Hivi ni kwanini lakini?! Wanaume naombeni majibu

Dena Amsi

R I P
Joined
Aug 17, 2010
Posts
13,080
Reaction score
4,273
Najiuliza.................

Ni kweli mpango wa kando a.k.a nyumba ndogo husaidia kupunguza stress za nyumbani kwako??

Kama si kweli mbona unakwenda kumsimulia mpango wa kando mambo/matatizo yako na mkeo???

Kama ni kweli mbona humuoi huyo mpango wa kando akawa mke mdogo/wa pili ili hizo stress za home uzimalizie bila kificho wajameni???

Najiuliza sana sipati majibu kwanini uende kumueleza matatizo/shida/ugomvi wako na mkeo huyu mwanamke wa nje tena unaomba akupunguzie stress?? Eeehhh??

Yaani unakutana na kimpango wa kando kinakujua kuliko eeeeehhhhh wajameni.......................

Najua Asprin Dark City Mr Rocky Erickb52 na wengineo mtanipa majibu NISAIDIENI TAFADHALI
 
Last edited by a moderator:
Ni kisingizio tu. Kama kweli walikuwa na nia ya kupunguza stress za nyumbani wangejaribu kusuluhisha mambo huko kuliko kuenda kujiongezea sababu nyingine ya kuharibu mahusiano na nyumba kubwa.
 
.....hata kibusati cha mlangoni kinajua taka za viatu vilipotokea.

Relax.
 
Last edited by a moderator:
ushamba tu.kama vipi ahamie huko kabisa
dadangu shem wangu mbona ananiaibisha hivi jameni?
relax jipende na wanao,maisha sio lazima mwanaume bwana.utakuja kufa bure unawaacha wenyewe wanafwaidiii
 
Kiukweli mwanaume anayetoka nje halafu akadiriki kuelezea siri za mkewe huyo hafai kabisa
.
 
Huwa wanajaribu ku win confidence za nyumba ndogo ili waone wanajaliwa.
Ila nikipata kile nakitaka natimua vumbi, ndo maana hatuwaowi, tunawatumia kupata ladha tofauti.
 
Kiukweli mwanaume anayetoka nje halafu akadiriki kuelezea siri za mkewe huyo hafai kabisa
.
ila wanaume wengi ndo zenu,hata mkitongoza tu mnaponda wake zenu .oooh sijui nilimuoa wa nini? oooh nililazimishwa na wazazi...oooh nilikuwa mdogo ptuuuuuuu! mi waume za watu ptuuuu wazushi sana
 
ushamba tu.kama vipi ahamie huko kabisa
dadangu shem wangu mbona ananiaibisha hivi jameni?
relax jipende na wanao,maisha sio lazima mwanaume bwana.utakuja kufa bure unawaacha wenyewe wanafwaidiii

Acha tu yaani kimpango wa kando kinanikasirisha sana
 
Huwa wanajaribu ku win confidence za nyumba ndogo ili waone wanajaliwa.
Ila nikipata kile nakitaka natimua vumbi, ndo maana hatuwaowi, tunawatumia kupata ladha tofauti.

Hapo kwenye bluu inawezekana ni kweli aisee
 
ila wanaume wengi ndo zenu,hata mkitongoza tu mnaponda wake zenu .oooh sijui nilimuoa wa nini? oooh nililazimishwa na wazazi...oooh nilikuwa mdogo ptuuuuuuu! mi waume za watu ptuuuu wazushi sana

Wajinga sana hawa eti ooohh kwanini hatukukutana mapema kabla ya huyu mwanamke sijui ni nini "Bure Kabisa"
 
Kucheat nje ya ndoa, iwe kwa mwanamme au mwanmke ni tabia na wala sio matatizo yalipo ndani ya ndoa, kuna ndoa nyingi ndani zina matatizo lakini kwa sababu wahusika hawana tabia ya kucheat, zinaendelea na wala hawatoki nje ya ndoa.
 
Acha tu yaani kimpango wa kando kinanikasirisha sana
sasa sis wangu yaani na ujanja wako wote ,ndoa inakushinda.realy i feel so sory for you my dear?
sali basi jamani? au wapi unakosea?
hebu tuambie lifestyle yenu ,nataka uwe happy bwana daah!
 
ila wanaume wengi ndo zenu,hata mkitongoza tu mnaponda wake zenu .oooh sijui nilimuoa wa nini? oooh nililazimishwa na wazazi...oooh nilikuwa mdogo ptuuuuuuu! mi waume za watu ptuuuu wazushi sana
h ha haaaaaa, sasa my dear wasipowadanganya hivyo watawapataje?
yaani mtu aje akuambie naishi kwa raha mustarehe na mke wangu ila nataka nikutumie tu mara mojamoja nikijisikia kubadilisha mtajisikiaje?
lazima akuweke kwenye anga za kukufanya ujione una thamani machoni mwake ili apate anachotaka, na ndo maana hamwachi mkewe sababu anajua hapo anapita tu........
ukiwasikiliza vizuri hao watu story nyingi huwa ni za uongo, ni gia tu ya kumpata mdada. Smile hii nimeandika kama nakuambia wewe lakini siyo..... ni kwamba tu nimeshindwa niiwekaje, lakini inamaanisha wale wanaofwatwa kuwa mpango wa kando......
 
Last edited by a moderator:
Kucheat nje ya ndoa, iwe kwa mwanamme au mwanmke ni tabia na wala sio matatizo yalipo ndani ya ndoa, kuna ndoa nyingi ndani zina matatizo lakini kwa sababu wahusika hawana tabia ya kucheat, zinaendelea na wala hawatoki nje ya ndoa.

Ukishacheat ujue lazima kuna shida/tatizo huwezi kucheat kama hakuna matatizo. sijazungumzia Tabia hapa
 
sasa sis wangu yaani na ujanja wako wote ,ndoa inakushinda.realy i feel so sory for you my dear?
sali basi jamani? au wapi unakosea?
hebu tuambie lifestyle yenu ,nataka uwe happy bwana daah!

Hakinishughuli kivileeeeeee ila ni cha mtaani ndo shida inakuja lazima nitakiona nishajipanga zangu toka zamani sana hata mwenyewe anajua sishughuliki nae
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…