Japokuwa nipo kinyume na huyu dada na wote mfano wake. Sisi wanaume ambao ni watawala wa wanawake na ni wasimamizi pia,tunatakiwa tutumie marejeo kwa usahihi kuliko kutumia uongo ili kujiweka ju,hakuna haja hiyo kwani sisi ni wasimamizi kwao,anasema Allaha aliye juu :Adamu aliumbwa kwa mfano wa Mungu. Akatawale viumbe wote. Baadaye Mungu akaona hakuna wa kufanana na Adamu. Na ndipo wazo la kumuumba Hawa likazuka.
34. Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayo yatoa. Basi wanawake wema ni wale wenye kut'ii na wanao jilinda hata katika siri kwa kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha wajilinde. Na ambao mnachelea kutoka katika ut'iifu wanasihini, muwahame katika malazi na wapigeni. Wakikut'iini msiwatafutie njia ya kuwaudhi bure. Hakika Mwenyezi Mungu ndiye aliye juu na Mkuu.
35. Na mkichelea kutakuwapo mfarakano baina ya mke na mume basi pelekeni muamuzi kutokana na jamaa za mume, na muamuzi kutokana na jamaa za mke. Wakitaka mapatano Mwenyezi Mungu atawawezesha. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi Mwenye khabari. (an Nisaa : 34 - 35)
Si kweli kwamba Mola alimuumba Adamu kwa mfano wake,sababu Mola hafanani na kiumbe chochote,na si kweli ya kuwa sababu ya kuumbwa Hawa ilikuwa ni baada ya Mola kuona hakuna wa kufanana na Adamu,suala la kuumbwa Hawa lilikuwa ni katika mpango wa Mola,na Mola huwa anafanya mambo kwa wakati na kwa utaratibu,kwahiyo madai yako ni ya uongo sababu yanamtia dosari Mola wetu muumba,mjuzi wa kuumba na kupanga mambo.
Kwahiyo tukiandika tuandike ya kweli na haki hakuna haja ya kutumia uongo kuwajibu wanawake,kwani kuna hoja nyingi za kweli ambazo hakuna Mwanamke mwenye akili timamu awezae kuzipinga ukiona wanazipinga ujue hao hawako timamu.
Tuko pamoja kaka.
Nipo .....