Siyo lazima NEC wasubiri matokeo ya miji midogo kutangaza matokeo. Kama population ni ndogo, na namba za watu waliopiga kura haziwezi kufikia zile ambazo tayari zimeshapigwa, NEC wanao uwezo kutangaza matokeo bila ya kusubiri hayo matokeo. Is all about Mathematics.
Superman, unafikiri hata kama Chadema ingeweza kutoa matokeo yote na ushahidi wote basi watu wangekubaliana kuwa ushindi wa CCM una mashaka? Tarehe 3 Novemba wakati Dr. Slaa ametoa wito kuwa kuna tofauti za kura na akatolea mfano wa jimbo moja tu la Geita isingetosha kuwafanya Tume wasitishe na kusikiliza? Leo hii yametolewa majimbo mengi zaidi na baadaye yatatolewa zaidi unafikiri wana CCM na mashabiki wao watakuja na kusema "tupitie kura zote ili Rais wetu asionekane kabebwa"? Really?
Hapa the only point is to make NEC better ready for 2015 "Thats why nashauri wacompile evidence zote na story A to Z na kitungwe kitabu kigawiwe bure Tanzania na Nje ya Tanzania Mwanakijiji with your journalistic background am sure you can compile a book kwa kuhihusisha chedema and with proper evidence ofcourse
Wabongo kwa kupangia kazi wenzetu tu hatujambo. Utafikiri Mwanakijiji nchi ndiyo yake sisi wengine ni watakia heri tusio raia ambao haturuhusiwi kushiriki.
Basi hivi hivi hata mabadiliko tutaachia watu fulani tu kutokana na "backgrounds" zao. Ndiyo maana mabadiliko yanakuwa magumu, kila mtu anamtegemea fulani. Vipi kama tungekuwa na wanavijiji kadhaa wanatokea kila mwezi ?
Mkuu unapoona ukweli wa aina yoyote ile unachakachuliwa lazima uuweke sawa. Uchakachuaji wa ukweli kuhusu kumlinganisha Dr. King na Dr. Slaa ilibidi usahihishwe kwanza kisha tuendelee na mjadala. Tukirudi kwenye mada kuu: Kosa moja goli moja - kosa lilifanyika siku ya kuhesabu kura ambapo watu walijikita kufuatilia na kulinda kura za Ubunge na kusahau za Urais japo walikumbushwa sana hadi humu jamvini! Kilichobaki sasa ni kutorudia kosa kwa kuanza kujenga mazingira ya kuziba mianya yote ya uchakachuaji kati ya sasa na 2015. Nawasilisha.
Duh! jamani hivi kweli Bongo tunatumia mfumo gani huu wa demokrasia?..Kama kuna vituo ambavyo hadi leo hesabu yake haijatolewa, inawezekana vipi NEC kumtangaza mshindi hali hawana hesabu kamili ya kura zote zilizopigwa?
No, your fighting different warKuna kitu kinaitwa Specialization Mkuu, Kila kitu kinahitaji expertisim, am sure when it comes with journalism na uandishi MKijiji ananiacha mbali and am not talking about the IQ and thinking capacity bali his journalistic contacts and all that kwake ni rahisi kupata hizo evidence kuliko mimi and likewise it is easy kwake kuonge na dr Slaa et al . kuliko mimi.... Amigo tusipigane am sure we are fighting the same war
To Mwanakijiji; so umekubali responsibility ya ku compile kitabu kuhusu huu wizi, myself tachangia gharama na kukisambaza bure mitaani
Nadhani message ya Wabunge na ya kwangu iko very clear isipokuwa kwa mtu anayetaka tu kuispin au kuibadilisha kwa sababu anayoitaka mwenyewe. Naomba kurejea mambo ya msingi kwa wale ambao kwa bahati mbaya yamewapita na wana nia ya kuelewa ili spinning hii isiwabughudhi.Mara baada ya uchaguzi, tarehe 3 November, 2010 Dr. Slaa alifanya Press Conference Makao Makuu ya Chadema kama Mgombea Urais ambaye hakuridhika na mchakato wa uchaguzi na Matokeo yaliyokuwa yakitolewa kupita Vituo vya TV na Jaji Lewis Makame, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.
