Mimi nimewekeza kwenye mfuko mmoja wapo pale UTT unaitwa mfuko wa jikimu ambao napata gawio kila robo mwaka lakini gawio hilo silichukui linaendelea kununua vipande.

sasa ninachouliza hii UMOJA FUND na JIKIMU FUND ipi nzuri kuwekeza?

maana nilimsikia mfanyakazi mmoja wa UTT akielezea kuhusu UMOJA FUND unawanufaisha watu kwa 75% kwa fedha uliyo iwekeza tangu ianzishwe mpaka sasa. Lkn mimi nikiangalia fedha yangu niliyoiwekeza kwenye JIKIMU FUND haija panda thamani kiasi hicho.

Sasa je ni bora nianzishe nguvu nyingine kwenye umoja fund ndo unalipa au niendelee kuongeza kwenye Jikimu Fund?

ushauri wako mkuu.
 
Huna muda, okey nijiby swali hili.
Una masaa 24 kwa siku.
Unalala masaa 8
Unafanya kazi masaa 8 au tuweke 12 kwa sababu una hasira sana yankusaka hela.
Kula, kupumzika masaa 2
Unabaki na masaa 2 kwa siku, huwa unayafanyia nini?
Nasubiri jibu lako mkuu, nitakupa mpango mzuri sana ambao utabadili maisha yako.

Hayo masaa mbona ujaweka na kuwa kwenye foleni na kusubiria usafiri hasa kwa walio mijini.
 
Mimi nimewekeza kwenye mfuko mmoja wapo pale UTT unaitwa mfuko wa jikimu ambao napata gawio kila robo mwaka lakini gawio hilo silichukui linaendelea kununua vipande.

sasa ninachouliza hii UMOJA FUND na JIKIMU FUND ipi nzuri kuwekeza?

maana nilimsikia mfanyakazi mmoja wa UTT akielezea kuhusu UMOJA FUND unawanufaisha watu kwa 75% kwa fedha uliyo iwekeza tangu ianzishwe mpaka sasa. Lkn mimi nikiangalia fedha yangu niliyoiwekeza kwenye JIKIMU FUND haija panda thamani kiasi hicho.

Sasa je ni bora nianzishe nguvu nyingine kwenye umoja fund ndo unalipa au niendelee kuongeza kwenye Jikimu Fund?

ushauri wako mkuu.

Sina hakika sana kuhusu JIKIMU FUND ila najua hiyo unaweka kiasi fulani halafu unakuwa unapewa gawio.
UMOJA FUND hakuna gawio bali vipande ndio vinakua thamani na mara nyingine vinakua sana hivyo watu kufaidiaka sana.
Nenda kwenye ofisi zao wakuelezee, ila kwa upande wangu naona UMOJA is the best.
 
Hayo masaa mbona ujaweka na kuwa kwenye foleni na kusubiria usafiri hasa kwa walio mijini.

Sasa huo ndio wakati mzuri sana wa kusoma au kusikiliza vitabu vilivyosomwa(audio books).
Kama upo kwenye foleni ndani ya gari lako unaweka audio cd na kusikiliza.
Kama upo kwenye daladala hata kama umesimama unaweka earphone zako na kusikiliza audio books ambazo unakuwa umeweka kwenye simu yako.
Ukiwa umekaa kwenye foleni nyingine na kusubiri huduma, kama kwenye ofisi au bank unatoa kitabu chako iunaendelea kusoma.
Mimi muda mwingi ninaopata wa kusoma ni wa aina hii popote nilipo nakuwa na audio books na pia nakuwa na kitabu. Nikipata dakika kumi nasoma.
Kujua zaidi jinsi unavyoweza kuitumia foleni kwa manufaa fungua link hii http://www.amkamtanzania.com/2013/11/hivi-ndivyo-ninavyoifurahia-foleni.html
 
Kama unasema haiwezekani endelea kulalamikia maisha halafu baadae utatuambia kulalamika kwako kumekusaidia nini.
Miaka 20 au 30 nimetumia tu kuonesha ukuaji, target kubwa ni miaka mitano au kumi ambapo mabadiliko ya fedha yanakuwa sio makubwa sana na unaweza kuendelea kujifunza kuhusiana na biashara husika.
Milioni kumi ya mwaka 2009 na milioni kumi ya leo ina tofauti gani kwenye kuanzisha biashara? Ipo lakini sio kubwa sana kiasi cha kukufanya ushindwe kuanza biashara.
Tatizo kubwa la watanzania ni kutokujifunza na kuishi kwa mazoea tu na mwisowe kusema kitu hakiwezekani kwa sababu wewe hujawahi kufanya au hujawahi kumuona mtu anafanya.
Kwa miaka mitatu iliyopita nimesoma vitabu karibu mia tatu, sasa unasema kwa kujiamini kabisa kwamba miatano haviwezekani?
Nakuambia uweke elfu moja pembeni, elfu moja ambayo ungekunywa soda isiyo na maana kwenye maisha yako au kutumia hovyo tu na baada ya muda itakua na kufikia kiwango kikubwa kidogo, unasema pia haiwezekani?
Naweza kukuambia neno moja tu, KAFE MASIKINI.

