Arien
JF-Expert Member
- Aug 29, 2017
- 11,245
- 11,767
Hivyo vitabu umevisoma?Huyu ndo alinifanya nikaelewa maana ya kuweka akiba na kuiwekeza..re-invest..yuko poa sana sn
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hivyo vitabu umevisoma?Huyu ndo alinifanya nikaelewa maana ya kuweka akiba na kuiwekeza..re-invest..yuko poa sana sn
Hii ndo akili ya kumsaidia mtu.Kwa maana nyingine haumshauri mtu kuhusu uwekezaji, mm kwa kuongezeka juu ya ushauri wako mzuri, hizo hela ulizopata kwa mwezi tafuta sehemu zifanye kazi nazo pia zikuingizie 1000 kila siku au hata 500 na sio kumshauri mtu akaiweke hela iwafaidishe hao Company. Huwezi kupata hela ukapeleka bank, ikafanye nini na kwanini kwanza, Eti unataka utajiri, utajiri ni uwekezaji na sio kuweka pesa kiasi hiko.
NB: ushauri wako wauchukue lakini wasikubali kupeleka hela wanayoipata kwenye taasisi hiyo au hata bank mimi siwashauri, hakuna tajiri au mtu atakaye pata utajiri kwa utaratibu huo, haya kwa mfano hiyo hela unayoiweka mda huo, baadae unafanyia nini kama sio kubweteka kama mwanzo tu. USHAURI WANGU WEKEZA USIWEKE HELA BANK, hapo utapata mala 100 ya hela hiyo
VUTA PICHA
Kama una mtaji ambao utakuingizia 1000 kila siku, kwa wastani itakuwa biashara ya mtaji wa 50,000, ambayo kwa mwezi unapata 30,000 baada ya miezi 2 ukiwa unaweka hiyo buku una 60,000 ambayo tayari imezidi mtaji uliozizalisha hizo 60,000, kwa hapo ukianzisha biashara nyingine kwa siku unaanza kuweka 2000 na sio 1000 kama mwanzo, na kwa mwezi unakuwa na 60,000 na yenyewe pia ukifanya hivo kwa mwezi ni 90,000. Ukiwa unafanya hivo ndio inaitwa kuwekeza, na sio kumpeleka taasisi wa nini kama sio kumtajilisha na uzembe wa mawazo #kumradhi
Ulisema miaka miwili ila ni miaka mitano Sasa elfu moja still inanunua pipi na inalipa nauli.Hivi unajua kitu kinaitwa "time value of money?" Hiyo TZS 1,000 yako ya sasa baada ya miaka 2 tu hata pipi huwezi kununua. Hivyo unaweza kuweka hizo 1,000 moja zako na baada ya miaka 30 zikawa na nguvu ya sawa na 50,000 ya sasa.
Hongera sana mkuu kwa kuchukua hatua kwenye andiko hili la karibu miaka 10 iliyopita na kuona manufaa yake.Makirita Amani nakuomba uandike uzi mwingine kurejerea uzi huu jumatatu nilijaza form ya kuuza vipande vyangu pesa yangu nimeshaingiziwa kwenye akaunti yangu vipande hivi nlianza kununua baada ya kusoma uzi huu 2014 jumatatu nakwenda kulipia kiwanja mlandizi na nadhani ntabakiwa na Kama milioni tatu hivi hapa napiga mahesabu nizungushie fensi au ninunue pikipiki kisha mapato yake niendelee kuwekeza wakati huo kiwanja pia kikipanda thamani.
Moderator JamiiForums au Makirita Amani unaweza kuuatach hii comment hapo juu kwenye uzi ulipokua ukishauri na watu wengi humu wakabeza.
Ahsante sana
Mkuu, baada ya kukupa maua yako hapo juu, nikuchane kidogo.jumatatu nilijaza form ya kuuza vipande vyangu pesa yangu nimeshaingiziwa kwenye akaunti yangu vipande hivi nlianza kununua baada ya kusoma uzi huu 2014 jumatatu nakwenda kulipia kiwanja mlandizi na nadhani ntabakiwa na Kama milioni tatu hivi hapa napiga mahesabu nizungushie fensi au ninunue pikipiki kisha mapato yake niendelee kuwekeza wakati huo kiwanja pia kikipanda thamani.
Mtaji ni nini ?Moja ya sababu kubwa ambayo watu wengi husema kwamba inawazuia kufanya biashara ni mtaji. Mimi huwa nakataa sana sababu hii kwa sababu haiwezekani leo huna mtaji, mwaka kesho huna mtaji na hata miaka mitano ijayo huna mtaji.
Upo kwenye huduma gani nyingine ningependa kufahamu zaidi Kama hutojali unipe mawasilianoHongera sana mkuu kwa kuchukua hatua kwenye andiko hili la karibu miaka 10 iliyopita na kuona manufaa yake.
Ni vile watu humu wamezoea kupinga kila kitu lakini ukweli hakuna daraja rahisi la uwekezaji hapa Tanzania kama UTT.
Siku hizi nimeacha kupiga kelele na kila mtu kwenye hili, lakini watu wote waliopo kwenye huduma zangu nyingine kuwekeza UTT ni sharti la lazima.
Na hakuna ambaye amewahi kufuata ushauri huo akajutia, zaidi ya kila mmoja kufurahia kwa manufaa makubwa anayoyapata.
Kwa mtu yeyote makini na anayetaka kujenga kesho yake ya kifedha bora, basi sina kingine cha kumshauri zaidi ya kumwambia soma huu uzi kama ulivyo na anza kuwekeza mara moja.
Kiwango weka chochote unachoweza, lakini kadiri unavyoweka kiwango kikubwa, ndivyo manufaa yanavyokuwa makubwa pia.
Tuwasiliane kwa namba 0752977170Upo kwenye huduma gani nyingine ningependa kufahamu zaidi Kama hutojali unipe mawasiliano
Basi tujiwekezee hata bank ili tuwe tunaziona kaka. Nimeona hili andiko leo ila ni kama naiona 2014 na harakati zangu. Hadi najisikia aibu.Isije ikawa kama pesa zetu za NSSF ambazo baadae unaanza kupangiwa uzitumiaje na wakupe kiasi gani