Hivi, ni kipi Kenya inaweza ikapoteza tukifungiana mpaka na Tanzania


Hii haijajibu swali langu maana ni yale yale mliaminishwa kwamba Kenya yote inamilikiwa na wazungu, hilo tulishalijadili tukajaribu kuwaelimisha lakini kwa mlivyo mabumbumbu hamkuelewa. Ni kama tusemavyo utajiri asilimia 70% wa Tanzania umemilikiwa na wahindi na waarabu ambao ndio kumi bora kwa wanaoimiliki Tanzania, maana humo Watanganyika weusi hawana lolote, labda mmoja tu yule Mchagga bwana Mengi, wengine wote kajamba wa Manzense.
 

Leta takwimu za malighafi kiasi gani ambacho kinatoka Tanzania, na kama kweli kuna asilimia kubwa ya maliighafi inahuska kwenye mauzo ya bidhaa zetu, ina maana tukifungiana mipaka, na nyie pia mtaishia kujamba huko maana zitaozea huko huko.
Hayo ya madini hayana mashiko maana yanawanufaisha Wakenya na Watanzania wachache, hivyo sio kitu cha kupoteza muda kukijadili humu.
 
Unajua maana ya 10% au unaropoka Tu? Kama vipi Ondokeni tuuu na dharau zenuu..

Ndio nataka nijuzwe hiyo 10% ni kiasi gani cha kusababisha tuangamie tukiikosa.
 
Mshauri Mh. Kenyatta afunge tu huo mpaka hakuna jinsi.
 
mleta mada ombea hilo lisitokee maana kila mmoja atapata hasaha kwa kiasi chake na watakao umia ni raia wengi.Kikubwa ambacho kinatakiwa ni kuondoa tofauti zetu hasa kwa viongozi wetu ili kuendelea kudumisha urafiki ambao kwa sasa unaonekana upo kimya kimya uwe wa wasi ili kudumisha biashara zetu ktk ukanda wetu.
Hata kama faida ni ndogo au kubwa kwa kila upande kutegemeana lkn umoja ni muhimu kudumishwa na tusiombee utengano hata siku moja
 
Kwa ufupi kama kusipokuwa na tatizo la upungufu wa mvua Tanzania ina uwezo wa kutoa guarantee ya food security kwa population yote ya East Africa community kitu ambacho nchi ya Kenya haiwezi kufanya kufanya hivyo kujitosheleza kwa chakula yenyewe hata kwa mwaka mmoja rejea scenario ya mwaka jana baada ya Tanzania kukaza kutouza mahindi yake nje nchi ya Kenya walipata taabu sana mpaka kulazimika kufanya Importation ya mahindi kutoka nchi nyingine. Kwahiyo jeuri inayopata Tanzania kutokana na mauzo yake ya bidhaa za chakula kwa nchi jirani ndiyo inawapa nguvu ya manunuzi(purchasing power) watanzania walio wengi rejea wananchi wengi wa Tanzania wanajishughulisha na kilimo. Kitu ambacho ni tofauti na Kenya uchumi wa Kenya unategemea viwanda vya kati ambavyo soko lake kuu ni Tanzania kwa bidhaa kama Kiwi, Maziwa n.k. na profit inayopatikana kwa viwanda hvy hairudi kwa wananchi wa Kenya but owners wa hvy viwanda ambavyo asilimia kubwa ni Foreigners hali inayowapelekea wananchi wengi wa Kenya kuwa na Maisha duni na kuwa watumwa ndani ya nchi yao. Rejea hata hy KQ uliyoitaja fuatili share holders wa shirika hilo ni wakina nani tofauti na Air Tanzania.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa jinsi Al Shaabab wanavyowachapa, fungeni mipaka halafu muone! All ur access to SADC countries will evaporate also! Tourism package will also seize! Mlifunga 1977 mpaka Leo mnalilia Bolongoja gate!
 
