Hivi ndivyo wenye picha za ngono katika simu watakavyonaswa

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
25,030
Reaction score
61,298
KAMA hujaisikia mbiu, ni vyema ukutangaziwa wazi kwamba wale ambao bado tunahifadhi picha na video za ngono kwenye simu zetu za mkononi kinyume na amri ya Mkuu wa Mkoa Paul Makonda ya kututaka tuzifute TUMEKWISHA; Hakiyanani hakuna wa kupona kwa mujibu wa vyanzo vya ndani ya vyombo vya usalama na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ‘TCRA’.

Wasiojua mbinu za kiusalama za kuzuia uhalifu kwenye simu wamekuwa wakibishabisha kwamba: “Simu yangu ninayo mwenyewe, nimeifunga kwa namba za siri; hao TCRA wanawezaje kujua **** nina picha chafu na kunikamata?”

Kauli hii ni sawa na mbwa anavyoweza kujipeleka kwa chatu huku akipepesa mkia akidhani yu salama kumbe anakwenda kumezwa, Uwazi limeambiwa teknolojia ya kisasa inaweza kumbaini mtu aliyetuma au kuhifadhi picha alizotumiwa kirahisi kabisa na kumtia mbaroni.

MSIKIE MTAALAMU KUTOKA TCRA

“Kufanya kazi ya kuwafuatilia wahifadhi picha za ngono kwa wingi wao inaweza kuwa ngumu, lakini haishindikani pale inapotakiwa wahusika kupatikana. “Watu wanatakiwa kujua, vitu vingi siku hizi vinahifadhiwa kwa mfumo kama vinasaba DNA kwamba kila kitu kina utambulisho wake ambao hauingiliani na mwingine.

“Mfano kwenye simu kuna namba ya utambulisho inaitwa IMEI, hii kila simu inayo ya kwake, hazifanani, kwa msingi huo tukitaka kumjua mtu anayetumia simu aina fulani tunaweza kuanzia kwenye kuangalia hiyo namba na kufuatilia mambo mengine kwa kufuata sheria.

“Kwa hiyo hata hizi picha unazoziona nazo zina namba ya utambulisho ambao haufanani na nyingine, wataalam wakiikagua wanaweza kujua ilipigwa lini, kutumia kifaa gani, ilikuwa saa ngapi na eneo gani?
“Ukipata taarifa hizi nilizokutajia ni rahisi kufuatilia nani mhusika na pengine kama kuna aliowatumia unamjua mmojammoja na kuwakamata inawezekana,” kilisema chanzo chetu kinachofanya kazi TCRA katika kitengo cha Tehama.

WATAKAMATWA WOTE?

Kwa mujibu wa chanzo hicho inaelezwa kuwa kufanya oparesheni ya kuzuia uhalifu si lazima watu wote wakamatwe lakini wakipatikana nguli wa mambo hayo na kushugulikiwa tatizo linaweza kumalizika. “Unajua pengine kutokana na wingi wa watu kuwa na picha za ina hiyo ndiyo maana wengi wanajifariji kuwa serikali haiwezi kuwakamata wote.

“Nilipita sehemu moja mitaa ya Kinondoni (jijini Dar) nikamsikia kijana mmoja anawaambia wenzake agizo la mkuu wa mkoa ni la kutishia watu kwa sababu haiwezekani kuwamata wote wenye picha hizo kwani wanaweza kujaza mahabusu. “Lakini kama nilivyosema, lengo si wote kukamatwa, lakini wakipatikana mia au hamsini wakachukuliwa hatua si itakuwa fundisho kwa wengine!” Chanzo kilifafanua.

SHERIA INASEMAJE?

Sheria inakataza mtu kuhifadhi picha chafu kwa sababu anaweza kusababisha zikachapishwa jambo litakalomtia hatiani kwa kufungwa miaka 10 au kulipa faini ya shilingi milioni thelathini.

Aidha ni kosa pia kumuonesha sha picha au video za ngono mtu ambaye si mke au mpenzi wako, jambo linalowapa mamlaka polisi kumtia mbaroni mtu yeyote anayehifadhi picha chafu na kumfikisha mahakamani.