Mkuu kuweka elfu moja siyo tatizo, ila kusoma vitabu mia 3, kwa miaka mitatu hii kwangu ni tatizo na ninakuona kama muongo labda kama vitabu vyenyewe vina page 10-20,

Je member anaweza kukopa kwa dhamana ya mchango wake anaojiwekea?au itabidi asubiri miaka 5 ndio aonje utamu wa mfuko?
 
Hakuna kisichowezekana, na tafadhali usiniite muongo. Kama hujawahi kuona ikifanyika haimaanishi haiwezi kufanyika.
Ndio unaweza kutumia vipande vyako kama dhamana ya kupata mkopo. Nenda ofisi zao watakupa maelezo mazuri.
Narudia tena watanzania wenzangu tuwe TUNAJIONGEZA, nilichoandika mimi sio sheria, kwa mfano hiyo miaka nimeandika kama ushauri wangu. Unaweza kuwekeza miaka miwili ukaona umepata kiasi cha kutosha ukafanya mengine. Unaweza kuwekeza miezi sita, ukaona imekutosha ukafanya mengine, maamuzi ni yako. Mimi nilikuwa nakuonesha faida ya kuweka kwa muda mrefu.
 
Mkuu nimekuita muongo kwa sababu mimi ni msomaji mzuri sana wa vitabu na pia kulingana na kazi yangu ya masaa 8 kwa Siku, muda wa kukaa na familia, muda wa kujipumzisha akili na shughuli za kijamii nasema ni vigumu kusoma vitabu 2 ndani ya wiki na kufanya discussions hata ukiwa jobless na hata ukiwa na uwezo huo hiyo hali haiwezi kuwa consistent na utakuwa huwezi kupata chochote kutoka kwenue hivyo vitabu labda kama unasoma majarida.

Na hata kukumbuka vitabu ulivyosoma na ulichokipata kutoka kwenye hicho kitabu itakuwa ngumu sana. Ila kama umeweza kusoma vitabu 300 ndani ya miaka 3, inamaana ndani ya wiki umesoma vitabu 2 nakuita wewe nI EXCEPTIONAL
 
Ndio maana nasema kama wewe huwezi usiseme haiwezekani. Mimi nimeshasoma vitabu vingi sana na kwa muda mfupi sana.
Ukijipanga vizuri unapata masaa mawili kwa siku, na wikiend unaweza kupata hata masaa matatubau manne. Kwa hiyo minimum unaweza kupata masaa 16 kwa wiki, je vitabu viwili haviishi?
Anza hivi, wahi kuamka saa moja kabla ya muda wako wa kawaida wa kuamka na tumia muda huo kusoma(hii inamaanisha uwahi kulala pia). Tembea na kitabu popote ulipo, ukiwa kwenye foleni soma, ukiwa umasubiri mtu au kitu soma.
Acha kuangalia tamthilia au movie, ni kupoteza muda, acha kupoteza muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii. Na pia punguza muda unaokaa kupiga story zisizo na msaada kwako.
Fanya hivyo uone kama vitabu viwili havitaisha.
Tatizo letu watanzania tunataka mabadiliko yatokee bila ya sisi wenyewe kubadilika. Unahitaji kubadilika kwanza na kiubadili maisha yako ndio uweze kufanya mambo hayo.
 
Hapana miaka 30 ni mingi mno. Ungetuambia maswala ya kuweka akiba tu na kuwekeza kwenye mambo mengine kama ufugaji, ukulima na biashara ndogo ndogo..

hiki ndyo watanzania mnachotaka mnapenda sana kazi za kutoka jasho,na kuumia sana mkipewa option ya kutengeneza kipato kwa njia rahisi mnaona mnatapeliwa.....
 
