Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutajirika Kwa Kuanza Na Shilingi Elfu Moja

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutajirika Kwa Kuanza Na Shilingi Elfu Moja

Moja ya sababu kubwa ambayo watu wengi husema kwamba inawazuia kufanya biashara ni mtaji. Mimi huwa nakataa sana sababu hii kwa sababu haiwezekani leo huna mtaji, mwaka kesho huna mtaji na hata miaka mitano ijayo huna mtaji. Nasema mtaji ni kigezo tu ambacho watu wengi hutumia kuficha sababu halisi ya kutokuingia kwenye biashara ambayo ni kutokujipanga na kutokuwa tayari. Leo nakushirikisha siri moja ambayo itakuwezesha kufikia mafanikio makubwa sana japo utaanza kidogo. Kupitia siri hii unaweza kuanza na tsh elfu moja na baadae ukapata mtaji ambao utakuwezesha kufanya biashara kubwa. Pia tutaangalia kama ukianza na kiasi kikubwa kidogo itakavyokuwa bora zaidi. ANGALIZO; Mambo utakayoyasoma hapa yatabadili kabisa maisha yako kama ukiyatumia. Ila kama utayasoma na kupita utaendelea kuwa na maisha magumu huku ukilalamika bila ya msaada wowote. Hivyo chukua hatua, huu ndio ukombozi wako. Siri kubwa nitakayoizungumzia hapa ni kuweka akiba kidogo kidogo kila siku na kwa muda mrefu ili kuweza kuondoka kwenye tatizo la fedha uliloko nalo sasa. Na akiba hii hitaiweka benki ambako utawafaidisha sana na hela yako kuliwa na mfumuko wa bei, bali utaiweka kwenye mfuko wa dhamana ambao una uhakika wa kukua kwa asilimia sio chini ya kumi kwa mwaka. Mfano wa mfuko wa dhamana ni Umoja Fund wa UTT(Unit Trust of Tanzania) maarufu kama mfuko wa umoja au vipande vya umoja. Kupitia mfuko huu unanunua vipande ambavyo vinakua kwa thamani kadiri muda unavyokwenda. Kwa mwaka vinakua sio chini ya asilimia kumi na mara nyingi inakuwa zaidi ya hapo. Hivyo hii ni njia nzuri sana ya wewe kukuza mtaji wako hata kama unaanzia sifuri. Sasa tuone maajabu ya kuweka fedha kwa muda mrefu. 1. Kama utaanza kuweka tsh elfu moja kwa siku. Naamini kama unasoma hapa huwezi kukosa tsh elfu moja kila siku. Hata uwe ni mmachinga, mama ntilie, au mpiga debe unaweza kupata tsh elfu moja kila siku. Usiidharau elfu moja hiyo maana ni njia yako ya kuelekea kwenye utajiri. Kama kila siku utaweka tsh elfu moja, kwa mwezi itakuwa tsh elfu 30, kwa mwaka itakuwa tsh 360,000/=. Kama utaweka fedha hii kwenye mfuko unaokua kwa asilimia 10 kwa mwaka, kwa miaka mitano itakuwa tsh 2,997,403.20 hii ni sawa na tsh milioni tatu. Hiki ni kiasi ambacho huenda hujawahi kukipata kutoka kwenye vyanzo vyako mwenyewe ndani ya miaka mitano iliyopita. Kama utaweka elfu moja hiyo kila siku kwa miaka kumi itakuwa tsh 7,244,967.43, milioni saba ni fedha ambayo huenda hujawahi kuota kuishika. Kama bado ni kijana na ukaiweka fedha hii kwa miaka 20 itakuwa tsh 25,102,799.78(milioni 25) na ukiiweka kwa miaka 30 itakuwa tsh 71,421,417.80(milioni 71). Yaani kama wewe una miaka 35 au chini ya hapo, kama utaanza kuweka tsh elfu moja kila siku na ukaiweka fedha hii kwenye mfuko wa umoja utakapokuwa na miaka 60 utakuwa na tsh milioni sabini. 2. Kama utaanza na tsh elfu hamsini kwa mwezi. Kama unafanya kazi ila una mshahara kidogo sana bado unaweza kujikusanya na kupata mtaji wa kutosha kukuondoa hapo ulipo. Kwa mfano kama mshahara wako uko kati ya laki mbili mpaka laki tano, kwa njia yoyote ile unaweza kujikaza na ukaweka pembeni tsh elfu 50 kila mwezi. Kama fedha hii utaiweka kwenye mfuko wa umoja, kwa miaka mitano itakuwa tsh 4,995,672.00(milioni 5), miaka kumi tsh 12,074,945.71, miaka 20 tsh 41,837,999.64 na miaka 30 tsh 119,035,696.34. Milioni tano kwa miaka mitano, 12 kwa miaka kumi, 41 kwa miaka 20 na 119 kwa miaka 30 ni fedha ambazo unaweza kuanzia nazo na ukafanya mabadiliko