POLISI WANENA

Kufuatia agizo la mkuu mkoa wa Dar lililozua gumzo la kuwataka watu wote wenye picha chafu kuzifuta kabla ya Novemba 5 mwaka huu, jeshi la polisi kwa upande wake nalo liko tayari kuanza kazi ya kuwasaka watuhumiwa.

Akizungumza na Uwazi afisa wa polisi kutoka kitengo cha upelelezi kanda maalumu ya Dar ambaye hakupenda kutaja jina lake alisema: “Kusaka wahalifu kuko kwa njia nyingi ikiwemo ya kushuku, sasa kama mtu anasema atakuwa na simu yake ameiweka password, polisi akimshuku si anamuita na kumwambia aifungue ili ikaguliwe.

“Ugumu uko wapi, ni wazi wengi watakamatwa, watahojiwa na wale watakaopatikana na kosa watapelekwa mahakamani. “Hata kama mimi si msemaji wa jeshi la polisi nilikuwa nawaomba wananchi na hasa watumiaji wa simu za mkononi kutii sheria bila kushurutishwa, haya mapicha ya ngono ya nini kwenye simu? Si wayafute?”

Kaimu Meneja Mawasiliano TCRA, Semu Mwakanjala alipotafutwa kwa lengo la kutolea ufafanuzi wa namna mamlaka hiyo itakavyoweza kuwanasa watuhumiwa wa kuhifadhi picha chafu hakuweza kupatikana kutokana na simu yake kuita bila kupokelewa. Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro alipotafutwa hakupatikana kuzungumzia agizo la mkuu wa mkoa wa Dar.

FARAGHA YA MAWASILIANO YATAJWA

Wakati mjadala wa kuwatia mbaroni watuhumiwa wa kuhifadhi picha chafu ukiendelea na hofu ya simu za watu kupekuliwa, baadhi ya watu wamekuwa na hofu kuwa huenda mambo haya yakaleta uvunjifu wa katiba ya nchi. Ibara ya 16 ya Katiba ya nchi kifungu 1 inasema; Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi

kwa naafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na unyumba wake, pia heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake binafsi. Hata hivyo katika kifungu kidogo cha pili cha ibara hiyo kinaweka mazingira ambayo faragha ya mtu inaweza kuingiliwa bila kuathiri kifungu cha kwanza.

“Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kwa mujibu wa ibara hii, Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa sheria kuhusu hali, namna na kiasi ambacho haki ya mtu ya faragha na ya usalama na nafsi yake, mali yake na maskani yake, yanaweza kuingiliwa bila ya kuathiri ibara hii.

MEZA YA MHARIRI

Kutokana na hali halisi ilivyo, meza ya mhariri inawashauri watumiaji wa simu za mkononi kuwa makini na matumizi mabaya ya teknolojia ya mawasiliano na badala yake kutumia mawasiliano kama njia ya kuboresha maendeleo na siyo kutumiana picha za ngono.
 
Kukosa kazi za kufanya wapuuzi tu.

Tanzania ina mambo mengi ya kufanya wanataka kupoteza muda na vitu vya kijinga, mtu anaangalia porn kwenye simu yake inaathiri mipango na maendeleo ya nchi?

Wamefeli suala la ving'amuzi wanaanza kujipa kazi za kishilawadu
 
mtoa hoja una uchoyo wa ukweli,hakuna technolojia rahisi hivyo iliyopo itakayosaidia hilo jambo,kuingia ndani ya simu ya mtu ni zoezi linalogharimu mno na halina uhakika kama linaweza fanikiwa;kumbuka kesi ya yule mwanariadha kilema pale SA ambapo lilikuwa ni jambo zito mno kujua kilichojili kwenye simu yake,na kama ni mfuatiliaji mzuri wa habari hivi karibuni kuna issue ya simu ya waziri mmoja kwenye serikali ya SA ambaye picha zake za uchi zimeenea kwenye social netsworks na hana uwezo wa kugundua zimevuja vipi na afterall hii ni personal issue utakiwa ni ujinga mno kwa serikali yangu kujiingiza kwenye issue kama hii,tunahitaji jeshi letu lifanye majukumu yake kama kulinda mipaka yetu ambayo inatumiwa na syndicates nyingi na hatari mno kama human trafficking na drugs etc etc.
 
