Hivi ni kwanini Baraza Kuu la CCM liliwaita na kutaka kuwahoji akina Membe na kumwacha Musiba?

Hivi ni kwanini Baraza Kuu la CCM liliwaita na kutaka kuwahoji akina Membe na kumwacha Musiba?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Kwenye sheria ni lazima unapohitaji haki itendeke uhusishe pande zote ili uujue ukweli na ufanye uamuzi usiopendelea upande mmoja

Nimesikia kwenye kikao cha baraza kuu la CCM kilichomalizika siku chache zilizopita, huko Mwanza, kuwa kimeamua kuwaita akina Bernard Membe, Abdurahman Kinana na Yusufu Makamba kuwahoji kuhusu tuhuma zinazowakabili za kuvuja kwa sauti zao kwenye audio clips

Nina maswali machache ninataka kuwauliza hao wajumbe wa NEC walioazimia azimio hilo

1. Ni kwanini muwaite akina Membe na kutaka kuwahoji wakati mmeacha kumuita Musiba, ambaye ndiye "root cause" ya haya yote yanayotokea ikiwa mnatafuta haki itendeke kwa kusikiliza pande zote za mgogoro huo?

2. Hivi "privacy policy" haipo tena nchini Tanzania, ambapo mtu analindwa kisheria katika maongezi yake ya faragha??

3. Mnawezaje kuwa nyinyi baraza la CCM kuwa ndiyo waamuzi wa kesi hiyo, wakati mnajua kabisa kuwa mnakiuka "principle" kuu ya "natural justice" inayosema "You can't be a judge in your own case"

4. Hivi kwa kitendo kilichofanywa na baraza la CCM, siyo kinazidi kuthibitisha shutuma za wananchi walio wengi kuwa huyo Musiba anakingiwa kifua na anatumwa na mtu mzito sana ndani ya nchi hii kutoa hizo shutuma zake zisizokuwa na ushahidi??

Hili Taifa kama linafanya maamuzi yake kwa ubaguzi wa waziwazi kabisa, katika kuwashughulikia wahusika wake linalowatuhumu, kama huu tunaouona sasa tujue kama Taifa tupo hatarini kusambaratika

Naomba nijibiwe kwa hoja, wala si kwa kutoa povu
 
4. Hivi kwa kitendo kilichofanywa na NEC ya CCM, siyo kinazidi kuthibitisha shutuma za wananchi walio wengi kuwa huyo Musiba anakingiwa kifua na anatumwa na mtu mzito sana ndani ya nchi hii kufanya huo upuuzi wake??
[emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144] Mystery,
 
Kwani Msiba ameshiriki kwenye ule waraka na zile audio clips zenye lengo la kudharirisha Chama na Mwenyekiti wake?
 
Kwanini CCM
1. Inavunja katiba? Kuingilia mawasiliano ya watu binafsi.

2. Kwanini inafanya unyanyapaa kwa wanachama wake?

A) Musiba Haitwi kuhojiwa

B) wazee wanaitwa

Waitwa wote A) na B) hapo juu haki intendee.

3. Kwanini ccm hairuhusu kukosolewa?

A) kuambiwa ukweli ni kosa?

B) kushauliwa nikosa?
 
Musiba sio mwanachama unapo mwita unamwita kama nan?
Hajanonesha uthibitisho kuwa yeye ni ccm hao wengine ni zaid ya wqnachama manake kwa nyakati zao qashakuwa viongozi wa kubwa ndani ya chama na selikal

Sent using Jamii Forums mobile app

Mwenyekiti wa chama ni amilijeshi mkuu

Waziri wa mambo ya ndani ni kada wa ccm

Je ccm inabariki uvunjifu wa sheria ?

Je ccm inaruhusu wanachama wake kutukanwa na kuzushiwa ?

Je ccm inaruhusu wanachama wake kudhalauliwa na kudhalilishwa?

Ikiwa sheria ipo wazi kwanini waziri hawezi kumshughulikia Musiba?

Musiba yupo juu ya ccm kuliko wanachama wa ccm?
 
Musiba sio mwanachama unapo mwita unamwita kama nan?
Hajanonesha uthibitisho kuwa yeye ni ccm hao wengine ni zaid ya wqnachama manake kwa nyakati zao qashakuwa viongozi wa kubwa ndani ya chama na selikal

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama siyo mwanachama aligombeaje ubunge kule Mwibara kwa tiketi ya CCM na kubwagwa na Kangi Lugola?!!
 
adolay,
Ndiyo kitu kinachoshangaza, ni kwa vipi huyu mtu aitwaye Musiba aruhusiwe kuwatukana na kuwadhalilisha viongozi mbalimbali bila kuchukuliwa hatua yoyote??

Ndiyo maana wananchi wengi wanaamini kuwa huyu Musiba anakingiwa kifua na kutiwa kiburi na mtu mmoja mzito sana ndani ya nchi hii
 
Back
Top Bottom