makubwa kwenye maisha yako. 3. Kama utaanza na laki moja kwa mwezi. Kama unafanya kazi na mshahara wako ni kati ya laki tano na milioni moja kwa mwezi, unaweza kujibana na kuweka pembeni tsh laki moja kila mwezi. Kama utaiweka fedha hii kwenye mfuko wa umoja unaokua kwa asilimia 10 kwa mwaka mambo yatakuwa hivi; Miaka mitano tsh 9,991,344.00(milioni 10), miaka 10 tsh 24,149,891.43, miaka 20 tsh 83,675,999.27 na miaka 30 tsh 238,071,392.67. Milioni kumi kwa miaka 5, 24 kwa miaka 10, 83 kwa miaka 20 na hata milioni mia mbili na arobaini kwa miaka 30 ni fedha ambayo inaweza kubadili kabisa maisha yako kama utaanza kuweka tsh laki moja kila mwezi. Hii ndio siri kubwa ninayokushirikisha leo na kama utaanza kuitumia leo, namaanisha leo hii utaona mabadiliko makubwa sana. Kama usipoitumia naomba unitafute tarehe 10/10/2019 (miaka mitano ijayo) na uniambie ni kipi kikubwa ulichofanya. Miaka mitano sio mingi kabisa rafiki yangu, kama unafikiri ni mingi kumbuka ni lini ulifanya uchaguzi mkuu na mwaka kesho ni uchaguzi mwingine. Hoja yangu kubwa ni kwamba kama umeweza kuteseka kwenye kazi kwa miaka zaidi ya kumi na huoni mabadiliko makubwa kwa nini usijipe miaka kitano tu au kumi tu na uweke kiasi fulani cha akiba na baada ya hapo upate mtaji wa kuanzia? Na katika miaka hii mitano au kumi ambayo mtaji wako unakua na unaendelea kuuweka, jifunze kuhusu biashara unayotaka kufanya. Jifunze kwa kujisomea, jifunze kwa kufanya utafiti na pia jifunze kwa kufanya kazi inayohusiana na biashara unayotaka kuja kufanya. Kama kila siku kwamiaka motano au kumi utajifunza kuhusiana na kitu unachotaka kufanya utaona fursa nyingi sana za wewe kutoka. Uanzie wapi? 1. Leo hii nenda katika ofisi za UTT(kama upo dar nenda sukari house ghorofa ya kwanza, unaweza kutembelea tovuti yao www.utt-tz.com), jiandikishe kuwa mwanachama na watakupa utaratibu wa kuwa unatuma fedha zako hata kwa mpesa, hivyo huna haja ya kwenda benk au ofisini kila mara. Ukisema unasubiri jumatatu au mwisho wa mwezi tayari fursa hii imekupita, na miaka mitano ijayo utajuta sana. 2. Baada ya hapo weka tsh elfu moja pembeni kila siku, unaweza kuwa unaiweka kwenye mpesa halafu kila mwisho wa mwezi unatuma UTT tsh elfu 30. Pia unaweza kutuma zaidi ya hapo kulingana na mipango yako, hiyo 30 kwa mwezi ni kiwango cha chini ambacho kila mtu ambaye yuko makini na maisha yake anaweza kukiweka. Kama unataka kuweka kiwango tofauti na nilivyotumia hapo juu au kwa miaka tofauti bonyeza maandishi haya na utakuta fomula niliyotumia. 3. Wakati unaendelea kuweka fedha hizi na kuzikuza endelea kujifunza kuhusiana na biashara unayotaka kufanya. Unaweza kukaribia kwenye kundi letu la TANZANIA VORACIOUS READERS ambapo tunapanga kusoma vitabu 500 kwa miaka mitano(nitumie email kujua zaidi kuhusu kundi hilo, amakirita@gmail.com). Kama kwa miaka hii 5 utasoma vitabu 500 na wakati huo unaendelea kukuza mtaji, mambo yataanz akufunguka kabla hata hujafika miaka hiyo mitano. Chukua hatua sasa hivi, kama unafikiri haiwezekani kaendelee kulalamika. Kama umechoka kulalamika huu ndio wakati wa kushika hatamu ya maisha yako. Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kufikia mafanikio makubwa. TUKO PAMOJA. Endelea kutembelea AMKA MTANZANIA ili kujifunza zaidi.
Mimi nashukuru sana kwa hii hoja na nilikuwa natamani sana kupata uchambuzi wa hii UTT.nna maswali yafuatayo?1.Je nnapowekeza kwenye mfuko huo kama ni laki moja kwa mwezi,gawio langu mwisho wa mwezi laweza kuwa shs ngapi?2. Naweza pata ufafanuzi kuhusu tofauti kati ya Umoja Fund,Wekeza Maisha, Jikimu Fudn,Watoto Fund na Liquid Fund coz zote zipo chini ya UTT sasa mtu kama mm nnayeanza maisha najikita wapi kati ya hizi.
 