Kukosa kazi za kufanya wapuuzi tu.

Tanzania ina mambo mengi ya kufanya wanataka kupoteza muda na vitu vya kijinga, mtu anaangalia porn kwenye simu yake inaathiri mipango na maendeleo ya nchi?

Wamefeli suala la ving'amuzi wanaanza kujipa kazi za kishilawadu
Mambo ya msingi yamewashinda,pesa ngumu,ajira kila siku zinapotea,kila kitu hakieleweki,huku kwenye kongamano LA uchumi "CCM" ma profesa wa mwendo kasi wanaimba kama kasuku kuhusu uzuri wa takwimu,huku waziri wa fedha,anaweka wazi hari ya uchumi ni mbovu,
Hivi kweli unajenga ghorofa,watoto wanakula mlo mmoja ugari na mlenda,wakiuliza,unawaambia vumilieni hili ghorofa,litawasaidia mkiwa wakubwa,!!what an ass hole!!,unajuaje kama watafikia umri huo??,wakifa kwa afya mbovu?
 
Mkuu umeandika andiko lefu sana lisilo na nadharia, Hii siyo rahisi kama unavyofikiria sababu kuwa na picha au kitu chochote kwenye simu yako si sawa na kuchati text kwa kutumia mtandao wa voda na txt zikabaki kwenye server zao. Tatilia kesi mbali mbali duniani kwenye technology kubwa ndo utajua nini namanisha.

Just tuwe tu wazalendo na kutambua kuwa ikitokea simu yako imepotea au kuibiwa na vile visimu vyetu vya techno havina privacy wala security mtu akazisambaza. Basi kesi itakuangukia wewe. So ni tahadhari tu ila sio huo uongo.

Pia kwa technology tuliyonayo Tanzania na uhaba wa wafanyakazi kwenye hizo tasisi wallah wakiamua kufuatilia means idara zote za makosa ya mtandao watakuwa busy na kazi iyo moja mwaka mzima ndo wawapate, kitu ambacho hakiwezekani sababu kuna kazi kibao na za maana still hawalazipatia ufumbuzi.
 
Write your reply...
hivi kulikuwa na haja gani kuwafukuza wakoloni!!
sasa si bora nyerere angetuacha tuendelee kutawaliwa na wazungu kuliko kutawaliwa na washamba flani kutoka kolo mi je..
 
Mambo ya msingi yamewashinda,pesa ngumu,ajira kila siku zinapotea,kila kitu hakieleweki,huku kwenye kongamano LA uchumi "CCM" ma profesa wa mwendo kasi wanaimba kama kasuku kuhusu uzuri wa takwimu,huku waziri wa fedha,anaweka wazi hari ya uchumi ni mbovu,
Hivi kweli unajenga ghorofa,watoto wanakula mlo mmoja ugari na mlenda,wakiuliza,unawaambia vumilieni hili ghorofa,litawasaidia mkiwa wakubwa,!!what an ass hole!!,unajuaje kama watafikia umri huo??,wakifa kwa afya mbovu?
Teh teh teh...mkuu umenivunja mmbavu kwa maswali yako mwisho[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] ,, je wakifa kwa afya mbovu?!!
 
Waanza kufungia website za ngono waone voda na mitandao mingine watakavyolalamika matumizi ya bundle yanapungua kwa 80%

Kwanza hio teknolojia policcm wetu failure wa std 7 na form 4 wanaijua kweli au ndio hadithi za abunwasi
 
Hivi mtu kujipiga picha mwenyewe na kuzihifadhi kwenye Simu yake isiyoonwa na mtu mwingine kuna athari gani? Yaani kosa vyote usikose akili!!
 
Write your reply...
hivi kulikuwa na haja gani kuwafukuza wakoloni!!
sasa si bora nyerere angetuacha tuendelee kutawaliwa na wazungu kuliko kutawaliwa na washamba flani kutoka kolo mi je..
Hata Mimi nimeanza kutamani ukoloni.
 
