Hivi Netanyahu ana elimu kweli, mbona anaendesha nchi kama viongozi wa shithole countries?

Hivi Netanyahu ana elimu kweli, mbona anaendesha nchi kama viongozi wa shithole countries?

6 Pack

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2022
Posts
3,952
Reaction score
8,807
Niaje waungwana

Mtu ukiisoma na kuijadili hii thread kimihemko, na kiitikadi bila kuzingatia uhalisia wa kilichoandikwa, hakika itakuwa ngumu mno kunielewa.

Lakini ukiisoma na kuijadili hii thread kisomi, kiakili na kiuweledi. I'm telling you that itakuwa rahisi mno kwako kuielewa na kufahamu kilichoandikwa.

TWENDE SASA KWENYE MADA 👇

Netanyahu ni mmoja wa viongozi wakubwa ambao wamejipatia umaarufu mkubwa kupitia njia za
1. UKATILI
2. CHUKI
3. VITA
4. MAUAJI YA KIMBARI (hii ni kwa mujibu wa kesi yake huko ICC)
5. NA UFISADI (kwa mujibu wa kesi yake ya ufisadi huko Israel)

Inasemekana jamaa hutumia kichaka cha vita, na migogoro ya kisiasa nchini Israel, kuiba mabilioni ya kodi za walalahoi wanyonge wa kiyahudi, na kwenda kuyaficha Marekani.

Sasa basi kinachofanya nimfananishe Netanyahu na viongozi wa nchi za shithole ni aina mbovu ya uongozi wake. Yani kama kiongozi ameshindwa kutengeneza mifumo ya kujitegemea. Anataka kila kitu wawe wanategemea kutoka Marekani na Ulaya. Huyu ana tofauti gani na kina Ndayishimiye wa Burundi?

A) Viongozi wa shithole countries wana utaratibu wa kukimbilia Ulaya, na Marekani kuomba misaada ya kuendesha nchi zao, Na Netanyahu amekuwa akifanya hivyo hivyo. Muda wa miezi 6 tu ashaenda Marekani mara 2 kuomba hela, dawa na silaha za kupambana na vikundi vya vijana wasiozidi elf 20.

B) Viongozi wa shithole wana utaratibu wa kupeleka watoto wao Ulaya kusoma, kwa sababu ya kukwepa uduni wa elimu katika nchi zao, Netanyahu na yeye hivyo hivyo, mtoto wake anaishi na kusomea huko Miami, Marekani kwa sababu ya kukwepa ubovu wa elimu yao huko nchini Israel. Huyu anaonekana hata akipata ugonjwa wa serious ambao utaonekana kuhatarisha usalama wa maisha yake basi ataenda tu kutibiwa Marekani.

Mtu unashindwa kuelewa ni kina nani ambao huwa wanampa ushauri wa namna hii Netanyahu!!

Ni kwanini wasingemshauri atumie mbinu zile walizotumia wajapan na wachina!

Japan walitumia ukaribu wao na nchi za magharibi kupeleka watu wao Ulaya na Marekani, kujifunza mambo mbali mbali kama vile teknolojia, udaktari na mambo mbali mbali ya kimaendeleo. Baada ya muda wajapan walirudi nchini kwao Japan na kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi nchini kwao, na duniani kwa ujumla. Hadi kupelekea nchi zilizokuwa zinaidharau Japan kuanza kuiheshimu, na kuiogopa kwa teknolojia na maendeleo yao.

Kadhalika China nayo ilipopata mwanya wa kupenyeza watu wao huko Ulaya na Marekani, waliitumia njia hiyo kujifunza mambo ya teknolojia, uchumi, tiba, na maendeleo. Leo hii tunavyoongea China inashika nafasi ya pili kwa uchumi duniani, ikiwa imeziacha mbali nchi zilizotawala dunia kama vile UK, Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi nk.

Tukija kwa India nayo pia haikubaki nyuma kimaendeleo ya teknolojia, uchumi, udaktari nk.

Hizo nchi zote nlizozitaja hapo juu (ukiitoa Israel) zinajitegemea kiuchumi, teknolojia, elimu nk.

Sasa kwanini hawa wanaoitwa the "chosen ones" washindwe akili, na maarifa na nchi hizo nlizozitaja hapo juu? Wataendelea kuwa wanaenda Marekani, na Ulaya kuomba misaada ya kijeshi, madawa na hela za kuendeshea serikali mpaka lini?

Why wasitumie hela za misaada hiyo kujenga taasisi imara za kujisimamia, na kujitegemea kama China na Japan?

Wale wasomi wao wanaoishi Ulaya na Marekani, wanaogopa nini kurudi nyumbani kwao kuijenga nchi yao, na kuiendeleza kama vile walivyofanya wachina na wajapan?

Hata waajemi (Iran) ambao wana vikwazo vya kiuchumi, na kijeshi kwa zaidi ya miaka 50, hatujawahi kuwaona wakikimbilia Marekani, UK, Ufaransa, China, Russia au Uturuki kuomba hela za kuendesha serikali, pamoja na silaha za bure.

Sasa kulikoni Israel asiokuwa na vikwazo?

Wanakwama wapi?

Na Netanyahu ana mpango gani kwa future ya baadae!

Maana kuna msemo unaosema kuwa "Mtegemea vya ndugu, hufa masikini".

Ni aibu kwa Netanyahu kwenda Marekani mara 2 kwa muda wa miezi 6, bila kiongozi mkuu wa Marekani Donald Trump kufanya hivyo kwa Israel.

Hili lingefanywa na kiongozi wa nchi ya shithole kila mtu angemcheka, ila kwa Netanyahu watu wamekaa kimya mpaka wenye akili tumeamua kumsanua.
 
Hata jana alikua huko, et anampendekeza Trump na tuzo ya amani.
Netanyahu mjanga, mnafiki na mlaghai sana. Ni kama tu Motto ya Mossad inavyosema kuwa by the way of deception they shall rule the world.
 
Mayahudi ndio matajiri pale marekani, ndio wanaendesha serikali, sanuka.
Propaganda uchwara... Unaendeshaje serikali na uchumi wa nchi nyingine, huku nchi yako ikiomba msaada kwa nchi zingine kama vile Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi nk?

Why wasitumie utajiri huo katika nchi yao kama vile China, Japan, India nk?
 
Propaganda uchwara... Unaendeshaji serikali na uchumi wa nchi nyingine, huku nchi yako ikiomba msaada kwa nchi zingine kama vile Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi nk?

Why wasitumie utajiri huo katika nchi yao kama vile China, Japan, India nk?
Wewe hata ueleweki mkuu, matajiri wakubwa pale marekani ni mayahudi, Hao Jamaal wanapesa na Wana uwezo wa kuendesha serikali wanavyotaka, wewe ona mambo kama unavyoona.. Kuna muda ujinga ni baraka..
 
Back
Top Bottom