Watanzania hatuna jema... tuwezacho ni kunung'unika! Kwanini tusiwe realistic? Kwanini tusiyageuza maelezo ya mtoa mada in other way round? Hivi wale mama n'tilie tulionao huku uswahilini ni wangapi wanaweza kuwa na laki saba ya pamoja? Je, hawa hawana uwezo wa kuweka sh. 1000 kila siku na baada ya miaka miwili kuwa na hiyo laki 7 ambayo inaweza kum-boost? Wale watembeza karanga barabarani ni wangapi wanaweza kuwa na laki 7 ya pamoja? Je, nao hawana uwezo wa kuweka sh. 1000 kila siku kwa miaka miwili na kuwa na laki 7 inayoweza kuwa-boost? Naona wengi mnataka kusema the whole thing is shit kwa sababu tu ya kutaja miaka 30! Hivi hatujiulizi ile miaka 3-4 ya chuo inavyotupita tukiwa kama tumesimama? Je, hiyo sh. 1000 mara miaka 3 si milioni moja hiyo? Hivi yule jamaa mtembeza tai na soksi barabarani hawezi kuweka 1000 kwa miaka 3 ambayo itampa hiyo 1 m inayoweza kum-boost?

Kuna uncle wangu, nitamuita hapa... alianza na kuku wa mayai 200 tena kijijini... walipoanza kutaga, kwa siku alikuwa anapata minimum trey 5 @Tsh. 9000/-! Hivi mwanachuo anayepata mkopo hawezi kuweka 1000 kwa siku na baada ya miaka 3 anapomaliza akawa na kianzio cha kuku 100 akawa anapata trey 2.5 au kuku 200 akawa anapata trey 5? Why hiyo 30 years ionekane ndio big issue badala ya kufikiria kinamna nyingine?