KAMA hujaisikia mbiu, ni vyema ukutangaziwa wazi kwamba wale ambao bado tunahifadhi picha na video za ngono kwenye simu zetu za mkononi kinyume na amri ya Mkuu wa Mkoa Paul Makonda ya kututaka tuzifute TUMEKWISHA; Hakiyanani hakuna wa kupona kwa mujibu wa vyanzo vya ndani ya vyombo vya usalama na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ‘TCRA’.

Wasiojua mbinu za kiusalama za kuzuia uhalifu kwenye simu wamekuwa wakibishabisha kwamba: “Simu yangu ninayo mwenyewe, nimeifunga kwa namba za siri; hao TCRA wanawezaje kujua **** nina picha chafu na kunikamata?”

Kauli hii ni sawa na mbwa anavyoweza kujipeleka kwa chatu huku akipepesa mkia akidhani yu salama kumbe anakwenda kumezwa, Uwazi limeambiwa teknolojia ya kisasa inaweza kumbaini mtu aliyetuma au kuhifadhi picha alizotumiwa kirahisi kabisa na kumtia mbaroni.

MSIKIE MTAALAMU KUTOKA TCRA

“Kufanya kazi ya kuwafuatilia wahifadhi picha za ngono kwa wingi wao inaweza kuwa ngumu, lakini haishindikani pale inapotakiwa wahusika kupatikana. “Watu wanatakiwa kujua, vitu vingi siku hizi vinahifadhiwa kwa mfumo kama vinasaba DNA kwamba kila kitu kina utambulisho wake ambao hauingiliani na mwingine.

“Mfano kwenye simu kuna namba ya utambulisho inaitwa IMEI, hii kila simu inayo ya kwake, hazifanani, kwa msingi huo tukitaka kumjua mtu anayetumia simu aina fulani tunaweza kuanzia kwenye kuangalia hiyo namba na kufuatilia mambo mengine kwa kufuata sheria.

“Kwa hiyo hata hizi picha unazoziona nazo zina namba ya utambulisho ambao haufanani na nyingine, wataalam wakiikagua wanaweza kujua ilipigwa lini, kutumia kifaa gani, ilikuwa saa ngapi na eneo gani?
“Ukipata taarifa hizi nilizokutajia ni rahisi kufuatilia nani mhusika na pengine kama kuna aliowatumia unamjua mmojammoja na kuwakamata inawezekana,” kilisema chanzo chetu kinachofanya kazi TCRA katika kitengo cha Tehama.

WATAKAMATWA WOTE?

Kwa mujibu wa chanzo hicho inaelezwa kuwa kufanya oparesheni ya kuzuia uhalifu si lazima watu wote wakamatwe lakini wakipatikana nguli wa mambo hayo na kushugulikiwa tatizo linaweza kumalizika. “Unajua pengine kutokana na wingi wa watu kuwa na picha za ina hiyo ndiyo maana wengi wanajifariji kuwa serikali haiwezi kuwakamata wote.

“Nilipita sehemu moja mitaa ya Kinondoni (jijini Dar) nikamsikia kijana mmoja anawaambia wenzake agizo la mkuu wa mkoa ni la kutishia watu kwa sababu haiwezekani kuwamata wote wenye picha hizo kwani wanaweza kujaza mahabusu. “Lakini kama nilivyosema, lengo si wote kukamatwa, lakini wakipatikana mia au hamsini wakachukuliwa hatua si itakuwa fundisho kwa wengine!” Chanzo kilifafanua.

SHERIA INASEMAJE?

Sheria inakataza mtu kuhifadhi picha chafu kwa sababu anaweza kusababisha zikachapishwa jambo litakalomtia hatiani kwa kufungwa miaka 10 au kulipa faini ya shilingi milioni thelathini.

Aidha ni kosa pia kumuonesha sha picha au video za ngono mtu ambaye si mke au mpenzi wako, jambo linalowapa mamlaka polisi kumtia mbaroni mtu yeyote anayehifadhi picha chafu na kumfikisha mahakamani.

