FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 40,956
- 47,046
Hii ni moja ya michango bora katika Bunge linaloendelea sasa. Hamna gari inayostahili kulipia road licence kama haipo barabarani, cha ajabu wamiliki wenye magari yasiyotembea kwa ubovu ama ajali yangali yanachajiwa road licence na penalty juu na zaidi ya yote hata kama gari langu ni zima ila siko barabarani kwa muda tajwa ya nini nilipie road licence?
Wenye mamlaka jiongezeni kidogo tu, hamna gari itakayokuwa barabarani bila nishati na kadiri mtu atakavyotumia barabara ndivyo jinsi itakovyombidi kununua nishati husika na ndivyo jinsi atakavyolipia barabara na probably kipato cha serikali kitaongezeka zaidi.
Hongera mtoa hoja, hongera wabunge wote mwitikio wenu tumeuona, kazi kwenu serikali!!
=====
Serikali imeahidi kuifanyia marekebisho sheria inayoagiza tozo ya umiliki wa vyombo vya moto (road license) ili kuondoa kero kwa wananchi.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Ashatu Kijaji amesema hayo bungeni leo (Ijumaa) alipojibu swali la Dk Raphael Chegeni aliyetoa pendekezo hilo ili kodi hiyo iendane na matumizi halisi ya vyombo vya moto barabarani.
"Tozo hii ipo kisheria. Serikali imesikia mapendekezo ya wabunge na itaangalia namna nzuri ya kuboresha ukusanyaji wa mapato hayo," amesema Dk Kijaji.
Wabunge wengi, akiwamo Spika wa Bunge Job Ndugai wamependekeza kufutwa kwa kodi hiyo inayowaathiri zaidi walioegesha magari kwa muda mrefu kutokana na ubovu au ajali.
Umenena sana hongeraKwa style hii, yule atakaetumia barabara zaidi ndie atakaelipa zaidi, sio mtu unatumia gari mara moja kwa mwaka lakini ulipe sawa na mtu aliesababisha foleni kila siku mwaka mzima! Pia itaindoa usumbufu wa kulipa na kubandika mastika pamoja na kusimamishana eti ukaguzi wa stika, ni harassment kwa kweli.
Atakaetumia barabara au atakaetumia mafuta mengi ndio atalipa zaidi? Najua unajiuliza kivipi? Ni hivi toyota passo akiweka lita 10 approximately 20,000 atatembea zaidi ya 100km.Kwa style hii, yule atakaetumia barabara zaidi ndie atakaelipa zaidi, sio mtu unatumia gari mara moja kwa mwaka lakini ulipe sawa na mtu aliesababisha foleni kila siku mwaka mzima! Pia itaindoa usumbufu wa kulipa na kubandika mastika pamoja na kusimamishana eti ukaguzi wa stika, ni harassment kwa kweli.
Una hoja ila matumizi ya mafuta ni zaidi ya vyombo vya moto; kuna generator, chain saw nk.Kwa style hii, yule atakaetumia barabara zaidi ndie atakaelipa zaidi, sio mtu unatumia gari mara moja kwa mwaka lakini ulipe sawa na mtu aliesababisha foleni kila siku mwaka mzima! Pia itaindoa usumbufu wa kulipa na kubandika mastika pamoja na kusimamishana eti ukaguzi wa stika, ni harassment kwa kweli.
Wazo zuri sana bro lkn bei ya mafuta haitabiriki, soko lapanda na kushuka duanianiKwa style hii, yule atakaetumia barabara zaidi ndie atakaelipa zaidi, sio mtu unatumia gari mara moja kwa mwaka lakini ulipe sawa na mtu aliesababisha foleni kila siku mwaka mzima! Pia itaindoa usumbufu wa kulipa na kubandika mastika pamoja na kusimamishana eti ukaguzi wa stika, ni harassment kwa kweli.
