Inaniwia vigumu kuwalaumu vijana wa Dar....maana Dar es salaam mwili wako ndio rasilimali yako pekee inayokufanya uishi na kumudu gharama za maisha ya mjini......
Hivyo huna budi kujichunga sana na majanga ambayo yanaweza kukuweka nje ya shughuli zako kwa kipindi kirefu....
Hao vijana wanaoitwa PANYA ROAD huwa wanafanya ambush na huwa wanakuwa wengi kwa wakati mmoja....jaribio lolote la wewe kujirinda au kutaka kukabiliana nao linaweza kukuletea madhara makubwa sana....au hata kugharimu maisha yako.....kwanini ujiweke hatarini ili uonekane shujaa wakati unaweza ukajiepusha na bado ukabaki salama.........
SIKU ZOTE KWA SHUJAA KUNAENDA KILIO......
NB;
Nawashauri vijana kama kuna nafasi ya kuwaepuka au hata kuwakimbia ni vyema kufanya hivyo kuliko kujaribu kuonekana shujaa......labda kama umebananishwa na wanakushambulia na unahitaji kupigania maisha yako..........