POLISI WANENA

Kufuatia agizo la mkuu mkoa wa Dar lililozua gumzo la kuwataka watu wote wenye picha chafu kuzifuta kabla ya Novemba 5 mwaka huu, jeshi la polisi kwa upande wake nalo liko tayari kuanza kazi ya kuwasaka watuhumiwa.

Akizungumza na Uwazi afisa wa polisi kutoka kitengo cha upelelezi kanda maalumu ya Dar ambaye hakupenda kutaja jina lake alisema: “Kusaka wahalifu kuko kwa njia nyingi ikiwemo ya kushuku, sasa kama mtu anasema atakuwa na simu yake ameiweka password, polisi akimshuku si anamuita na kumwambia aifungue ili ikaguliwe.

“Ugumu uko wapi, ni wazi wengi watakamatwa, watahojiwa na wale watakaopatikana na kosa watapelekwa mahakamani. “Hata kama mimi si msemaji wa jeshi la polisi nilikuwa nawaomba wananchi na hasa watumiaji wa simu za mkononi kutii sheria bila kushurutishwa, haya mapicha ya ngono ya nini kwenye simu? Si wayafute?”

Kaimu Meneja Mawasiliano TCRA, Semu Mwakanjala alipotafutwa kwa lengo la kutolea ufafanuzi wa namna mamlaka hiyo itakavyoweza kuwanasa watuhumiwa wa kuhifadhi picha chafu hakuweza kupatikana kutokana na simu yake kuita bila kupokelewa. Naye Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro alipotafutwa hakupatikana kuzungumzia agizo la mkuu wa mkoa wa Dar.

FARAGHA YA MAWASILIANO YATAJWA

Wakati mjadala wa kuwatia mbaroni watuhumiwa wa kuhifadhi picha chafu ukiendelea na hofu ya simu za watu kupekuliwa, baadhi ya watu wamekuwa na hofu kuwa huenda mambo haya yakaleta uvunjifu wa katiba ya nchi. Ibara ya 16 ya Katiba ya nchi kifungu 1 inasema; Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi

kwa naafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na unyumba wake, pia heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake binafsi. Hata hivyo katika kifungu kidogo cha pili cha ibara hiyo kinaweka mazingira ambayo faragha ya mtu inaweza kuingiliwa bila kuathiri kifungu cha kwanza.

“Kwa madhumuni ya kuhifadhi haki ya mtu kwa mujibu wa ibara hii, Mamlaka ya Nchi itaweka utaratibu wa sheria kuhusu hali, namna na kiasi ambacho haki ya mtu ya faragha na ya usalama na nafsi yake, mali yake na maskani yake, yanaweza kuingiliwa bila ya kuathiri ibara hii.

MEZA YA MHARIRI

Kutokana na hali halisi ilivyo, meza ya mhariri inawashauri watumiaji wa simu za mkononi kuwa makini na matumizi mabaya ya teknolojia ya mawasiliano na badala yake kutumia mawasiliano kama njia ya kuboresha maendeleo na siyo kutumiana picha za ngono.
Swali la kujiuliza je ni muhimu kufanya haya? Kama ninayo kwenye simu simuoneshi mtu naangalia mwenyewe nkiwa peke yangu je kunifatilia ni muhimu kuliko kupeleka vitabu shuleni wanafunzi wasome, kuna sehemu nyingi tu hazina huduma za jamii, je kumfuatilia mtu anayeangalia video za ngono ni muhimu kuliko kuumiza vichwa vyao jinsi gani watahudumia jamii
 
Bora wangeendelea kukamata mashoga kwani hilo zoezi la kutafuta picha za ngono kwenye simu litanifanya niwadharau kama funza
 
Hivi mtu kujipiga picha mwenyewe na kuzihifadhi kwenye Simu yake isiyoonwa na mtu mwingine kuna athari gani? Yaani kosa vyote usikose akili!!
Kuna siku simu inaweza kupotea au kuharibika, sasa huko picha zikasambaa, ukweli kuacha picha za utupu Katika simu ni Bomu
 
Back
Top Bottom