Malighafi nyingi mnazopata kutoka tz ni za wizi na madini ya wizi

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Bado hili halijajibu swali langu maana mahindi ni yenu, ardhi ni yenu lakini hela za kununua ni zetu, hamtupi kama msaada, mwaka mlioshindwa kuzalisha mahindi ya kujitosheleza, kwa njaa zenu na chuki mkazuia kutuuzia, lakini kwa sababu tulikua na hela zetu, mataifa mengine yakapiga hodi na kutuuzia tena kwa kutubembeleza, hiyo inaitwa jeuri ya kuwa na hela.
Swali langu lilikua, ikitokea tumefungiana, ni kwa jinsi gani Kenya itaangamia, leo hii tumeona mkifungia vitu ambavyo huwa tunawategemea navyo, na bado hatukuangamia, hayo mahindi kuna mataifa mengi tu yanazalisha na mazao yanaozea kwenye maghala kwa kukosa wanunuzi, hivyo ukiwa na jeuri ya hela hutababaishwa.

Ni kweli tukifungiana mipaka kuna jinsi tutaumia, na sio mara ya kwanza kufungiana mpaka, lakini na nyie pia cha moto mtakiona huko huko na umaskini wenu, chochote mnachotuuzia kitaozea huko huko.
 
Malighafi nyingi mnazopata kutoka tz ni za wizi na madini ya wizi

Sent using Jamii Forums mobile app

Nimekuambia hayo ya wizi yanawanufaisha wachache, maana Wakenya hawaji na kuiba wenyewe, lazima kuna Watanzania wanashirikiana nao, hivyo ni wachache tu wataona cha moto kama ikitokea tumefungiana, biashara za magendo hunufaisha mabwenyenye wachache, haswa kwenye nchi yenu hiyo shamba la bibi inaliwa sana na Wasouth, Wachina, Wahindi na Waarabu.
Watanganyika wengi ni makajamba wa kukaa pembeni wakiona mkiliwa na mabeberu, kuna siku mliahidiwa noah kwa kila Mtanzania ila ikaishia stori.
 

Binafsi siombei, lakini kwa utawala wenu wa leo mumezidisha chuki sana dhidi ya Kenya hadi sioni nafuu gani ya muungano ambayo inafaa kuruhusu yanayotendeka leo. Ni kweli tukifungiana tutaumia sote, kuna asilimia kiasi fulani itaumia pande zote mbili, lakini Watanzania wengi wameminishwa na kudanganywa kwamba wao hawana lolote la kupoteza na ndio inawapa jeuri ya kuendekeza chuki.
 
Wewe ndiyo ulete takwimu from reliable sources, acha kutapika sukuma wiki.
 
Mshauri Mh. Kenyatta afunge tu huo mpaka hakuna jinsi.

Ningependa wanaomshauri rais Uhuru wapitie huku ili watuambie kipi tutapoteza na kuangamia iwapo tutafungiana.
 
Wewe ndiyo ulete takwimu from reliable sources, acha kutapika sukuma wiki.

Mimi nimeomba wataalam wa uchumi waniambie tutaangamia vipi ikitokea tumepeana talaka na Tanzania, sasa kama wewe mtaalam, tiririka na takwimu zako tuone jinsi gani tutakosa hewa na kufa.
 
Samahani kwa kutoka nje ya mada, naomba kujua una asili ya kutoka mji gani wa Kenya?
Maana una dalili zote za kuwa mTz.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Keny, ndio taifa lenye deni kubwa kuliko yote EAC. Yaani deni la kenya ni sawa na robo y auchumi wa Tz, halafu deni lenyewe halilipiki, mchina anachukua Kenya yake. Bora tu tufunge mpaka
 
Kule kuanza kufikiria tu kufunga mpaka ni mawazo potofu. Hilo lije tu panapokuwepo na mgogoro halisi ambao umeshindikana kutatuliwa. Mbali na hayo, kama kunakuwepo na kutoelewana hapa na pale, hiyo ni kawaida ya maisha. Tutatue hilo tatizo na kuendelea mbele. Hata kwenye familia kunakuwepo kutofautiana kati ya mume na mke au mzazi na mtoto. Huwezi kuanza kufikiria talaka au kufukuza mtoto mpaka hapo kila kitu kingine kitakapokuwa kimeshindikana.
 
Based on this, you are trying to tell us something. Not otherwise.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…