Hivi ni kwanini tunasema 'juu mbinguni' na 'chini motoni'?!

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Kwa umbo la Dunia jinsi lilivyo, hapo uliposimama wewe, muelekeo wa kichwa chako ndio unapaita juu, na muelekeo wa miguu yako ndio unapaita chini. Lakini, kwa alie upande wa pili wa dunia, kule wewe unapopaita chini, kwake yeye ndio anapaita juu,na kule wewe unapopaita juu, yeye huko ndio muelekeo wa miguu yake hivyo anapaita chini. Kwahiyo in principle hapa ulimwenguni hakuna juu wala chini bali ni endless in all directions possible! sasa kama hakuna juu wala chini maana yake kauli ya 'Juu mbinguni' vilevile haipo, halikadhalika mbinguni kwenyewe.

images

DON FRANCIS
 
Ni msemo tu : Juu kama ulivyosema ni kila muelekeo au directions na infinite distance yani hakuna kikomo na anga imtapakaa poote na hizi ndio sifa za mbingu na uwezo wa Mwenyezi Mungu. Chini kuna kikomo na ni mahali tunapa kanyaga, kitu unacho kikanyaga ni cha hali duni na dhaifu
 
Inaaminika mbinguni sio duniani hapa ni outer space ambapo kwenda you must go up...

Na jehanam inaaminika ni kwenye inner core of the planet ambapo kwenda you must go down..
 
Hayo maneno kwamba mbingu iko juu na moto uko chini uliyapata wapi? i mean imani gani? or whatever.

Na kwanini mbingu na moto umevihusisha na umbo la dunia?
 
Ni uoga tu wa binadamu, hata huko motoni sijui mbinguni sidhani kama kupo.
 
je unakataa chini hakuna moto ??
 
Inaaminika mbinguni sio duniani hapa ni outer space ambapo kwenda you must go up...

Na jehanam inaaminika ni kwenye inner core of the planet ambapo kwenda you must go down..
Huko motoni inaenda roho au mwili, kama ni roho je roho inangozi? na kama haina ngozi huo moto unakuunguzaje?!
 
Nakubali. je huko motoni inaenda roho au mwili, kama ni roho, je roho ina ngozi? na kama haina je huo moto unakuunguzaje?!

kwani hii mada inahusu nini mbona ni mada juu ya mada ??
 
Kwa umbo la Dunia jinsi lilivyo, hapo uliposimama wewe, muelekeo wa kichwa chako ndio unapaita juu, na muelekeo wa miguu yako ndio unapaita chini. Lakini, kwa alie upande wa pili wa dunia, kule wewe unapopaita chini, kwake yeye ndio anapaita juu,na kule wewe unapopaita juu, yeye huko ndio muelekeo wa miguu yake hivyo anapaita chini. Kwahiyo in principle hapa ulimwenguni hakuna juu wala chini bali ni endless in all directions possible! sasa kama hakuna juu wala chini maana yake kauli ya 'Juu mbinguni' vilevile haipo, halikadhalika mbinguni kwenyewe.

images

DON FRANCIS

Kwa nini unaziamini hizi principles ??
ushawahi kufanya uchunguzi au unaandika walioandika watu ??
 
Maisha ya binadamu yametawaliwa na hisia kuliko ufahamu kwa kiwango kikubwa. Na kuhusu uwepo wa juu kama "mbinguni" na chini kama "motoni" bado ni nadharia iliyojikita katika uzio wa DINI, ambayo haiwapi nafasi waamini wa DINI husika kuweza kuchanganua yaliyomo vitabuni.

chini kuna moto au hakuna ?
 
Kwa nini unaziamini hizi principles ??
ushawahi kufanya uchunguzi au unaandika walioandika watu ??
Nimesema hayo logically kabisa.., its pure logic na wala si imani, kwa hiyo sio kwamba naamini bali nime-deduce hayo logically. sasa wewe unauliza nini sijui..
 
Juu na chini, zinatofautiana kutokana na maumbo. Umbo la mviringo juu na chini yako inasomeka pale uliposimama kwa muda huyo siyo kwa kufananisha na mwingine kasimama wapi kwa muda upi.
 
Kwa umbo la Dunia jinsi lilivyo, hapo uliposimama wewe, muelekeo wa kichwa chako ndio unapaita juu, na muelekeo wa miguu yako ndio unapaita chini. Lakini, kwa alie upande wa pili wa dunia, kule wewe unapopaita chini, kwake yeye ndio anapaita juu,na kule wewe unapopaita juu, yeye huko ndio muelekeo wa miguu yake hivyo anapaita chini. Kwahiyo in principle hapa ulimwenguni hakuna juu wala chini bali ni endless in all directions possible! sasa kama hakuna juu wala chini maana yake kauli ya 'Juu mbinguni' vilevile haipo, halikadhalika mbinguni kwenyewe.

images

DON FRANCIS

Ni kwa sababu wakati Binadamu wameanza kusema ya kwamba Mungu yuko Mbinguni juu (Mawinguni) sayansi ya Dunia na Mbingu na ilikuwa bado haijulikani!
Binadamu alikuwa bado hajaelewa hata kama Dunia Ni Mviringo kwa kifupi alikuwa hajui lolote kuhusu mazingira yake na hivyo hilo neno limebakia tu!
 
To London, the Antipodes is down.

To the Antipodes, London is down.

Habari za juu mbinguni, in fact habari za juu na za mbinguni, ni ujinga uliotokana na kufikiri dunia ni bapa na mungu yupo respectively.

Dunia si bapa na mungu hayupo (kama yupo thibitisha).

Kuamini mungu yupo ni sawa na kuamini kwamba dunia ni bapa.
 
Maisha ya binadamu yametawaliwa na hisia kuliko ufahamu kwa kiwango kikubwa. Na kuhusu uwepo wa juu kama "mbinguni" na chini kama "motoni" bado ni nadharia iliyojikita katika uzio wa DINI, ambayo haiwapi nafasi waamini wa DINI husika kuweza kuchanganua yaliyomo vitabuni.
Kuna dini ambazo hazitoi hizi fursa mkuu?
 
Back
Top Bottom