Biashara matangazo.... Labda iwe kwa dola ila syo sh. Ya Tz.. Tuheshimiane. Hapo watakaonufaika ni UTT... wao wanawiri mimi niendelee kuwa maskin kusubiri miaka 60,
 
Moja ya sababu kubwa ambayo watu wengi husema kwamba inawazuia kufanya biashara ni mtaji. Mimi huwa nakataa sana sababu hii kwa sababu haiwezekani leo huna mtaji, mwaka kesho huna mtaji na hata miaka mitano ijayo huna mtaji. Nasema mtaji ni kigezo tu ambacho watu wengi hutumia kuficha sababu halisi ya kutokuingia kwenye biashara ambayo ni kutokujipanga na kutokuwa tayari.

Leo nakushirikisha siri moja ambayo itakuwezesha kufikia mafanikio makubwa sana japo utaanza kidogo. Kupitia siri hii unaweza kuanza na tsh elfu moja na baadae ukapata mtaji ambao utakuwezesha kufanya biashara kubwa. Pia tutaangalia kama ukianza na kiasi kikubwa kidogo itakavyokuwa bora zaidi.

ANGALIZO; Mambo utakayoyasoma hapa yatabadili kabisa maisha yako kama ukiyatumia. Ila kama utayasoma na kupita utaendelea kuwa na maisha magumu huku ukilalamika bila ya msaada wowote. Hivyo chukua hatua, huu ndio ukombozi wako.
Siri kubwa nitakayoizungumzia hapa ni kuweka akiba kidogo kidogo kila siku na kwa muda mrefu ili kuweza kuondoka kwenye tatizo la fedha uliloko nalo sasa. Na akiba hii hitaiweka benki ambako utawafaidisha sana na hela yako kuliwa na mfumuko wa bei, bali utaiweka kwenye mfuko wa dhamana ambao una uhakika wa kukua kwa asilimia sio chini ya kumi kwa mwaka. Mfano wa mfuko wa dhamana ni Umoja Fund wa UTT(Unit Trust of Tanzania) maarufu kama mfuko wa umoja au vipande vya umoja.

Kupitia mfuko huu unanunua vipande ambavyo vinakua kwa thamani kadiri muda unavyokwenda. Kwa mwaka vinakua sio chini ya asilimia kumi na mara nyingi inakuwa zaidi ya hapo. Hivyo hii ni njia nzuri sana ya wewe kukuza mtaji wako hata kama unaanzia sifuri.

Sasa tuone maajabu ya kuweka fedha kwa muda mrefu.

1. Kama utaanza kuweka tsh elfu moja kwa siku.

Naamini kama unasoma hapa huwezi kukosa tsh elfu moja kila siku. Hata uwe ni mmachinga, mama ntilie, au mpiga debe unaweza kupata tsh elfu moja kila siku. Usiidharau elfu moja hiyo maana ni njia yako ya kuelekea kwenye utajiri.

Kama kila siku utaweka tsh elfu moja, kwa mwezi itakuwa tsh elfu 30, kwa mwaka itakuwa tsh 360,000/=. Kama utaweka fedha hii kwenye mfuko unaokua kwa asilimia 10 kwa mwaka, kwa miaka mitano itakuwa tsh 2,997,403.20 hii ni sawa na tsh milioni tatu. Hiki ni kiasi ambacho huenda hujawahi kukipata kutoka kwenye vyanzo vyako mwenyewe ndani ya miaka mitano iliyopita.

Kama utaweka elfu moja hiyo kila siku kwa miaka kumi itakuwa tsh 7,244,967.43, milioni saba ni fedha ambayo huenda hujawahi kuota kuishika.

Kama bado ni kijana na ukaiweka fedha hii kwa miaka 20 itakuwa tsh 25,102,799.78(milioni 25) na ukiiweka kwa miaka 30 itakuwa tsh 71,421,417.80(milioni 71). Yaani kama wewe una miaka 35 au chini ya hapo, kama utaanza kuweka tsh elfu moja kila siku na ukaiweka fedha hii kwenye mfuko wa umoja utakapokuwa na miaka 60 utakuwa na tsh milioni sabini.

