hapa nazungumzia nilichoambiwa na huyo dada, alitembea nae kisa alitaka hiki na kile, na jamaa alimuahidi kumfanyia hiki na kile,tamaa mbele, na hakufanyiwa hata kimoja,labda kama alimchuna za mfukoni tu, nilimtesa yule dada mpaka nikaridhika na nafsi yangu mwenyewe, alivyokuwa ananitobolea masiri yao ndio nilikuwa nakasirika zaidi, na jamaa home anatubu yale yale niliyoambiwa, hahah mke mtamu ati, aliomba msamaha akiusindikiza na haleluya kuu, yule dada alikuwa mchumba wa mtu, nilimfata mpaka yule mchumba wake ofisini na nikamcal mdada nikamwambia nipo kwa mume wako mtarajiwa, nikuharibie? aliteseka yule dada, alilia mpaka basi, natembea na picha za mchumba wake kama bible vile kwenye pochi yangu,hahaha kila mmoja nilimtesa kivyake,tukija kwenye ishu ya performance hapo ndio ntajua mwanaume nilienae anaweza hata kuombwa na wanaume wenzie akawapa pia kisa "wanajiweza" hapo tena ni kesi nyingine na naomba isinifike mana atanitia kinyaa cha milele, kwamba anatumika na wanaojiweza kisa performance yake? uuuuh, ipitie mbali kwa sasa.