Asante sana mkuu kwa kuelewa vizuri na kwa mfano mzuri ulioongeza.
Tatizo la watanzania wenzetu hawapendi kujifunza na kujaribu mambo mapya. Mtu yuko radhi atumikishwe kwenye ajira miaka kumi ijayo ila kumwambia ajiamdalie mpango wa kumkomboa wa miaka michache anakuona wewe kichaa.
Watu hao hao ndio kila siku wanalalamika.
 
Kwa wale wanaouliza maswali kuhusu UTT na mifuko yao mingine naomba ili mpate maelezo mazuri tembeleeni website yao au nendeni pale sukari house ghorofa ya kwanza ulizia tu utt na waambie unataka kupata taarifa za uwekezaji watakueleza vizuri sana.
Mimi sio mfanyakazi wa utt wala mtangazaji wao, bali ni mwekezaji hapo na nilianza kidogo kidogo ila sasa hivi kila nikichek statement kwa mwezi naona mambo yanakuwa mazuri sana.
Hivyo nawahamasisha watanzania wenzangu hata kama hiutaki kuweka kwenye hiyo utt anza na mpango huo kidogo wa kuweka buku pembeni na uweke ambapo huwezi kuitoa.
Nilipendekeza utt kwa sababu hela huwezi kuitoa haraka, unaamdika barua kisha unapewa ndani ya siku kumi hivyo zile njaa za kuchomoa kama kwenye atm au mpesa/tigo pesa hazitakuwepo.
Kwa hivyo watanzania wenzangu hata kama huo mfumo hapo juu huwezi tengeneza wakwako ila usiishi HAND TO MOUTH ni hatari sana kwa maisha yako.
Nawatakia kila la kheri,
TUKO PAMOJA.
 
Mimi nashukuru sana kwa hii hoja na nilikuwa natamani sana kupata uchambuzi wa hii UTT.nna maswali yafuatayo?1.Je nnapowekeza kwenye mfuko huo kama ni laki moja kwa mwezi,gawio langu mwisho wa mwezi laweza kuwa shs ngapi?2. Naweza pata ufafanuzi kuhusu tofauti kati ya Umoja Fund,Wekeza Maisha, Jikimu Fudn,Watoto Fund na Liquid Fund coz zote zipo chini ya UTT sasa mtu kama mm nnayeanza maisha najikita wapi kati ya hizi.

una wazo zuri.... lkn hii njia ya ku cout maelezo yote sio nzuri.....
 
mkuu Makirita Amani hii mada kama umeikopi ipo humu zaidi ya miaka sita
 
Last edited by a moderator:
Kama unasema haiwezekani endelea kulalamikia maisha halafu baadae utatuambia kulalamika kwako kumekusaidia nini.
Miaka 20 au 30 nimetumia tu kuonesha ukuaji, target kubwa ni miaka mitano au kumi ambapo mabadiliko ya fedha yanakuwa sio makubwa sana na unaweza kuendelea kujifunza kuhusiana na biashara husika.
Milioni kumi ya mwaka 2009 na milioni kumi ya leo ina tofauti gani kwenye kuanzisha biashara? Ipo lakini sio kubwa sana kiasi cha kukufanya ushindwe kuanza biashara.
Tatizo kubwa la watanzania ni kutokujifunza na kuishi kwa mazoea tu na mwisowe kusema kitu hakiwezekani kwa sababu wewe hujawahi kufanya au hujawahi kumuona mtu anafanya.
Kwa miaka mitatu iliyopita nimesoma vitabu karibu mia tatu, sasa unasema kwa kujiamini kabisa kwamba miatano haviwezekani?
Nakuambia uweke elfu moja pembeni, elfu moja ambayo ungekunywa soda isiyo na maana kwenye maisha yako au kutumia hovyo tu na baada ya muda itakua na kufikia kiwango kikubwa kidogo, unasema pia haiwezekani?
Naweza kukuambia neno moja tu, KAFE MASIKINI.

usikatishwe tamaa katika kuwasaidia watu, wenye kuhitaji Masada wako watakuwa wamenufaika na mawazo yako.
 
usikatishwe tamaa katika kuwasaidia watu, wenye kuhitaji Masada wako watakuwa wamenufaika na mawazo yako.

