This is very unrealistic.. My Arguments are;
1. Kusoma vitabu 100 ndani ya mwaka mmoja ni jambo lisilo na faida yeyote.. Ideas gani unazitafuta kenye vitabu 8 kila mwezi?? Je, ikifika December utakikumbuka ulichokisoma the first week of January?? Kwangu ni bora uchague vitabu 6 vizuri usome 1 taratibu kwa miezi miwili, hapo utapata muda zaidi wa kukichambua kitabu vizuri..
2. Kusikiliza audio books kwenye daladala zetu za kibongo hapohapo ukapata point ya kinachoongelewa ni kujidanganya.. Audio books zinahitaji concentration ya hali ya juu, ni sawa na mtu anayeenda na madaftari club akitegemea atasoma akaelewa..
3. Kusoma vitabu 500 na kuweka 1000 kila siku kwa miaka mitano is another unrealistic thing.. Let's say kila kitabu kina mawazo matatu mazuri, which means ubebe mawazo 1500 ili baada ya miaka mitano uanze kuyafanyia utekelezaji ni kujidanganya na kuchosha akili bure..
4. Hiyo hoja yako haina tofauti na kitu kinaitwa "pig bank", its obvious that ni ngumu kwa mtu mzima anayetegemewa kuweza kuyatekeleza hayo, kuna mambo ya muda (kuhusu vitabu 500) na matatizo mbalimbali, hivyo hii idea ni nzuri kuwafundisha watoto wetu, mfano kwa mwaka wa kwanza unakua unamwekea mia 5 kwenye kibubu then unampa task ya yeye kufanya hivyo kwa miaka kumi, ikiwa kila ikifika birthday yake mnakivunja na kuhesabu then unaenda kumwekea kwenye account yake. Hii itamjenga ajue saving na pia akiendelea hivyo mpaka anamaliza university atakua na mtaji mzuri tu (sasa hapo he/she can decide kujiajiri ama kuajiriwa).. Kwetu sie watu wazima ni ngumu
Pia, naona una malengo yako binafsi kwenye hii elimu unayoitoa, kwanini watu wakikataa hoja yao unaleta maneno ya kejeli na unajibu kwa ghadhabu?? Kwa maisha ya watanzania hiyo njia yako ni ngumu mno, na ambao wanaweza ndio kama huyo mkuu hapo juu aliyesema mtakua exceptional.. Kuna njia nyingi za kupata mitaji na kutajirika... Si Bahressa, Mengi wala Patrick Ngowi ametumia hizo njia zako lakini they are known all over (Forbes). So, MTU kukataa hoja yako haina maana atakufa maskini, futa hiyo kauli yako, si ya kistaarabu kutolewa na mtu kama wewe