2. Kama utaanza na tsh elfu hamsini kwa mwezi.

Kama unafanya kazi ila una mshahara kidogo sana bado unaweza kujikusanya na kupata mtaji wa kutosha kukuondoa hapo ulipo. Kwa mfano kama mshahara wako uko kati ya laki mbili mpaka laki tano, kwa njia yoyote ile unaweza kujikaza na ukaweka pembeni tsh elfu 50 kila mwezi. Kama fedha hii utaiweka kwenye mfuko wa umoja, kwa miaka mitano itakuwa tsh 4,995,672.00(milioni 5), miaka kumi tsh 12,074,945.71, miaka 20 tsh 41,837,999.64 na miaka 30 tsh 119,035,696.34. Milioni tano kwa miaka mitano, 12 kwa miaka kumi, 41 kwa miaka 20 na 119 kwa miaka 30 ni fedha ambazo unaweza kuanzia nazo na ukafanya mabadiliko makubwa kwenye maisha yako.
3. Kama utaanza na laki moja kwa mwezi.
Kama unafanya kazi na mshahara wako ni kati ya laki tano na milioni moja kwa mwezi, unaweza kujibana na kuweka pembeni tsh laki moja kila mwezi. Kama utaiweka fedha hii kwenye mfuko wa umoja unaokua kwa asilimia 10 kwa mwaka mambo yatakuwa hivi; Miaka mitano tsh 9,991,344.00(milioni 10), miaka 10 tsh 24,149,891.43, miaka 20 tsh 83,675,999.27 na miaka 30 tsh 238,071,392.67. Milioni kumi kwa miaka 5, 24 kwa miaka 10, 83 kwa miaka 20 na hata milioni mia mbili na arobaini kwa miaka 30 ni fedha ambayo inaweza kubadili kabisa maisha yako kama utaanza kuweka tsh laki moja kila mwezi.

Hii ndio siri kubwa ninayokushirikisha leo na kama utaanza kuitumia leo, namaanisha leo hii utaona mabadiliko makubwa sana. Kama usipoitumia naomba unitafute tarehe 10/10/2019 (miaka mitano ijayo) na uniambie ni kipi kikubwa ulichofanya. Miaka mitano sio mingi kabisa rafiki yangu, kama unafikiri ni mingi kumbuka ni lini ulifanya uchaguzi mkuu na mwaka kesho ni uchaguzi mwingine.

Hoja yangu kubwa ni kwamba kama umeweza kuteseka kwenye kazi kwa miaka zaidi ya kumi na huoni mabadiliko makubwa kwa nini usijipe miaka kitano tu au kumi tu na uweke kiasi fulani cha akiba na baada ya hapo upate mtaji wa kuanzia?

Na katika miaka hii mitano au kumi ambayo mtaji wako unakua na unaendelea kuuweka, jifunze kuhusu biashara unayotaka kufanya. Jifunze kwa kujisomea, jifunze kwa kufanya utafiti na pia jifunze kwa kufanya kazi inayohusiana na biashara unayotaka kuja kufanya. Kama kila siku kwamiaka motano au kumi utajifunza kuhusiana na kitu unachotaka kufanya utaona fursa nyingi sana za wewe kutoka.

Uanzie wapi?
1. Leo hii nenda katika ofisi za UTT(kama upo dar nenda sukari house ghorofa ya kwanza, unaweza kutembelea tovuti yao www.utt-tz.com), jiandikishe kuwa mwanachama na watakupa utaratibu wa kuwa unatuma fedha zako hata kwa mpesa, hivyo huna haja ya kwenda benk au ofisini kila mara. Ukisema unasubiri jumatatu au mwisho wa mwezi tayari fursa hii imekupita, na miaka mitano ijayo utajuta sana.
2. Baada ya hapo weka tsh elfu moja pembeni kila siku, unaweza kuwa unaiweka kwenye mpesa halafu kila mwisho wa mwezi unatuma UTT tsh elfu 30. Pia unaweza kutuma zaidi ya hapo kulingana na mipango yako, hiyo 30 kwa mwezi ni kiwango cha chini ambacho kila mtu ambaye yuko makini na maisha yake anaweza kukiweka. Kama unataka kuweka kiwango tofauti na nilivyotumia hapo juu au kwa miaka tofauti bonyeza maandishi haya na utakuta fomula niliyotumia.
3. Wakati unaendelea kuweka fedha hizi na kuzikuza endelea kujifunza kuhusiana na biashara unayotaka kufanya. Unaweza kukaribia kwenye kundi letu la TANZANIA VORACIOUS READERS ambapo tunapanga kusoma vitabu 500 kwa miaka mitano(nitumie email kujua zaidi kuhusu kundi hilo, amakirita@gmail.com). Kama kwa miaka hii 5 utasoma vitabu 500 na wakati huo unaendelea kukuza mtaji, mambo yataanz akufunguka kabla hata hujafika miaka hiyo mitano.

Chukua hatua sasa hivi, kama unafikiri haiwezekani kaendelee kulalamika. Kama umechoka kulalamika huu ndio wakati wa kushika hatamu ya maisha yako.
Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kufikia mafanikio makubwa.
TUKO PAMOJA.
Endelea kutembelea AMKA MTANZANIA ili kujifunza zaidi.

