Kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufuta uchaguzi na kutangaza upya marudio ya uchaguzi kwa kuwa Tofauti zilizoko ni kubwa sana, na nikatoa mfano wa Tarakimu za
Geita CCM 17,792 CDM 3,789 ( Iliyotangazwa na RO Geita CCM 30,960 CDM 22,031) Ni wazi kilichotokea hapa ni kuchakachua kwa lengo la kupunguza kabisa kura za Dr. Slaa, japo za JK nazo zimepunguzwa).
Jimbo la Hai CCM 35,910 CDM 18,513 (Iliyotangazwa Hai na RO CCM 20,120 CDM 26,724) Uchakachuaji uliofanyika hapa ni wa kumwongezea JK kwa zaidi ya kura 15,000 na kupunguza za Dr. Slaa kwa zaidi ya 8,000).
Nilitoa pia mfano wa Ubungo ambapo kwa mujibu wa CCM 68,727 CDM 65,450 (iliyotangazwa na RO CCM 70,472 CDM 72,252) hapa na uchakachuaji ulioafanyika ni wa kupunguza kura za Dr. Slaa kwa Takriban 8,000 na kupunguza za CCM kwa kama 2000 hivi)
Katika Jimbo la Bunda CCM 20,836 CDM 571 (Iliyotangazwa na RO CCM 20,836 CDM 18,445) Tarakimu za Bunda zimerekebishwa katika Taarifa ya mwisho ya NEC. Taarifa hii inaonyesha kuwa Dr. Slaa alipewa kura za Lipumba).
Jimbo la Karatu ni kichekesho zaidi kwani kwa mujibu wa Taarifa ya awali ya NEC iliyonukuliwa na Mwananchi CCM 24,364 CDM 41 (iliyotolewa na RO CCM 24,364 CDM 43,137) Taarifa ya mwisho ya NEC imerekebishwa kufanana na ya RO Karatu.