Katika Press Conference hiyo Dr. Slaa alitaja dosari nzito katika mchakato wa uchaguzi na hasa katika hatua ya kujumlisha na kutangaza Taifa ambapo matokeo yaliyokuwa yakitangazwa na NEC yalitofautiana kwa kiwango kikubwa sana na yale yaliyotangazwa na Wasimamizi wa Uchaguzi (W) pale ambapo zoezi hilo lilifanyika. Nikatoa Mfano wa Geita.
.Pili, nilieleza kuwa Katika majimbo takriban 25 zoezi la majumlisho halikufanyika kama inavyotakiwa na sheria na hivyo matokeo kutangazwa na wasimamizi kwa utaratibu kinyume na sheria na kanuni za uchaguzi
Tatu, nilieleza kuwa katika maeneo mengine kama Kinondoni masanduku yapatayo 25 ambayo tunayo namba zake tunazo yalipatikana katika ghala la Shule ya Sekondari ya Biafra Jijini Dar-Es-Salaam ambayo hayajahesabiwa na matokeo yamekwisha kutolewa.
Nne, Siku ya tarehe 28 October, Tume ya Taifa ya uchaguzi ilialika Wataalam wa IT wa vyama, na kuwa mbele ya Wataalam hao mfumo wa computer uliokuwa unatumika uli "collapse" na Tume kuwajulisha Wataalam kuwa wataita LapTop zote kutoka nchi nzima zirejeshwe Dar kwa matengenezo ya program husika. Na kuwa wataitwa tena kujulishwa kama zimetengenezwa. Hawakuitwa tena.
Hivyo mfumo wa Computer uliotumika kukusanya matokeo na upeleka Taarifa NEC unatia mashaka makubwa. Hata hivyo, baadaye tulipokea Barua kutoka NEC ya tarehe 28/10 ambayo ililetwa kwa Dispatch Makao Makuu Chadema tarehe 5 November, ikisema " Watalaam walikuwa na kukagua mfumo wa IT unaotumika na Tume na waliridhika" . Ni dhahiri barua hii inatia mashaka kwanini barua ya tarehe 8/10 iletwe kwa dispatch na ifike siku takriban 8 baadaye? Hali hii inatia mashaka kuwa barua hii imekuwa backdated kwa Tume kuficha ukweli wa Scandal kubwa iliyotokea katika mfumo ambao uligharimiwa kwa fedha nyingi na UNDP.
Iwapo Tume inaweza kudanganya katika swala kama hili tutatukuwa na imani gani na Tume tena.
Kutokana na dosari hizo kubwa (pamoja na mambo hayo yaliyojitokeza baadaye) Dr. Slaa, kama Mgombea aliitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi ifanye mambo yafuatayo: Kusimamisha Zoezi la Kutangaza matokeo hadi uchunguzi kamili utakapokuwa umefanyika ili kuondoa hisia na tofauti zilizoanza kujitokeza. Ikumbukwe kuwa Tofauti hizi kimsingi ziligundulika na Wananchi wenyewe kutokana na Tarakimu alizosoma Jaji Makame kutofautiana na zile zilizotangazwa na Wasimamizi katika maeneo yao.
Matokeo yake wananchi waliingia mitaani kupinga hali hiyo. Hayo yalitokea Geita, Shinyanga, Mbozi Mashariki na kadhaa. Matokeo yake wananchi hao waliokuwa wanadai haki zao walipigwa mabomu na polisi. Njia ya Busara ilikuwa kuitaka Tume kusitisha zoezi hili ili lisilete athari zaidi, japo hawakufanya hivyo.
Chadema tulifanya jitihada za ziada kuwasihi wananchi wetu wasiingie mitaani kuepusha shari.
Kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufuta uchaguzi na kutangaza upya marudio ya uchaguzi kwa kuwa Tofauti zilizoko ni kubwa sana, na nikatoa mfano wa Tarakimu za
Geita CCM 17,792 CDM 3,789 ( Iliyotangazwa na RO Geita CCM 30,960 CDM 22,031) Ni wazi kilichotokea hapa ni kuchakachua kwa lengo la kupunguza kabisa kura za Dr. Slaa, japo za JK nazo zimepunguzwa).
Jimbo la Hai CCM 35,910 CDM 18,513 (Iliyotangazwa Hai na RO CCM 20,120 CDM 26,724) Uchakachuaji uliofanyika hapa ni wa kumwongezea JK kwa zaidi ya kura 15,000 na kupunguza za Dr. Slaa kwa zaidi ya 8,000).
Nilitoa pia mfano wa Ubungo ambapo kwa mujibu wa CCM 68,727 CDM 65,450 (iliyotangazwa na RO CCM 70,472 CDM 72,252) hapa na uchakachuaji ulioafanyika ni wa kupunguza kura za Dr. Slaa kwa Takriban 8,000 na kupunguza za CCM kwa kama 2000 hivi)
Katika Jimbo la Bunda CCM 20,836 CDM 571 (Iliyotangazwa na RO CCM 20,836 CDM 18,445) Tarakimu za Bunda zimerekebishwa katika Taarifa ya mwisho ya NEC. Taarifa hii inaonyesha kuwa Dr. Slaa alipewa kura za Lipumba).
Jimbo la Karatu ni kichekesho zaidi kwani kwa mujibu wa Taarifa ya awali ya NEC iliyonukuliwa na Mwananchi CCM 24,364 CDM 41 (iliyotolewa na RO CCM 24,364 CDM 43,137) Taarifa ya mwisho ya NEC imerekebishwa kufanana na ya RO Karatu.
Tume ilikiri kuwa imekosea Taarifa ya Geita japo hadi leo haijarekebisha Taarifa hiyo.
Hadi leo hii tarehe 19/11 Tume haijatangaza matokeo ya Geita, Tumbe, Tunduru Kaskazini, na Vunjo kwenye Website yake. (Tume ilikiri siku ya kujumlisha matokeo Taifa kuwa Vunjo kulikuwa na Taarifa mbili na ikaamua kutumia ile ambayo haikusainiwa na mawakala na kutumia ambayo haina saini ya mawakala. Ni akili ya kawaida tu kujua kuwa kuna jambo hapo.
Haswaa! Kichwa ndio kitambulisho cha kiwiliwili :teeth:Hata kichwa cha mada ni sehemu ya hoja vilevile......
Mkuu wangu sivyo inavyokwenda... Vituo vya habari au watabiri na hata kambi ya CCM wanaweza kutangaza ushindi pasipo hesabu iliyobakia, wakijua kwamba haiwezi kubadirisha matokeo lakini chombo cha mwisho kama NEC hakitakiwi kutangaza matokeo pasipo kuwa na uhakika kwa asilimia 100 kwa sababu mbali na hizo kura chache zilibakia inawezekana pia kuna makosa ya uhesabuji au makosa mengine yeyote yanaweza kutokea hivyo maadam chombo hiki ndicho cha mwisho na chenye kutoa tamko la mwisho ni lazima wawe na hesabu zote zilizothibitishwa.Siyo lazima NEC wasubiri matokeo ya miji midogo kutangaza matokeo. Kama population ni ndogo, na namba za watu waliopiga kura haziwezi kufikia zile ambazo tayari zimeshapigwa, NEC wanao uwezo kutangaza matokeo bila ya kusubiri hayo matokeo. Is all about Mathematics.
Ulitaka umaanishe nini?Tafadhali ndugu, Dr. Slaa si Dr. Martin Luther King Jr.
Petty kama kawaida. hapa lazima upate support ya Kiranga.Hata kichwa cha mada ni sehemu ya hoja vilevile......
Duh! jamani hivi kweli Bongo tunatumia mfumo gani huu wa demokrasia?..Kama kuna vituo ambavyo hadi leo hesabu yake haijatolewa, inawezekana vipi NEC kumtangaza mshindi hali hawana hesabu kamili ya kura zote zilizopigwa?