Nimeanza kusoma, nilipofika hapo kwenye red nikaacha. Umejifunza wapi Math?
 
Haihitaji kujua hesabu, tumia fomula niliyoweka hapo kwenye link. Halafu kuna vingi vya kujifunza hapa zaidi ya hiyo hesabu moja.
 
........ .. kipato chako chenyewe ni 1000 kwa siku, then ukaiweke 1000 hiyo hiyo katika mfuko wa akiba .. pia kila siku utahitaji si chini ya 1500 kama gharama za usafiri kupeleka hiyo pesa kwenye huo mfuko, pia utahitaji zaidi ya masaa matatu hadi manne kwa siku ili kuifikisha hiyo 1000 panapohusika.. inamaana katika masaa 10 ambayo ulikuwa unaitafuta 1000 utabakiwa na masaa 6 tu ya kutafuta 2500.. teh tehh... okay hesabu rahisi katika miaka mitano utakuwa na mil 1,800,000 safi sana hapo panafurahisha na kuona mafanikio.. haya sasa twende katika garama za kuifikisha hiyo 1000 pale panapo husika ni sh 2,700,000.. maajabu ya musa hayo sasa unatumia 2,700,000 ili kutunza 1,800,000. huu ni uchizi aisee
 
Mkuu unaweza kuyapanga mawazo yako vizuri ili tuweze kukuelewa na kukusaidia inapobidi?
Maana nimejitahidi kukuelewa nimeshindwa.
Ila kidogo ninachoweza kukuambia kwa maelezo hayo no hivi; kama unapata hiyo elfu moja kwa siku utaendelea kupata hiyo mpaka lini? Na je unafikiri kuna maajabu gani yatatokea kukutoa hapo ulipo?
Hii ndio inatakiwa iwe changamoto ya wewe kukuza kipato chako na sio kutumia kama sababu ya kiuendelea kuwa makini.
Karibu sana.
 
nadhani hapo wazo liwe kuweka hiyo 1000 kwa ajili ya malengo ya baadae kwa familia... ila sio wewe kujikwamua kwa umasikini. nilichokuelewa hapo ni kwamba niweke akiba kwa miaka 60 wakati hata life span ya mtanzania haifiki miaka 50
 
Wazo zuri lakn watanzania wengi wanaishi chini ya dola moja yaani namaanisha pato langu ni 1500 hii natakiwa nitumie matumizi yangu yote unafikir mtu wa aina yangu atasave chochote
 
nadhani hapo wazo liwe kuweka hiyo 1000 kwa ajili ya malengo ya baadae kwa familia... ila sio wewe kujikwamua kwa umasikini. nilichokuelewa hapo ni kwamba niweke akiba kwa miaka 60 wakati hata life span ya mtanzania haifiki miaka 50

Nani kakuambia miaka 60! Nimeweka miaka mitano hapo ina maana hukuiona?
Ondoa mtizamo hasi ulionao mkuu, weka elfu moja kwa miaka mitano ijayo ufanye kitu cha kukukomboa.
Ukiendelea kutafuta sababu za kwa nini usiweke hiyo buku utazipata nyingi sana. Na hakuna mtu atakuja kukutoa hapo ulipo.
Chukua hatua sasa.
 
Hiyo buku kuiweka au kuizungusha upate faida lipi jema?
 
Mkuu unaweza kuisoma vizuri hii makala na kuielewa ndio uweke post? Maana hakuna sehemu niliyosema uweke buku akiba nimekuambia uiwekeze hiyo buku sehemu inayokua.
Halafu hebu niambie unawezaje kuizungusha buku ukapata faida?
 
Nduhu uliyeanzisha hii tread umeongea vitu vya kweli kabisa na nina kuunga mkono asilimia 100.

Tatizo la watanzania ni la muda mrefu sana, tangia utoto hatijapata elimu za muhimu kwa mfano kuhusu mambo ya pesa au kujisomea.

Mimi binafsi nimejifunza mambo mengi yaliyonibadilisha kutokana na kusoma, Bill Gates mwenyewe anasoma kitabu kimoja kila wiki, jiulize mpaka leo amesoma vitabu vingapi?

Naamini kabisa kuwa kipato chako kinaweza kulingana na mambo uliyojifunza kwenye maisha. Yaani kichwani una nini? Ndio maana yake hiyo. Wanaojua vitu vingi wanapata hela nyingi. Period.

Watanzania wengi wameshakubaliana na hali walizonazo, wana taka slope tu. Kujitaabisha wala!
 
Back
Top Bottom