Asante mkuu,
Sijakata tamaa na wala siwezi kukatishwa tamaa na mtu yeyote yule. Hiki ni kitu ambacho nimechagua kufanya maisha yangu yote. Ila kuna watu wanahitaji majibu makali kidogo ili akili zao zifikiri vizuri.
TUKO PAMOJA.
 
Makirita amani big up sana. Umeongelea ukweli halisi wa sisi watanzania we ye kipato kidogo from hand to mouth, huu ndio uwekezaji unaotufaa. Alaf watu wanapinga sbb 1,000/= kwao ni unrealistic, mbona mnaweza kuwekeza zaidi ya 1,000/= nadhan mfikirie mnaweza kuwekeza kiasi gani na kwa muda gani kadri ya malengo yako tusitegemee kilichoandikwa humu kiwefatwe hivyo hivyo, kama idea ni nzur basi tuichukue na kuirekebisha kadri itakavyotufaa sio kupinga tu haitatujenga.
Hakuna kinachoshindikana kwa mtu mwenye nia na dhamila ya dhati
 
Makirita amani big up sana. Umeongelea ukweli halisi wa sisi watanzania we ye kipato kidogo from hand to mouth, huu ndio uwekezaji unaotufaa. Alaf watu wanapinga sbb 1,000/= kwao ni unrealistic, mbona mnaweza kuwekeza zaidi ya 1,000/= nadhan mfikirie mnaweza kuwekeza kiasi gani na kwa muda gani kadri ya malengo yako tusitegemee kilichoandikwa humu kiwefatwe hivyo hivyo, kama idea ni nzur basi tuichukue na kuirekebisha kadri itakavyotufaa sio kupinga tu haitatujenga.
Hakuna kinachoshindikana kwa mtu mwenye nia na dhamila ya dhati

Asante sana mkuu.
Kwa kweli mtu anatakiwa akisoma hapa aone ni jinsi gani anaweza kuiprove au kuifanya iweze kuaply katika hali yake.
 
Wazo zuri ila sio kwa kutafutia mtaji tu; ili wazo linafaa sana kwa kuwekeza pesa ya mtoto kama ukizaa mtoto tu ukamfungulia account yenye interest ya maana na ukawa unaweka huko kila siku / mwezi akikua nadhani hautasumbuka kuhusu fees za university au siku akiondoka kuanza maisha unampa kianzio. Kwa msaada hapa labda ungeorodhesha fixed accounts zenye best percentage interests sababu ninavyojua nyingi kwakweli interests zao zinasikitisha ukiweka na inflation yaani mwisho wa siku pesa utakayochukua dhamani inakuwa imeshuka sana. Anyway saving for the rainy day is way to go.... Ila kama kuna uwezekano wa kupata asset kama nyumba ukanunua na kupangisha its way better though not easier
 
sasa huu ni ushauri au upotoshaji.huu mfuko ni wa chama fulani kinataka kikusanye tena mradi wake wa casmpaign.....kumbuka yale ya NIKO NK
 
Wazo zuri ila sio kwa kutafutia mtaji tu; ili wazo linafaa sana kwa kuwekeza pesa ya mtoto kama ukizaa mtoto tu ukamfungulia account yenye interest ya maana na ukawa unaweka huko kila siku / mwezi akikua nadhani hautasumbuka kuhusu fees za university au siku akiondoka kuanza maisha unampa kianzio. Kwa msaada hapa labda ungeorodhesha fixed accounts zenye best percentage interests sababu ninavyojua nyingi kwakweli interests zao zinasikitisha ukiweka na inflation yaani mwisho wa siku pesa utakayochukua dhamani inakuwa imeshuka sana. Anyway saving for the rainy day is way to go.... Ila kama kuna uwezekano wa kupata asset kama nyumba ukanunua na kupangisha its way better though not easier

