Hivi ndivyo Viwango vya Sauti vinavyokubalika na "NEMC"

Sidhani kama ni sahihi!
Viwanda 65dba?
Makazi 35dba?

Hiyo 58dba tu kuna watu mkikaa mita 3 apart hawasikii!

Lengo ni nini? Uchafuzi wa mazingira au kulinda watumiaji?
Kuruhusu watu kufanya yao bila kuingiliana na wenye starehe
 
Huu ni mradi kama miradi mingine.Vipimo gani havina uhalisia.Lengo ni kukusanya pesa sio kutunza mazingira.
 
Makanisani na misikitini kiwango cha sauti ni decibel ngapi?
 
Hapa kijijini bitaraguru hizo decibel nazipimaje?
Hapo ulipo kuna chanzo cha Kelele?
Kama kuna chanzo cha Kelele, nenda kwenye Playstore ya simu yako, kisha-download "Sound Meter App".

Baada ya kui-download, ifanyie installation, then ifungue kwa ajali ya kunasa mawimbi ya sauti kutoka kwenye chanzo cha Kelele. Kama umepata majibu.
Jaribu kulinganisha dBA ulizozipata na za NEMC? je, zipo chini ya kiwango ama juu ya kiwango. Kama zipo juu ya kiwango ripoti NEMC kwa kuwa muathirika wa Uchafuzi wa Kelele.​
 
Makanisani na misikitini kiwango cha sauti ni decibel ngapi?
Wameanza kwanza na kwenye Mabaa, majengo ya shule, viwanda na Makazi ya Watu.
Utapata taarifa kamili baada ya mkutano unaokuja kati ya NEMC VS VIONGOZI WA DINI.
 
Wameanza na Kwanza na kwenye Mabaa, majengo ya shule, viwanda na Makazi ya Watu.
Utapata taarifa kamili baada ya mkutano unaokuja kati ya NEMC VS VIONGOZI WA DINI.
Hizo ni mbinu za kutafuta pesa hawana lolote, wanataka watu wakienda club au bar wasisikilize music
 
You must be fool, yaan kelele za BAR unahitaji kuzipima? Bar iko Km 3 na bado unasikia kelele za music, je waliokaribu na hiyo Bar watakuwa kwenye hali gani?

Tuache uswahili wakati mwingine, huko Ulaya unaweza tembea usisikie hizo kelele mwaka mzima, ukitaka kelele zama indoor huko.
 
Naona faini ndo zimegeukiwa kuwa chanzo cha mapato baada ya tozo kupigiwa kelele.
 
Naona faini ndo zimegeukiwa kuwa chanzo cha mapato baada ya tozo kupigiwa kelele.​
Sio kweli Mkuu.
Huu ni utaratibu kama utaratibu mwingine, tatizo letu hatupendi Sheria tunataka kuishi kama wanyama pori.

Lazima uelewe Dunia ni uwanja wa fujo, bila sheria kila mtu angefanya anavyotaka ndio maana sheria ipo ilikuweka mizania sawa.​
 
Kama Earphones ina kiwango cha sauti ambacho mtu ukizidi kuongeza "volume sound" kwenye simu yako inakwambia "Loud sound can damage your inner ear."

Sijui wanaona ajabu gani kwa NEMC kutoa katazo la kelele kwenye Mabaa na kumbi za starehe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…