Hivi ni kwanini siku hizi watu hawapigani mitaani kama miaka ya 1980s?

zile zilikua zinanaitwa enzi za ujinga,leo mtu anasifiwa pesa sio mabavu tena.nakumbuka hata mitaani kwetu walikua wanavuma zana wenye kupiga kumi na mabavu sana ila sasa watu tumeelimika maendeleo kwanza ndoo heshima hata kama mtoto utaitwa mzee,kitu mpungaaa.
 
heeeeee, boss hapo kuanguka na 10 kuzimama na 20 umekaanga mbuyu,,,,,hahahahaaaaa
 
Zamani Elimu haikua ya kutosha....wapumbavu walikua wengi kuliko wastaarabu...
Kadri siku zinavyokwenda wapumbavu wanakufa, wanapungua au wana badilika na kuwa werevu...ndio maana hamna kupigana pigana

Elimu muhimu Sana.
 
zamani watu walikuwa hawapelekani kwenye vyombo vya sheria kama sasa hv. Mambo yalikuwa yanaishia uwanja wa mapambano. Kwasasa utamtajirisha mtu bure. Halafu ustaarabu umeongezeka kwa watu wengi.
 
This is childhood thing hapo sio watu wazima wanaozungumziwa
 
Kipindi hicho walikua wanakula ugali wanashiba,sasa kizazi hiki cha chips yai na andazi nguvu za kupigana wanapata wapi.

Pia bangi za zamani zilikua og yani wahuni walikua wahuni kweli kweli.

Hiphop ngumu,sio sikuhizi mtoto wakiume anaimba nyimbo zote za zuchu.

What a loss generation
 
Ngumi nimepigana Sana Ila mapambano Kati ya sabini niliohudhuria mtaani kwetu hasa ukizingatia nilikuwa mwingi wa hasira na mwepesi kuzikunja ,kiukweli nakumbuka ni mawili tu ndiyo nilishinda Ila mengine nilichezea kipigo haswa uzuri Sina alama ya kuikumbuka kuwa nilikung'utwa
 
Vijana wengi wa 2000 afya hawana wapo wembamba kama askilimu au mnyoo nguvu za kupigana zitoke wapi kutembea tupu kijana kama zombi sijui kumetokea Nini Kwa vijana wa sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…