Ukisema road licence ilipiwe kwenye mafuta maanaake kwenye magari ya biashara ni kwamba road licence itakuwa inalipwa na walaji kama ni gari ya abiria hao abiria ndo watakaolipa hiyo road licence na kama ni gari ya mizigo mtumiaji wa hiyo mizigo ndo atakuja kulipa hiyo road licence.Kwa style hii, yule atakaetumia barabara zaidi ndie atakaelipa zaidi, sio mtu unatumia gari mara moja kwa mwaka lakini ulipe sawa na mtu aliesababisha foleni kila siku mwaka mzima! Pia itaindoa usumbufu wa kulipa na kubandika mastika pamoja na kusimamishana eti ukaguzi wa stika, ni harassment kwa kweli.
Ukisema road licence ilipiwe kwenye mafuta maanaake kwenye magari ya biashara ni kwamba road licence itakuwa inalipwa na walaji kama ni gari ya abiria hao abiria ndo watakaolipa hiyo road licence na kama ni gari ya mizigo mtumiaji wa hiyo mizigo ndo atakuja kulipa hiyo road licence.
Mfano mtu hana hata uwezo wa kununua baiskeli lakini akienda kununua nyanya ya kupikia anawekewa na gharama za mafuta(road licence) yaliyosafirishia hiyo nyanya.
Pia kumbuka kuna generators, mashine za kupump maji, mashine za kusaga mahindi huko vijijini e.t.c
Mimi naona hiyo itakuwa ni njia ya wenye vyombo vya biashara kuhamishia hizo gharama kwa mwananchi wa kawaida directly, manaake sasa hivi inawezekana bado mwananchi wa kawaida ndo analipia ila indirectly.
Bila shaka yo yote hii ni hoja murua sana waziri wa fedha anapaswa kuizingatia katika bajeti ijayo!!Kwa style hii, yule atakaetumia barabara zaidi ndie atakaelipa zaidi, sio mtu unatumia gari mara moja kwa mwaka lakini ulipe sawa na mtu aliesababisha foleni kila siku mwaka mzima! Pia itaindoa usumbufu wa kulipa na kubandika mastika pamoja na kusimamishana eti ukaguzi wa stika, ni harassment kwa kweli.
Ni njia mojawapo nzuri sana na nchi nyingi inatumia.Kwa style hii, yule atakaetumia barabara zaidi ndie atakaelipa zaidi, sio mtu unatumia gari mara moja kwa mwaka lakini ulipe sawa na mtu aliesababisha foleni kila siku mwaka mzima! Pia itaindoa usumbufu wa kulipa na kubandika mastika pamoja na kusimamishana eti ukaguzi wa stika, ni harassment kwa kweli.
Swadakta!
- Maafisa wa mapato na usalama barabarani wanapoteza muda mwingi kukagua stika barabarani wakati kama road license ingelipiwa kwenye mafuta wao wangeendelea na majukumu yao ya msingi yenye ulazima wa kufanyika manually, jambo la msingi hapa wangepaswa kusimamia na kuhakikisha kila kituo cha mafuta kinatoa receipt
- Yapo magari mengi ambayo hayalipii hiyo road licence kutokana na kufanya kazi pembezoni mwa miji ambako hao wakaguzi hawafiki, na mengine yanatembea usiku wakati hao maafisa hawako barabarani
- Kuna magari ya serikali yalishauzwa lakini bado yana namba za serikali, hayalipiwi road license na bado yanafanya kazi mitaani, mfano mmoja tu nilipata kuona lori moja lina namba za serikali na mlangoni limeandikwa Shule ya Sekondari Mazengo, japo sina uhakika kama hiyo shule bado ipo
- Kwa utaratibu wa kulipia kwenye mafuta mapato yangeongezeka kwasababu, kila chombo cha usafiri na mitambo kama matrekta yangechangia pato la taifa, kwa sasa hivi, bodaboda na bajaji hazilipii kabisa, na zipo nyingi na zinatumia barabara kwa kiasi kikubwa,
Ni kweli kabisa na ndio njia iliyotumika miaka ya nyuma, INA maana serikikali itapata mapato mengi kuliko ilivyo sasa. Kila chombo kitachangia, pikipiki, generators, tractors, chain saw, boats, na kadha wa kadha. Sijui ni nani wa kumpa pendekezo hilo lipitishwe.