Ni kweli kabisa mkuu. Kusave kwa ajili ya watoto ni vizuri mno.
Ila kwa benk hakuna haja ya kujisumbua hasa kwa hela ndogo hizi riba kubwa watakayokupa ni 3% ndio maana nimependekeza mutual fund ya umoja ambayo ina record nzuri ya kukua kwa zaidi ya 10% kwa mwaka.
 
sasa huu ni ushauri au upotoshaji.huu mfuko ni wa chama fulani kinataka kikusanye tena mradi wake wa casmpaign.....kumbuka yale ya NIKO NK

Mkuu tumia akili zako, acha kutumia akili za kushikiwa. Mutual funds ni uwekezaji unaojulikana dunia nzima. Kufa kwa niko ni kitu cha kawaida katika uwekezaji hasa management inapokuwa mbovu.
Sasa wewe endelea kuchanganya siasa na uwekezaji mwishowe uje ufe masikini. Kama unafanya kazi na unakatwa mafao yanaenda wapi? Si kwenye mifuko ambayo inamilikiwa na hivyo vyama? Mbona hujaacha kazi kwa sababu chama kinaweza kuiba hela zako na kukuacha solemba?
Fikiria kwa makini hasa inapokuja maswala ya uwekezaji.
 
thread nzuri ila naomba ufafanuz ktk hili.
hivi hawa UTT sio kama NICOL maana nasikia NICOL imeyumba sana.
 
Ni kweli kabisa mkuu. Kusave kwa ajili ya watoto ni vizuri mno.
Ila kwa benk hakuna haja ya kujisumbua hasa kwa hela ndogo hizi riba kubwa watakayokupa ni 3% ndio maana nimependekeza mutual fund ya umoja ambayo ina record nzuri ya kukua kwa zaidi ya 10% kwa mwaka.

Hizi Mutual Funds pia ni muhimu kufanya due diligence, unaweza ukawa on paper unaona pesa zimeongezeka kumbe ni kina Madoff Ponzi Scheme, (although sisemi kwamba hawa nao ndio wale wale)
 
Kusoma vitabu 500 eti ili utajirike ni kujitafutia uchizi.Hawa matajiri tulionao wengi hawajasoma vitabu ata 20.Wengine hawajasoma kabisa.

Hiyo kuweka 1000 pia kwa miaka 30 ni ngumu haiwezekani hakuna mtanzania anaweza.

Hiyo ya vitabu 500 pia ni ngumu.unacomplicate maisha.

Ni vizuri mtu akasoma vitabu vichache vinavyoweza kumsaidia kulingana na fani yake au shuguli yake.

Pia kuweka Akiba ni muhimu lakin sio kwa njia ya Kusadikika yani elfu moja kwa miaka 30

Hii ni ngumu mzeee

Why do Mr. Makirita is not polite in his answers? Because the truth hurts and he is copying American philantro-scam from the web.:thumbdown:
 
Why do Mr. Makirita is not polite in his answers? Because the truth hurts and he is copying American philantro-scam from the web.:thumbdown:

I am very sory if you find my answers not polite. I am doing it purposely because i have been telling people in more polite ways but they come with very awkward arguments. I may choose to ignore them but it wont help them. So i go straight, and tell them they have serious problem.
If you find me to be a scammer, please can you tall me how am i going to benefit when you start to save 1000 per day? I have not forced you to invest in mutual fund, that is one of the options.
So please sir, use the white stuff between your ears.
Sorry if that is hard to you.
 
Back
Top Bottom